Je mkuu anatanguliza Tanzania kwanza?

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,897
18,474
Mkuu leo amewataka waandishi wa habari kuwa wazalendo na kutanguliza Tanzania kwanza!

Je yeye mkuu anatanguliza Tanzania kwanza? Suala la Daudi Bashite limetupa mwanga mzuri na mapema kuwa mkuu ana shida kwenye eneo hili.

Kutokumchukulia hatua Daudi Bashite ambaye amedhihirika kutumia cheti fake na ameshindwa hata kukanusha kumemfanya mkuu adhihirike kutokutanguliza Tanzania kwanza,

maana Tanzania haina maslahi na mtu mdanganyifu anayetumia cheti fake!
Kikwazo kwa mkuu atakachokabiliana nacho kwenye mahubiri yake ya kuhamasisha uzalendo na kuweka Tanzania kwanza ni watu kumwambia mkuu "Toa boriti kwanza kwenye jicho lako ndipo utaona vema kukitoa kibanzi kwenye jicho la mwenzako"

Mkuu asikomae na msimamo wake wa kumwambia mwenye cheti fake "chapa kazi" halafu ategemee watu kusikiliza mahubiri yake!
Bila Bashite kutoka, mkuu atakuwa anatwanga maji kwenye kinu!
 
Back
Top Bottom