Je! Mungu ni yule yule?

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,878
5,432
Nikisoma Vitabu Vya Dini Hasa Biblia... Mungu wa Kuanzia Kitabu Cha Mwanzo Au Vitabu Vya Kale Ni Tofauti Sana kitabia na Mungu wa Agano Jipya.

Tabia za KiMungu Alizokuwa nazo Katika agano la Kale Nikilinganisha Na Agano jipya naona Tofauti Kubwa Sana

Mfano AGANO LA KALE
Mungu Alikuwa ni Wa Hasira Sana na Anayependa Sana Waumini wake Wafuate Sheria ... Kulikuwa na Sheria Za Kitakatifu Mfano Kujiosha Mwili... mavazi.. Kuhudumia Sehemu ya Kuabudia kwa usafi wa hali ya juu... kuvukisha Ubani... kujitawaza... n.k n.k

Sasa Nitapokuja Kusoma Agano jipya Mungu anakuwa Amebadilika Sana Hasa Katika Kuabudiwa.. .. Yale Mambo ya kale aliyotaka hayapo tena.. Je Mungu amebadilika Hataki Tena Ubani... Zawadi za kuteketezwa Alizosema zinamvutia?

Je Kuna Ubaya Gani Kutoa Sadaka Za hivyo.. kuna Ubaya Gani Kurudia Kule kwa Kale.. Kujisafisha Uendapo Kuabudu..... Kuwa Msafi Au kujitawaza kama kale...
 
Ubaya sasa tumeingia kwenye Dunia ya kiushindani, dini ikiwekewa masharti Sana huwapati waumini wengi. Ndiyo maana jamaa akaona apunguze maadhi ya masharti, yalazima sasa ni sadaka, hutakiwi kutoa chini ya Tsh. 5,000 Mchungaji hapokei, Maana Mungu aliweka kiwango.
 
Hakuna mungu, huyo unayemsoma ni hadithi tu zimetungwa na watu.

Ukijua hili swali lako halitakutatiza.
Hata unayosoma wewe na kukufanya useme hakuna mungu ni mawazo ya watu pia.Hivyo hauna tofauti na hao ambao unaona wanafuata hadithi tu,kuwa huru kwanza kwa kutofuata mawazo ya watu ili upate haki ya kusema wenzio kuwa wanafuata hadithi tu.
 
Unapo sema mungu ni yule yule inamana hizo hadithi ni yeye mungu aliziandika.
 
Hata unayosoma wewe na kukufanya useme hakuna mungu ni mawazo ya watu pia.Hivyo hauna tofauti na hao ambao unaona wanafuata hadithi tu,kuwa huru kwanza kwa kutofuata mawazo ya watu ili upate haki ya kusema wenzio kuwa wanafuata hadithi tu.
Tofauti ipo.

Hakuna mjadala kwamba watu wapo. Au unabisha?

Kuna mjadala kama mungu yupo.

Ukisema maneno haya yaameandikwa na watu, hilo halihitaji kuthibitishwa, hatuhitaji kuthibitisha kwamba watu wapo.

Tunahitaji kuthibitisha mungu yupo maana haonekani, haeleweki, wazo la kuwepo kwake linajipinga lenyewe.

Utasemaje mawili haya ni sawa?
 
Ningekujibu vema swali lako laiti kama ningekuwa ndiye mwenye kipawa, lakini bahati mbaya babu na bibi zetu hawakuwahi kuishi na Mungu huyo umsemaye bali waliletewa habari baadaye juu ya uwepo wake. Je, kuna mbegu nzuri ya mihogo inayoweza kutoa ishara nzuri ya hali ya kustawisha migomba ukizingatia kwamba inahitaji maji mengi?
 
Tofauti ipo.

Hakuna mjadala kwamba watu wapi. Au unabisha?

Kuna mjadala kama mungu yupo.

Ukisema maneno hata yaameandikwa na watu, hilo halihitaji kuthibitisha, hatuhitaji kuthibitisha kwamba watu wapo.

Tunahitaji kuthibitisha mungu yupo maana haonekani, haeleweki, wazo la kuwepo kwake linajipinga lenyewe.

Utasemaje mawili haya ni sawa?
Umeshindwa kunielewa kwa sababu hauna uhuru wa mawazo katika hili suala kama mnavyojisifu,wewe unawaambia wenzako wanasoma hadithi zilizotungwa na watu tu na ndiyo nami nikakwambia kuwa hata unayosoma wewe pia kuhusu kutokuwepo kwa mungu ni hadithi za watu tu wenye kutaka watu waelewe hivyo. Mungekuwa na mawazo huru msingekuwa mnakuja na hoja za "sitaki kuamini nataka kujua" mara "mbona huyo mungu haonekani?".
 
Hakuna mjadala kwamba watu wapo.

Sijakataa kwamba ninachosema kimesemwa na watu.

What's your point?

Anayesema mungu yupo katika ulimwengu ambao hatujathibitisha kwamba mungu yupo, ana tatizo la kuthibitisha kwamba mungu yupo.

Anayesema mungu hayupo, ukimwambia maneno yake ni ya watu tu, hujamkanusha. Maana hajawahi kusema mungu yupo.

Unaposema maneno yangu ni ya watu tu, unakanusha nini?

Sijawahi kusema mungu yupo, sasa unaponiambia maneno yangu ni ya watu tu, unakanusha nini?

Tatizo unageza kanusho langu kwangu visivyo.

Mtu anayeamini mungu yupo ukimwambia maneno ya mungu yupo ni ya watu tu, na mungu hayupo, umemkanusha.

Mtu anayesema mungu hayupo, ukimwambia maneno yake ni ya watu tu, hujamkanusha. Inawezekana ukawa umeongezea nguvu hoja yake.
 
Sorry Kiranga kuingilia imani yako ila mimi naamini kuwa kuna Mungu.Bahati nzuri hakuna aliyelazimishwa kuamini kama yupo au hayupo.
Kukusaidia tuu nitakuombea kwa huyo Mungu usiyeamini kuwa yupo ili akuonyeshe kuwa yupo.Atakuonyesha na utaleta thread hapa Jf.
Unajuaje kwamba mungu yupo na hii si imani potofu tu?
 
Nikisoma Vitabu Vya Dini Hasa Biblia... Mungu wa Kuanzia Kitabu Cha Mwanzo Au Vitabu Vya Kale Ni Tofauti Sana kitabia na Mungu wa Agano Jipya.

Tabia za KiMungu Alizokuwa nazo Katika agano la Kale Nikilinganisha Na Agano jipya naona Tofauti Kubwa Sana

Mfano AGANO LA KALE
Mungu Alikuwa ni Wa Hasira Sana na Anayependa Sana Waumini wake Wafuate Sheria ... Kulikuwa na Sheria Za Kitakatifu Mfano Kujiosha Mwili... mavazi.. Kuhudumia Sehemu ya Kuabudia kwa usafi wa hali ya juu... kuvukisha Ubani... kujitawaza... n.k n.k

Sasa Nitapokuja Kusoma Agano jipya Mungu anakuwa Amebadilika Sana Hasa Katika Kuabudiwa.. .. Yale Mambo ya kale aliyotaka hayapo tena.. Je Mungu amebadilika Hataki Tena Ubani... Zawadi za kuteketezwa Alizosema zinamvutia?

Je Kuna Ubaya Gani Kutoa Sadaka Za hivyo.. kuna Ubaya Gani Kurudia Kule kwa Kale.. Kujisafisha Uendapo Kuabudu..... Kuwa Msafi Au kujitawaza kama kale...
Kuamini uwepo wa mungu ni utumwa wa mawazo na fikra ikiwa ni pamoja na uvivu wa kuuhangaisha ubongo. Kuna maswali mengi juu ya uwepo wa mungu kiasi kwamba vitabu vya dini havina majibu yake mpaka wanafikiria kuviandika upya. Fungukeni nyie bibadamu hakuna mdudu yeyote anayeitwa mungu
 
Utajuaje unachofikiri umeona kabla hakijaonekana kipo na si ndoto tu?
Imani ni zawadi kutoka kwa Mungu kupitia mwanae wa pekee Yesu Kristo.

Imani ni ile Elimu yenye mapokeo sahihi na fikira sahihi zenye Maono bora na malengo Bora kwa ajili Utukufu wa Mungu. Elimu hii humfanya mtu kuwa na uhakika na anachofanya au amini. ( stable, reliable , Trustworthy)

Elimu hii inajengwa na vitu vikuu vitatu, yaani 1. Ujuzi (Knowledge) 2. Hekima 3. Uelewa. Kikubwa Kati ya vyote hivyo ni Uelewa.

Elimu hii pia hufundishwa kupitia vitu vikuu vitatu 1. Matendo 2. Kusikia 3. Kuona ; Kikubwa kuliko vyote ni kusikia

ea2efda2e080c07cefd5e483480e647d.jpg
 
Kabla ya kwenda mbali, thibitisha kwamba mungu yupo.
 
Back
Top Bottom