Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,808
- 6,502
Katika ulingo wa kisiasa, kuna aina ya mwonekano (Telltale signs) ambazo zinaashiria kutokea kwa jambo fulani la kisiasa katika wakati fulani.
Katika nchi kama Marekeni, ili mwanasiasa aweze kuchaguliwa kuliongoza Taifa kama Rais wa USA, lazima ashinde katika state zinazoitwa swing state. Kutokushinda katika state hizo mara nyingi ni tiketi ya kuuona Urais ukiota mbawa.
Kwa nchi kama UK, ili chama kishinde uchaguzi lazima kishinde kwenye sehemu wanazoziita marginal seat. Kutokushinda katika sehemu hizo, ni tiketi ya kutounda serikali isiyotegemea muungano wa vyama(The Coalition)
Tukirudi Tanzania, tunakutana na mwonekano katika maeneo mengi ambapo yanatoa picha ya matokeo ya uchaguzi wa mbunge na Rais.
Katika uchaguzi wa mbunge, Jimbo la Hai limetoa mwonekano unaofanana kuanzia miaka ya 1980's katika kumpata mbunge. Moja ya telltale sign ya Jimbo ya Hai ni kutokuchaguliwa kwa mbunge katika vipindi viwili mfululizo vya uchaguzi mkuu.
Kwa muda wa miaka 30, Jimbo la Hai limekuwa likichagua mbunge katika kipindi kimoja cha uchaguzi na linabadilisha na kuchagua mwingine katika kipindi kinachofuata. Rekodi zinaonyesha kama ifuatavyo;
Mwaka 1985-1990-->Charles Kileo (CCM)
Mwaka 1990-1995-->Prof. Aaron Massawe (CCM)
Mwaka 1995-2000-->Mwinyihamisi Mohamed Mushi (NCCR-Mageuzi)
Mwaka 2000-2005-->Freeman Aikaeli Mbowe (CHADEMA)
Mwaka 2005-2010-->Fuya Godwin Kimbita (CCM)
Mwaka 2010-2015-->Freeman Aikaeli Mbowe (CHADEMA)
Kwa mtiririko huo ninaona kwamba, Freeman Aikaeli kama ataamua tena kugombea ubunge katika jimbo hilo, basi ana kazi ya kupambana na trends and outcome za kisiasa za Jimbo la Hai zitakazopingana na uamuzi wake wa kuwa Mbunge wa jimbo hilo kwa vipindi viwili mfululizo.
Hoja yangu imechagizwa pia na maandiko ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Jenerali Ulimwengu katika gazeti la Raia Mwema wakati akielezea wasifu wa Marehemu Charles Kileo ambaye alikuwa ni Mbunge wa Hai kuanzia mwaka 1985-1990. Jenerali Ulimwengu alisema,
Jenerali Ulimwengu ana maana kuwa, Wazee wa Jimbo la Hai huwa wanamchoka Mbunge baada ya miaka mitano hasa pale anapokataa kuwa tarishi wao.
Hoja ya msingi, Je, Mhe. Freeman Mbowe ataweza kupambana na mzimu kisiasa wa Jimbo la Hai hasa ikichukuliwa kuwa matokeo ya Serikali za Mitaa yameonyesha katika Jimbo la Hai, a tight political race in October General Election.
Nini maandalizi ya Freeman Mbowe katika kukabiliana na mwonekano wa siasa za Jimbo la Hai?.

Jimbo la Hai lina wazee wanaojiona kama waamuzi wa masuala ya kisiasa wilayani humo. Hawa ni wazee wazito, wenye kauli zenye uzani. Wamezoea kwamba mbunge wa jimbo lao anakuwa ni tarishi wa wazee wakwasi wa Machame.