Je, mmemwelewa Joseph Butiku? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, mmemwelewa Joseph Butiku?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MVUMBUZI, Apr 30, 2011.

 1. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Katika Kongamano la Azimio la Arusha linalorushwa na ITV Live mzee J. Butiku ameeleza kwa nini azimio la Arusha lilikufa na tukajiingiza katika mfumo wa soko holela au ubepari. Alieleza jinsi misingi na miiko ya azimio la Arusha lilivyoifikisha nchi pabaya mpaka kufikia kukopa 10mil. USD nchini India. Aliongeza kuwa wengi wa viongozi walikuwa hohehahe kiasi cha kukosa hata hela ya kujikimu na hata kushindwa kujenga nyumba zao.

  Then akawauliza wasomi waliodai kutaka miiko na misingi ya Azimio kuingizwa kwenye katiba kama "WATAMUDU HIYO HALI ILIYOKUWEPO" Yaani kukubali kufunga makanda na kuishi tu kwa mshahara na kuishi bila kuitehemea IMF, World Bank na taasisi nyingine za wahisani.

  Ninaamini vijana wa UDSM hawakujua walichokuwa wanafanya walipoambiwa mtamudu wakasema NDIYOOOO!!!!!! bila kuelewa wanajibu nini. ukweli ni kwamba alichouliza J. Butiku ni swali gumu na ambalo kwa wakati wetu jibu rahisi ni kwamba HATUMUDU kurudia misingi na miiko ya Azimio la arusha kwani itabidi tuamua kufanya kazi sana ili tusiombe misaada.

  Mimi nafikiri ili kurudia misingi ya azimio la Arusha kinaga ubaga ni lazima tujenge uchumi wa nchi na wa mtu binafsi binafsi la sivyo itakuwa ngumu ku- re view na kuingiza misingi na miiko ya azimio la Arusha katika katiba mpa katika uso wa GLOBALISATION.
  Tutaweza tu ku modify hiyo misingi na iendane na wakati tuliopo na siyo kufanya cut and paste ya miiko ya 1967 na kuingiza moja kwa moja kwenye katiba mpya
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Azimio la arusha si lazzima lirudiwe kama lilivyo. Linaweza kufanyiwa marekebisho fulani yanayoendana na wakati wetu, na hasa ya le ya msingi. Si yote yaliyo katika Azimio hilo yanafaa kwa leo. Lakini pia si kila kilicho kwenye azimio hakifai. Yapo mengi mazuri hasa yale yanayosisitiza utu, haki, nk.
   
 3. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mimi naunga mkono baadhi ya miiko kwani mingine kwa sasa ni irrelevant . Tunatakiwa tuwe na modified version ya miiko na mingine inaweza kuwa adopted kama ilivyo ila tukianza kujidai kufunga mikanda kwa sababu ya ushabiki wa kisiasa tutarudisha nchi kusiko
   
 4. fige

  fige JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alichowauliza vijana si kubeba AA bali jukumu la Mageuzi wa kubeba mazuri ya AA kwenye katiba mpya.

  Ila nahasi yeye ndio hakumuelewa kijana wa UDOM kuhusu tofauti ya vipato.
   
 5. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Azimio la arusha lilikuwa na misingi ya uongozi, kwamba nani atakuwa kiongozi nz hatakiwi kufanya nini, kujifunga mkanda kulikuja baada ya vita
   
 6. A

  Ame JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Nadhani Butiku bado anaishi kwa mawazo ya zamani. Watu wanaotaka Azimio hawajasema lisiwe updated ili kuendana na hali na mazingira ili kuwe na mfumo unaoeleweka kuliko wa sasa ambapo unyonyaji uko legitimised. Wanafunzi wanaelewa kuwa wanaweza kuuboresha AA na kujenga nchi iliyoimara zaidi After all kwao ni bora hilo azimio kuliko maisha yaliyombele yao ambapo soko la ajira litakuwa flooded na hivyo kuishi kwa kudhalilika huku jamii ya kifisadi ikigeuka wafalme wao na wahisani ili waweze kukidhi mahitaji yao ya msingi maana wanamiliki njia zote kuu za uchumi kuanzia ardhi hadi mashirika ya huduma.
   
 7. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  ndugu wao kujubali sio kwamba hawajamuelewa. kama ww unabisha haina maana umemuelewa!
   
 8. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  huyu mzee butiko hata kuwa staki kabisa kusikia si kumuona tu. huyu ndo alieratibu vita na uganda ambavyo havikuwa na tija kwa taifa. kwa lugha nyepesi huyu ni part and parcel ya matatizo tuliyonayo na Tz with remarkable contribution. Najua wengi hamjui lakini huo ndo ukweli na sasa mnamuona kama shujaa. hamna kitu huyo mzee.
   
 9. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mambo ya Azimio la Arusha hayawezekani kwa nchi changa kama Tz nahasi viranja wakuu wakiwa wamebaki mabepari peke yao juu. ila tu kitu tunachoweza kufanya ni kulinda maadili ya uongozi. hili hata nchi za kibepari wanafanya. Otherwise azimio la arusha ni sikio la kufa. vijana wengi wa vyuo sasa hivi na wakufuata mkumbo tu hawaelewi undani wa haya mambo. serikali ifanye juhundi kuwelemisha watu na pia ilinde maadili ya uongozi.
   
 10. M

  Mkono JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  itakuwa hatua muhimu sana ktk ustawi wa taifa letu kama azimio la Arusha litarejeshwa.
   
 11. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Bwana mdogo soma historia ya nchi kabla ya kuongea!
  Kwa taarifa yako wakati wa vita ya Uganda kina Butiku walikuwa watu wadogo sana kiwadhifa na hakuwa na any direct link na vita vyenyewe au uendeshaji wake.
  Hata hivyo nimeiona debate ya Azimio la Arusha pale UDSM kwenye luninga na amechangia vizuri sana.
   
 12. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mbona wezi na Mafisadi tulionao leo wapo na wanapeta hadi Rais anawaogopa ingawa Sheria za kuwafikisha Mahakamani zipo?

  Azimio la Arusha la nini sasa? Achaneni usanii.
   
 13. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135

  Mkuu unajaribu kudhibitisha nini hapa...?

  Whta is wrong tukiamua kufanya kazi sana... ?

  Kwa nini unataka tusifanye kazi sana..?

  Kwa nini unataka tuombe misaada.. .. Mkuu tukuelewe vipi?
   
 14. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kutotaka kumuona au kumsikia mzee Butiku ni matatizo yako binafsi, mzee Butiku hakumualika Idd Amin Dada kuivamia Tanzania ili yeye aratibu vita ya kumuadhibu nduli yule. Humtendei haki mzee Butiku. Matatizo tuliyonayo sasa hivi yamesababishwa na viongozi wenye tamaa na ulafi wanao shindwa kukusanya kodi, wanaoingia mikataba ya hovyo, wanaokumbatia ufisadi, wanaokosa ubunifu na uongozi bora. Hao ndio wanaotakiwa kulaaniwa. Kuvunja miiko ya uongozi ndicho kinacho tugharimu sasa.
   
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Azimio la Arusha lilikuwa linajenga nchi kwa utaratibu wa kutoka chini kwenda juu (Bottom Up),- au kwa kiswahili cha mitaani " mwanzo mgumu." Kosa kubwa ni kuwa lilikuwa linazuia ubunifu miongoni mwa watu kwa vile lilikuwa linazuia ubinafsi. Kama mimi ndiye ningekuwa nimemrithi Nyerere, ningerekebisha vifungu vinavyozuia mtu binafsi kujipatia mali kwa ubunifu wake iwapo atakuwa ametumia njia halali. Ningeongeza utaratibu wa kuratibu mali za watanzania kwa kutumia idara ya kodi, akama ambavyo nchi zilizoendelea zinavyofanya. Vifungu vingine vyote vinavyohusu miiko ya uongozi ningeviacha kama vilivyo ingawa labda ningepambanua kwa kuongeza kuwa mali za kiongozi si siri yake, ni lazima aeleze jinsi alivyozipata baada ya kuwa kiongozi. Kiongozi anayegundulika kuficha mali zake binasfi basi zinataifishwa.

  Tanzania tatizo letu leo tunataka kujenga kutoka juu kwenda chini (top-down), ndiyo maana tunakimbilia kukopa pesa India bila kufahamu kuwa tunatakiwa kutengeneza pesa yetu wenyewe kwa kufanya kazi zaidi na kuwa makini katika matumizi ya hela zetu, siyo kununua rada kwa malipo ya mara tano ya bei halisi!! Viongozi wanaingia madarakani wakiwa maskini baada ya muda kidogo wanakuwa mabilionea wa kutupwa na wala hatuhoji!
   
 16. s

  salizajr New Member

  #16
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi hilo Azimio la Arusha...mbona hata watanzania hatufahamu misingi yake? kwa nini nakala yake isiwekwe kwa mfumo wa electronic ili tudownload na tusome tuelewe?
  Kwa uelewa wangu mdogo, kama nitakuwa sikosei...hivi si hili Azimio ndilo lilipelekea watu wajipangie foleni ya sukari na sabuni? Si hili hili Azimio lilisababusha watu kufulia majani ya mipapai kutokana na kukosa fursa ya kupata japo kipande cha sabuni?
  Sasa leo twataka turudie huko jamani? Ndiyo maana mzee Butiku ametia shaka kuwa hatutaliweza hilo azimio.Hivi tunasonga mbele au tunarudi nyuma?
  Mimi sidhani Azimio ndilo suluhisho la matatizo yetu. Kuna njia nyingi za kutransform bila hilo Azimio. Hebu watanganyika tusiwe wavivu wa kufikiri.


  ...If at first you didn't succeed...transform your database...
   
 17. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi hoja ni azimio la arusha ama siasa ya ujamaa na kujitegemea? Tusichanganye content za mambo haya mawili. Lakini kwa vyovyote vile miiko na maadili ya uongozi wa umma yanayo ainishwa na azimio la arusha tunayahitaji sasa kwa kiasi kikubwa kuliko wakati wowote ule wa historia ya nchi yetu. Wakati ni huu tunahitaji misingi hiyo irudi ikihuishwa na hali halisi ya mazingira tuliyo nayo sasa
   
 18. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #18
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu ulisoma elimu yako ya msingi na upili wapi hata usilisome azimio la arusha? Tanzania hii hii ama nje ya tanzania?

  Kwa hoja yako ya pili, kilichopelekea bidhaa kuadimika ni mchanganyiko wa sababu kadhaa, kubwa zaidi ni athari za baada ya vita vya kagera. Na hali hii si kwa tanzania tu imekwisha jitokeza sehemu nyingi ulimwenguni vita vilikopiganwa, kumbuka athari za vita ya kwanza na ya pili ya dunia katika nchi mbalimbali duniani, wao pia walikosa bidhaa muhimu kama ilivotokea hapa kwetu
   
 19. A

  Ame JF-Expert Member

  #19
  May 1, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Can we join hands to make this happen? I am about to start making my dream come true if you are committed can join me in the move.
   
 20. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 643
  Trophy Points: 280
  Jinsi hali ilivyo sasa ni sawa na kutibu kifua kikuu kwa kutumia "cofta" au sigara ya SM.Ila tukiweka misingi ya AA kwenye katiba,maana yake huwezi kuwa kiongozi kama wewe una mali nyingi...kwa mfano gari na kuendelea,wewe kama una gari kaa pembeni,umelipataje?
  Uongozi ni kitu cha kukalia mbali,sio kugombania!
   
Loading...