Je, mikoa ya Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Katavi na Iringa nayo haina mvua?

Mvua zinanyesha sana wakuu, kwa wale waliopo kinondoni, kwa mtogole, manzese na mabibo kuna mvua ya kufa mtu, leo ni wiki ya pili zinanyesha mfululizo.

Hata mazao yaliyokwisha pandwa yameshaota na yamestawi vizuri.
Inakadiriwa mavuno yake yatalisha dar yote na ziada itatosha kuilusha Rwanda na Burundi kwa pamoja.
Ndoto njema
 
Wakuu mvua mwaka huu ni shida maeneo mengi tuzidi kuomba tu hakuna namna maana hata hayo maeneo yanayosemekana inanyesha bado inanyesha kwa kusuasua tofauti na tulivyozoea
 
C360_2017-01-24-17-18-19-960.jpg
wakuu natokea chunya mida hii ndio hali ya chakula hayo ni mahindi wanaosema kuna njaa wanaitoa wapi?
C360_2017-01-24-17-16-24-695.jpg
 
Ruvuma inanyesha, nilikuwepo majuzi. Ila ni kwa kiwango tofauti na miaka yote (chache mno). Wengi waliopanda November-December walirudia Januari hii maana walivyopanda vilikauka. Kuna janga linanyemelea hali ikiendelea hivi.
 
Back
Top Bottom