DR. MWAKABANJE
JF-Expert Member
- Nov 7, 2012
- 1,976
- 3,127
Bila shaka wengi wetu pia wameweza kueleza maoni mbalimbali juu ya mwenendo wa uchumi nchini kwa sasa, nami kama mwananchi wa kawaida napenda nitoe ushuhuda wangu juu ya jambo hili hasa ukizingatia kuwa ujasiliamali ni sehemu ya maisha yangu pia!
Nina kabiashara kangu huko mkoani, uwezo wa mauzo yangu kwa wastani ilikuwa ni 80,000 Tshs. Kwa siku hadi kufikia December mwaka jana. Kufikia January 2016 hali ya biashara ilibadilika kiasi (mimi pamoja na watu wengine ninao wajua ) hii haikuleta hofu kabisa kwani tulijua ni kawaida kwa mwezi wa January hadi March biashara nyingi kuyumba kwa kuwa watu wanakuwa wametoka kwenye msimu wa sikuu na majukumu ya kupeleka watoto shule.
But hali imekuwa sivyo hadi June hii trend ya biashara ni bora ya January au February kuliko sasa, purchasing power ya wananchi imeshuka kwa kiasi kikubwa, binafsi napata mashaka sana hadi mtu unahisi kuna uwezekano wa kupoteza mitaji, nikiongea na jamaa kariakoo wanasema hali ni hiyohiyo! Najiuliza hiki ni nini? Mwisho wake lini? Sasa hivi mauzo sometimes yapo zero kwa siku, na ukiwauliza au kusimulia wengine wanasema bora hata mwenzetu!
Jukwaa hili ni pana, naomba wajuzi wa mambo haya watupe mwanga na pengine kututoa wasiwasi sisi wajasiriamali wadogo.
NB.Yanayonikumba mimi hayahusiani na ukwepaji kodi awali, kwani binafsi sijawahi kukwepa kodi wala sina mtaji wa kukwepa kodi maana nijuavyo wafanyabiashara wakubwa ndo walikuwa na mchezo huo.
Pia sintapenda kupewa majibu yasiyojitosheleza mf. Mtu anasema tupo kwenye mpito hali itatengamaa bila kueleza ni kwa vipi hali itatulia wakati hata sukari niliambiwa hivyo but bei ndo inazidi kupaa.