Je, napataje verification badge instagram?

Gai da seboga

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
478
962
Natumai muwazima wana JF

Kumekuwa na wimbi kubwa kwa sasa la viongozi wa kisiasa, wanamuziki na watu mbalimbali maarufu na ata wasio maarufu account zao za mtandao wa instagram kuwa na verification badge yaani kile kitiki cha blue.

Sasa je ni sifa zipi za ziada zinahitajika ili unapoomba hiyo badge instagram uweze kuipata? Ikumbukwe nilishawahi jaribu kuomba kwa kitambulisho cha kura na ata cha Nida lakini nilikosa hiyo badge.

Je kwa waliowahi kupata hii bagde au wenye uzoefu nini hasa cha kuzingatia au nini kiwekwe pale ukiachana na paspot, Nida, kitambulisho cha kura?

NB: kama sifa ni kuwa na followers wengi nimeshuhudia account zenye follower mpaka 2000 zikiwa na hii badge.

Nawasilisha.
images%20(27).jpg
 
Kwanza kwa mujibu wa instagram wenyewe, wanatumia vigezo vingi ila kati ya vigezo walivyoviweka idadi ya followers haipo.

Baadhi ya vigezo kutoka kwenye tovuti yao
1. Account imilikiwe na mtu halisi.
2. Account iwe na post angalau moja.
3. Uwe unafahamika na umma.
4. Watu wawe wanai-search mara kwa mara account yako kupitia instagram na search engine zingine.
5. Account yako itajwe kwenye tovuti na vyombo mbalimbali vya habari.
 
Back
Top Bottom