Je, Mzimu wa siasa za Jimbo la Hai utamshukia Freeman Mbowe?

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,502
Katika ulingo wa kisiasa, kuna aina ya mwonekano (Telltale signs) ambazo zinaashiria kutokea kwa jambo fulani la kisiasa katika wakati fulani.

Katika nchi kama Marekeni, ili mwanasiasa aweze kuchaguliwa kuliongoza Taifa kama Rais wa USA, lazima ashinde katika state zinazoitwa swing state. Kutokushinda katika state hizo mara nyingi ni tiketi ya kuuona Urais ukiota mbawa.

Kwa nchi kama UK, ili chama kishinde uchaguzi lazima kishinde kwenye sehemu wanazoziita marginal seat. Kutokushinda katika sehemu hizo, ni tiketi ya kutounda serikali isiyotegemea muungano wa vyama(The Coalition)

Tukirudi Tanzania, tunakutana na mwonekano katika maeneo mengi ambapo yanatoa picha ya matokeo ya uchaguzi wa mbunge na Rais.

Katika uchaguzi wa mbunge, Jimbo la Hai limetoa mwonekano unaofanana kuanzia miaka ya 1980's katika kumpata mbunge. Moja ya telltale sign ya Jimbo ya Hai ni kutokuchaguliwa kwa mbunge katika vipindi viwili mfululizo vya uchaguzi mkuu.

Kwa muda wa miaka 30, Jimbo la Hai limekuwa likichagua mbunge katika kipindi kimoja cha uchaguzi na linabadilisha na kuchagua mwingine katika kipindi kinachofuata. Rekodi zinaonyesha kama ifuatavyo;

Mwaka 1985-1990-->Charles Kileo (CCM)

Mwaka 1990-1995-->Prof. Aaron Massawe (CCM)

Mwaka 1995-2000-->Mwinyihamisi Mohamed Mushi (NCCR-Mageuzi)

Mwaka 2000-2005-->Freeman Aikaeli Mbowe (CHADEMA)

Mwaka 2005-2010-->Fuya Godwin Kimbita (CCM)

Mwaka 2010-2015-->Freeman Aikaeli Mbowe (CHADEMA)

Kwa mtiririko huo ninaona kwamba, Freeman Aikaeli kama ataamua tena kugombea ubunge katika jimbo hilo, basi ana kazi ya kupambana na trends and outcome za kisiasa za Jimbo la Hai zitakazopingana na uamuzi wake wa kuwa Mbunge wa jimbo hilo kwa vipindi viwili mfululizo.

Hoja yangu imechagizwa pia na maandiko ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Jenerali Ulimwengu katika gazeti la Raia Mwema wakati akielezea wasifu wa Marehemu Charles Kileo ambaye alikuwa ni Mbunge wa Hai kuanzia mwaka 1985-1990. Jenerali Ulimwengu alisema
,
Jimbo la Hai lina wazee wanaojiona kama waamuzi wa masuala ya kisiasa wilayani humo. Hawa ni wazee wazito, wenye kauli zenye uzani. Wamezoea kwamba mbunge wa jimbo lao anakuwa ni tarishi wa wazee wakwasi wa Machame.

Jenerali Ulimwengu ana maana kuwa, Wazee wa Jimbo la Hai huwa wanamchoka Mbunge baada ya miaka mitano hasa pale anapokataa kuwa tarishi wao.

Hoja ya msingi, Je, Mhe. Freeman Mbowe ataweza kupambana na mzimu kisiasa wa Jimbo la Hai hasa ikichukuliwa kuwa matokeo ya Serikali za Mitaa yameonyesha katika Jimbo la Hai, a tight political race in October General Election.

Nini maandalizi ya Freeman Mbowe katika kukabiliana na mwonekano wa siasa za Jimbo la Hai?.
 
Acha wananchi wa Hai waamue!!! Mbowe aliachia Ubunge kwa kuwa alikuwa anagombea Urais... Kwa sasa Wananchi wamempa dhamana yeye na hata akiamua kuachia ngazi bado wananchi watamtaka Mbowe awape Mbadala... Hai waichague CCM kwa lipi? Geita, Kahama na kote wanako chimba madini wanapewa MRABAHA kutokana na Rasilimali Madini ya Dhahabu yanayochimbwa LAKINI wananchi wahifadhi wa Mt Kilimanjaro huwa hawafaidiki kwa lolote ingawa Mlima unazailisha Trillions kwa mwaka ... Wanasubiri CCM ifungashe virago ili kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii na wao wapate kufaidi rasilimali zao ...

Wacha watu wajitokeze Kamanda Mbowe awagaragaze kabla ya saa nne asubuhi siku ya kupiga kura
 
Mbona Mramba aliweza kuvunja hiyo trend Rombo na kupata vipindi viwili rombo?pamoja na kuwa hapa mwaka huu Ben Saanane na Frate mmojawao ataipeperusha bendera yetu badala ya Selasini lakini siku zote nasema haiba ya mgombea na chama ndivyo hupishana.Hao uliosema wameshinda kipindi kimoja inawezekana haiba silipishana tu.CCM kwa kuwa ni waizi wa kura wakiona hii uloandika watafurahi kweli

Pia kule Kyela kwa Mwakyembe kuna trend kuwa Mbunge hachaguliwi zaidi ya vipindi viwili

Jimbo la Hai Mbowe bado ana nguvu kwani matokeo ya serikali za mitaa 2009 kule yalikuaje?
 
mbowe anakimbia jimbo anakwenda kugombea moshi mjini mzee ndesa anapumzika alee wajukuu.
 
mbunge pale nI martin munisi wazee wa kimachame washaaa amua muda sana

Siasa za Jimbo la Hai ni ngumu sana.

Ukiangalia waliowahi kuwa wabunge, utagundua Wazee wa Machame huwa hawaridhiki na kazi za mbunge wao kwa njia rahisi.

Mbowe akishinda tena kipindi cha pili mfululizo itakuwa ni sifa ya kipekee.

Jimbo la Hai ni moja ya majimbo ambayo ni magumu sana kiutawala.
 
Acha wananchi wa Hai waamue!!! Mbowe aliachia Ubunge kwa kuwa alikuwa anagombea Urais... Kwa sasa Wananchi wamempa dhamana yeye na hata akiamua kuachia ngazi bado wananchi watamtaka Mbowe awape Mbadala... Hai waichague CCM kwa lipi? Geita, Kahama na kote wanako chimba madini wanapewa MRABAHA kutokana na Rasilimali Madini ya Dhahabu yanayochimbwa LAKINI wananchi wahifadhi wa Mt Kilimanjaro huwa hawafaidiki kwa lolote ingawa Mlima unazailisha Trillions kwa mwaka ... Wanasubiri CCM ifungashe virago ili kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii na wao wapate kufaidi rasilimali zao ...
Mkuu,

Unashindwa kuelewa kama Freeman Mbowe aligombea ubunge katika jimbo hilo mwaka 1995 na kubwagwa na Mwinyihamisi Mushi wa NCCR-Mageuzi.

Akarudi tena kwenye uchaguzi wa mwaka 2000 na kushinda uchaguzi.

Mwaka 2005 akamua kuachia ubunge na kuwaletea Clement Zablon Kwayu (mbadala) lakini huyo mbadala wake akabwagwa na Fuya Kimbita wa CCM.

Hii inaonyesha ni jinsi gani Jimbo la Hai lilivyo katika kuwapata wabunge wa Jimbo hilo.
 
kashifa ya ndoa ya mbowe pia ni tatizo
 
kashifa ya ndoa ya mbowe pia ni tatizo
Mkuu,

Sidhani kama hilo ni tatizo kwa siasa za Tanzania. Wapiga kura wa Tanzania hawajafikia kiwango cha kuanza kuwachambua wagombea ubunge katika msingi wa maisha ya ndoa au familia zao.

Hii hoja haiuziki kwa wapiga kura labda kwenye nafasi ya Urais.
 
Hata katika urais bado sio tatizo
 
Hata katika urais bado sio tatizo
Nadhani kwa kiwango kikubwa hoja hii inauzika kwa sababu Rais wa Tanzania ni mmoja na pia ni kioo cha Taifa.

Kwa mfano, Sidhani kama Captain John Komba akijitokeza kugombea Urais halafu matendo yake katika picha kama hii hapa chini hasichukuliwe uzito mkubwa na wananchi wakati wa kupiga kura.

Wananchi wengi hawawezi wakakubali Rais wao kuwa na matendo kama haya ya Mbunge, John Komba.

mmmmh.png
 
Wacha watu wajitokeze Kamanda Mbowe awagaragaze kabla ya saa nne asubuhi siku ya kupiga kura
Mkuu,

Nimekupatia trends za kisiasa katika Jimbo. Nafikiri kwanza ingekuwa vizuri kuwafahamu wale watapambana naye ili kusaidia katika kupata angalizo ya kile kitatokea kutokana hali halisi ya kisiasa kama nilivyoonyesha kuanzia mwaka 1985.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom