Je! Mungu ni yule yule?

Sasa atathibitishaje kitu ambacho anaamini hakipo!?.Nyinyi mnaoamini kipo ndiyo mnapaswa kuthibitisha uwepo wa Mungu.Mi namwelewa sana Kiranga.

Acheni kuzunguka mbuyu wenyewe.
Zaidi, kama mtu anakubali logic na anaelewa "proof by contradiction" na anajua kusoma, na kashafuatilia thread hii, ataona kwamba uthibitisho huo unaodaiwa ushatolewa mara lukuki hapa.

Sasa kama kipofu anabishana tofauti ya rangi nyekundu na bluu wakati haioni, mimi siwezi kuwajibika kwa hilo.

Na kwa kweli huo utakuwa ushahidi zaidi kwamba Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hayupo.

Maana angekuwepo, dunia isingekuwa na vipofu.
 
Unasema Mungu hayupo?

Kanusha
 
Nikuulize ndugu swali dogo tu je kwa vile nyie hamuamini uwepo wa mungu je vp kuhusu neno dhambi unaamini kama kina dhambi
 
Sio nasema tu.

Mungu mjuziwa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Ulimwengu huu uliopo unamkataa na kumkanusha kabla mimi sijaandika lolote.
Hebu weka hayo makatazo ya ulimwengu kuhusu Mungu nami nione..

Mathalani Mimi nijiweke katikati kwamba ndo nasikia leo kuhusu uwepo au kutokuwepo kwa Mungu

Kwa nn unasema hakuna Mungu??
 
1. Wanaosema Mungu yupo, wanasema Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

2. Mungu huyo wa (1) hapo juu,alikuwa na uwezo wote,ujuzi wote na upendo wote kuumba ulimwengu ambao hauna dhambi, mabaya wala majanga ya asili yanayoua na kutaabisha wengi.

3. Mungu huyo wa hapo juu, hana sababu ya kimantiki ya kuumba ulimwengu ambao mabaya, dhambi, majanga ya asili yanawezekana kuwepo.

4. Ulimwengu huu umejaa mabaya, dhambi na majanga ya asili.

5. Ulimwengu huu haujaumbwa na Mungu huyo.

6. Munguhuyo angekuwepo,upendowake mkuu usingeruhusu mabaya, dhambi na majanga ya asili yawezekane kwenye ulimwengu wowote aliouumba.

7. Ulimwengu huu una mabaya, dhambi na majanga ya asili lukuki.

8. Hivyo, Mungu huyo hayupo. Ni hadithi ya kutungwa tu.

Kimantiki, hii inaitwa "proof by contradiction"

Proof by contradiction - Wikipedia
 
Kwenye 5 hapo umesema Mungu hajaumba ulimwengu, Je ni nani ameuumba? Lazima unalo jibu kwa kua umwkanusha.

Halafu Je, kila usiloweza kulithibitisha wewe kwa utashi wako halipo?

Je unakubali kua binadamu ana ukomo wa kuthibitisha mambo ambayo yako into existence??
 
Ukiniuliza square root ya 2 ni nini, nikakwambia sijui, hilo halina maana ya kwamba ukiniambia ni 10 (jibu potofu) ni lazima nikubali, kwa sababu sijui jibu sahihi.

Hasha. Naweza kushindwa kujua jibu sahihi, nikawa nalitafuta bado. Lakini ukanipa jibu potofu mara moja nikajua hili ni jibu potofu.

Mfano wa square root ya 2 na jibu la 10 unatuonesha hili.

Unaniuliza kuhusu nisiloweza kuthibitisha kwa utashi wangu, wakati mimi nimekuthibitishia Mungu hayupo kwa mantiki.

Umeelewa hata mantiki niliyotumia?

Kama binadamu ana ukomo wa kuthibitisha mambo yaliyo katika existence, huu ni ushahidi mwingine wa kwamba Mungu muweza yote, mwenye upendo wote na ujuzi wote hayupo.

Angekuwepo, kwa upendo wake wote, ujuzi wake wote na uwezo wake wote, asingeumba viumbe na kuwapa upeo mdogo tu wa kujua mambo na mengine mengi kuwaficha. Hiyo ni tabia ya ubinafsi na chogo ambayo hata watu wa kawaida wanaojitambua wanaikosoa, itakuwaje Mungu awe mbinafsi na mwenye choyo?

Kama Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote yupo, kwa nini kaumba ulimwengu ambao matetemeko ya ardhi yanaweza kutokea na kuua watoto wachanga wasio na hatia, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao matetemeko hayo hayawezekani kutokea?
 
Mfano wako wa square root ya 2 na jibu la 10 hauko sahihi, kwani umejengwa kwenye context iliyo kamili na yenye complete rules. Mathalani nikienda kwa muhadzabe ambae hajui hata 1 ni nini nikamwambia square root ya 2 ni 10 kukataa kwakwe kutakua tofauti na kukataa kwako (wote mtakua mmekataa lakini katika context mbili tofauti)

Wewe unakataa kama muhadzabe [hakuna complete rule jibu as reference kwenye guidance]

Hakujakua na End ambayo inaturudisha sasa kuweza kukataa square root ya 2 kwa kutumia clue.
 
Kwa hiyo kama wewe unakanusha kua Mungu hakuumba ulimwengu ndo uweke standard reference ya nani aliumba ulimwengu

Kama hakuumba niambie nani aliuumba ulimwengu??
 
Mfano wako wa square root ya 2 na jibu la 10 hauko sahihi, kwani umejengwa kwenye context iliyo kamili na yenye complete rules. Mathalani nikienda kwa muhadzabe ambae hajui hata 1 ni nini nikamwambia square root ya 2 ni 10 kukataa kwakwe kutakua tofauti na kukataa kwako (wote mtakua mmekataa lakini katika context mbili tofauti)

Wewe unakataa kama muhadzabe [hakuna complete rule jibu as reference kwenye guidance]

Hakujakua na End ambayo inaturudisha sasa kuweza kukataa square root ya 2 kwa kutumia clue.
Mfano wa square root ya 2 unaonesha kwamba, mtu anaweza kujua jibu fulani si sahihi hata kama jibu sahihi halijui.

Mfano huu ulitumika kuzima hoja yako kwamba, mtu anayeshindwa kujibu swali la watu tumetoka wapi (hajui jibu sahihi) hawezi kubishia jibu la kwamba tumeumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

Nimekuonesha kwamba mtu anaweza kuwa hajui jibu sahihini lipi (hajui square root ya 2 ni nini) lakini ukimpa jibu lisilo sahihi, kutokujua kwake jibu sahihi, hakumzuii yeye kujua kwamba hili jibu ninalopewa (10) si sahihi.

Kwa sababu anajua kanuni moja ya msingi.

Jibu la square root ya 2linatakiwa kuwa dogo kuliko 2, otherwise, mtu akitoa jibu lililo kubwa kuliko 2, litakuwa si jibu sahihi, kwa sababu lita contradict kanuni ya msingi ya kuzidisha.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ambaye akaenda kuumba ulimwengu huu wenye mabaya, dhambi na majanga ya asili, hayupo.

Kwa sababu anakuwa contradicted na ulimwengu tunaouona, kama vile jibu la "square root ya 2 ni 10" linavyocontradict hesabu za kuzidisha.

Ukikubali Mungu huyu yupo, ni sawa sawa na kukubali square root ya 2 ni 10.

Unakubali jibu ambalo si sahihi kwa kulazimisha.

Kwa sababu jibu lina contradiction.
 
Tofauti ipo.

Hakuna mjadala kwamba watu wapo. Au unabisha?

Kuna mjadala kama mungu yupo.

Ukisema maneno haya yaameandikwa na watu, hilo halihitaji kuthibitishwa, hatuhitaji kuthibitisha kwamba watu wapo.

Tunahitaji kuthibitisha mungu yupo maana haonekani, haeleweki, wazo la kuwepo kwake linajipinga lenyewe.

Utasemaje mawili haya ni sawa?
Akili hazionekani kwahiyo unataka kusema hakuna akili? Acha kujitoa ufahamu wewe
 
Kwani nani kasema Mungu muweza yote, mwenye upendo wote na ujuzi wote hayupo kwa sababu haonekani?

Mbona unanibishia kwa hoja ambayo sijaitoa?

Unaanzaje kunipinga kwa kitu ambacho sijakisema?

Sijasema Mungu hayupo kwa sababu haonekani. Wewe unanisemea mimi kwamba nimesema hivyo, halafu unanipinga wewe mwenyewe, kwa kitu ambacho sijakisema.

Unaelewa ninavyoandika?
 
Umesema haonekani unataka kukataa
Hoja ya msingi kabisa kwamba Mungu hayupo ni kwamba dhana (dhana, sikitu chochote kinachoonekana) ya kuwepo kwake, inajipinga yenyewe.

Dhana ya kuwepo Mungu ina contradiction.

Unaelewa hilo jambo?
 
kulubule

Mtiririko huu hapa chini wa kimantiki hauongelei lolote kuhusu kuonekana kwa Mungu.

Na unaonesha dhana ya kuwepo huyo Mungu inajipinga yenyewe.

1. Wanaosema Mungu yupo, wanasema Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

2. Mungu huyo wa (1) hapo juu,alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kuumba ulimwengu ambao hauna dhambi, mabaya wala majanga ya asili yanayoua na kutaabisha wengi.

3. Mungu huyo wa hapo juu, hana sababu ya kimantiki ya kuumba ulimwengu ambao mabaya, dhambi, majanga ya asili yanawezekana kuwepo.

4. Ulimwengu huu umejaa mabaya, dhambi na majanga ya asili.

5. Ulimwengu huu haujaumbwa na Mungu huyo.

6. Munguhuyo angekuwepo,upendowake mkuu usingeruhusu mabaya, dhambi na majanga ya asili yawezekane kwenye ulimwengu wowote aliouumba.

7. Ulimwengu huu una mabaya, dhambi na majanga ya asili lukuki.

8. Hivyo, Mungu huyo hayupo. Ni hadithi ya kutungwa tu.

Kimantiki, hii inaitwa "proof by contradiction"

Proof by contradiction - Wikipedia
 
Hoja ya msingi kabisa kwamba Mungu hayupo ni kwamba dhana (dhana, sikitu chochote kinachoonekana) ya kuwepo kwake, inajipinga yenyewe.

Dhana ya kuwepo Mungu ina contradiction.

Unaelewa hilo jambo?
Unaweza kuniambia sababu zinazokufanya usema hayupo
 
Unaweza kuniambia sababu zinazokufanya usema hayupo
1. Wanaosema Mungu yupo, wanasema Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

2. Mungu huyo wa (1) hapo juu,alikuwa na uwezo wote,ujuzi wote na upendo wote kuumba ulimwengu ambao hauna dhambi, mabaya wala majanga ya asili yanayoua na kutaabisha wengi.

3. Mungu huyo wa hapo juu, hana sababu ya kimantiki ya kuumba ulimwengu ambao mabaya, dhambi, majanga ya asili yanawezekana kuwepo.

4. Ulimwengu huu umejaa mabaya, dhambi na majanga ya asili.

5. Ulimwengu huu haujaumbwa na Mungu huyo.

6. Mungu huyo angekuwepo, upendo wake mkuu usingeruhusu mabaya, dhambi na majanga ya asili yawezekane kwenye ulimwengu wowote aliouumba.

7. Ulimwengu huu una mabaya, dhambi na majanga ya asili lukuki.

8. Hivyo, Mungu huyo hayupo. Ni hadithi ya kutungwa tu.

Kimantiki, hii inaitwa "proof by contradiction"

Proof by contradiction - Wikipedia
 
1. Wanaosema Mungu yupo, wanasema Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

2. Mungu huyo wa (1) hapo juu,alikuwa na uwezo wote,ujuzi wote na upendo wote kuumba ulimwengu ambao hauna dhambi, mabaya wala majanga ya asili yanayoua na kutaabisha wengi.

3. Mungu huyo wa hapo juu, hana sababu ya kimantiki ya kuumba ulimwengu ambao mabaya, dhambi, majanga ya asili yanawezekana kuwepo.

4. Ulimwengu huu umejaa mabaya, dhambi na majanga ya asili.

5. Ulimwengu huu haujaumbwa na Mungu huyo.

6. Mungu huyo angekuwepo, upendo wake mkuu usingeruhusu mabaya, dhambi na majanga ya asili yawezekane kwenye ulimwengu wowote aliouumba.

7. Ulimwengu huu una mabaya, dhambi na majanga ya asili lukuki.

8. Hivyo, Mungu huyo hayupo. Ni hadithi ya kutungwa tu.

Kimantiki, hii inaitwa "proof by contradiction"

Proof by contradiction - Wikipedia
Welcome back mkuu Kiranga!!!
 
Back
Top Bottom