Je, mwenye Degree ya historia anaweza somea nini Masters?

INNOXVII

Member
Apr 2, 2020
45
16
Habari za muda huu wakuu, hivi kwa mtu anayesoma bachelor of arts in history (UDSM), kwa level ya masters anaweza kuchukua kitu gani? Au lazima aendelee na hiyo ya histoy..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nipe namba yako kutokana na iyo post yako nmeona uko katika hali sawa na mm....nipe namba yako tushauriane kuusu jambo ilo pengine tutasaidiana.
 
Hiyo ada ya masters nenda veta kasome technician course yoyote.. iwe ya umeme, a.c , ama mechanics .. itakubeba sokoni kuliko hizo theory unazoenda kuzisoma kwenye masters kwa ada kubwa

Mkuu! Embu ongezea nyama hapa, nina degree ila nipo tu mtaani, nataka niende veta..

Kozi gani nzuri


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu! Embu ongezea nyama hapa, nina degree ila nipo tu mtaani, nataka niende veta..

Kozi gani nzuri


Sent from my iPhone using JamiiForums

Kozi nyingi za veta ni dili.. inategemea unapendelea nini.. kwa upande wangu nakushauri kafanye

Electric technicians, car mechanics, diesel engine mechanics ile ya kuwa na jukumu la kufanya service engine kubwa kama za malori ama magenerator makubwa
 
Mkuu chukua Prospectus ya chuo chochote hasa UDSM, UDOM, MZUMBE, TUMAINI N.K angalia kozi gani zinahitaji mtu mwenye sifa kama zako then chagua moja utakayoipenda.

ila nyie nyia mlitupigia sana sana kelele mabwenini A-LEVEL na CHUO (KIDDING)
 
unaweza kusoma history of america civil wars🤣🤣🤣🤣just kidding
lakini haya mambo bhana usipopata muongozo ni pasua kichwa sana aisee
 
Daah..! mkuu B.A History na bado tena unatamani upige master's ya vitu kama hivyo..tuliza kwanza kichwa..utatumia gharama kubwa na pengine bado mambo yakawa magumu sana..!
 
Kama ana GPA nzuri ya kuanzia 3.8 au walau 3.5 na ana passion ya kuwa mwanataaluma, mwambie afanye haraka afanye masters in history, kuna shortage kubwa ya walimu wa history at university level, na hamna hata mmoja alie mtaani hana kazi.

Mim nafanya PhD ya history kwa sasa na ni muajiriwa, nilibezwa sana ways back na kejeli nyingi ila sasa hivi all eyes on me!

Karibu kwa ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo jingine ni kuwa mtu anafika kidato cha 6 hana NDOTO yoyote, kaambiwa tu tangu mtoto kuwa elimu ufunguo wa "maisha" then anakwenda tu University kwa sababu ana vigezo vya kuchaguliwa na uwezo/fursa ya ada (bila kufahamu kwanini anakwenda). Anamaliza hafahamu anatakiwa afanye nini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom