Je, mimi ni introvert au extrovert?

XII Tz

JF-Expert Member
Aug 16, 2020
4,293
6,957
Habari wakuu,

Niende moja kwa moja kwenye mada, kwa muda mrefu nimekua nikisoma threads tofauti tofauti hapa JF zinazohusiana na watu wapole/wakimya (introvert) na wale wasio wapole/wacheshi (extrovert)

Binafsi nimekua nikijiuliza nipo kundi lipi bila kupata majibu kwa sababu sifa zote za introverts zilizoainishwa na wadau wa JF ninazo ninapokuwa home yani ni mgumu sana wa kusocialize, nikikukuta Yani ni salamu tu imetoka hiyo .. na nilikuwa na uwezo wa kukaa ndani hata wiki nzima nisikanyage nje ya geti, yani kwa ufupi ni kwamba naonekana kwa nadra sana na pia nina feel more comfortable kuwa peke yangu yani huwa sitegemei kabisa kampani ya mtu.

Pia nina tabia ya kuongea peke yangu, yani nina uwezo wa kukaa hata masaa mawili nikawa naongea mithiri ya mtu aliye kijiweni na kucheka kabisa (nipo vizuri kabisa kiakili) hali inayonifanya nijiulize hivi wanaosema wako bored kivipi yani mbona am always alone but I don't feel any sense of boredom?

Tuachane na hayo, hali hii imenifanya nijizolee maadui kibao mtaa ninaoishi mbaya zaidi nachukiwa hadi na watu wazima yani utawakuta wamekaa kwenye group unawasalimia wote hamna anayekujibu.

Alafu kingine ni kwamba, nimekua ni mwepesi mno wa kufanya hard decisions (maamuzi magumu) yani ni kitu cha kawaida mno kwangu mpka kuna muda huwa najiuliza 'hivi ni mimi ninayefanya haya'

Lengo hasa la Uzi huu ni hivi, kipindi nasoma kuanzia form 1 mpaka form 6 nilikuwa stubborn sana shuleni, kila mwalimu ali complain kuhusu mimi. Mara nyingi nilikua nikifukuzwa kati kati ya kipindi sababu ya kelele darasani.

Mara nyingi nikiwa shuleni nitajitahidi kujitenga na wana kusudi niweze kujisomea lakini nitakaa kwa muda wa 30mins only nitafunga kitabu nitarudi kwenye group na washkaji (Yani nilikua siwezi kukaa alone)

Mpaka nafika advance Ilikua baadhi ya lessons nisipo kuwepo basi darasa litapoa mno, kwa kifupi Nina ucheshi wa aina yake, ofauti ni kwamba ninapokuwa home haya yote niliyo yaorodhesha huwa ni kinyume chake, yani nakua mpole mno siwezi kabisa kujichanganya na watu kama ambavyo nakua shuleni.

Kwa kifupi mimi wa shuleni na wa nyumbani ni watu wawili tofauti.

Je, mimi nipo kundi lipi, introvert au extrovert, au nipo katikati?

Nawasilisha
 
Habari wakuu,

Niende moja kwa moja kwenye mada, kwa muda mrefu nimekua nikisoma threads tofauti tofauti hapa JF zinazohusiana na watu wapole/wakimya (introvert) na wale wasio wapole/wacheshi (extrovert)
Ila ya kukaa ndani wiki nzima bila kutoka nje hiyo kiboko. Umenizidi. Mimi naweza kukaa siku moja au mbili tu, siku ya pili lazima nitoke. Wiki! Hiyo ni komesha.
 
Huyu ana nidhamu tu ya woga sio introvert.
Akiwa mbali na nyumbani anakuwa huru ila akirudi nyumbani anakosa huo uhuru.
Hata vijana wanaoanzaga kupiga ganja huwa wanakuwaga hivyo pia
Hamna mkuu, home hakuna chochote cha kuninyima uhuru ila nipo hivyo tu .. yani sipendi kabisa hata kusikia kelele ..
 
Wewe sio extrovert wala introvert ila kuna matatizo unayapitia lakini bado haujayajua.
Binadamu yeyote lazima awepo kwenye mojawapo ya hayo makundi mawili,kwa mfano wewe mtoa huu uzi,nakuona wewe ni extrovert,kwa jinsi ulivyojieleza bilavl shaka wewe ni extrovert.
 
We ni semi-extrovert mkuu 😅😅😅!

Anyways uko flexible mkuu sema tu una aibu flani na una watu na watu sio kila mtu unajichanganya nae! Ofcourse huo utakatifu wa nyumbani ni tabia ambayo baadhi ya watu wanayo na chanzo ni kutokutaka uonekane sio ila ukiwa mbali na home unafanya vimbwanga tu kama Side mnyamwezi
 
Habari wakuu,

Niende moja kwa moja kwenye mada, kwa muda mrefu nimekua nikisoma threads tofauti tofauti hapa JF zinazohusiana na watu wapole/wakimya (introvert) na wale wasio wapole/wacheshi (extrovert)

Je, mimi nipo kundi lipi, introvert au extrovert, au nipo katikati?
Mimi naona wewe ni retrofit
 
Back
Top Bottom