Poleni na majukumu wakuu, nina Jambo la kushare na nyie ushauri wenu utakua wa muhimu sna.
Niliwahi kufanya kazi kweny shirika la umma Kwa muda wa mwaka mmoja na miezi 6 ila ni ajira za mikataba na nikawa nachangia PSSSF around 39000+, na mwajiri anachangia around 118,000+ kwa kila mwezi
Baada ya kupata ajira ya moja kwa moja nje ya shirika Nika terminate nao mkataba mwaka huu mwanzoni
Ivi karibuni nikaenda ofisi za PSSSF na namba ya uwanachama ya kule nilipotoka (shirikani) na kukuta taarifa zangu zipo ila michango haionekani nikawasiliana nao wakawa hawaeleweki kuwauliza wenzangu nao michango yao haionekani toka walipo ajiriwa.
Je, kuna uwezekano wa kupata izo pesa kwa takribani mwaka mmoja na nusu niliofanya kazi au ndo nimepoteza?
Ushauri wenu tafadhar maana huku nilipo michango inaenda kama kawaida na kweny app PSSSF kiganjani ninaiona
Wakuu karibu.