Je, maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu au vitu? Wachumi tusaidieni, uchumi wa Awamu ya 5, unalisaidia Taifa au utaliangamiza?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,103
Reaction score
128,722
Wanabodi,

Hii ni thread ya swali, ambalo linatakiwa kujibiwa na wachumi wetu, kuhusiana na dhana ya maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu au ni maendeleo ya vitu?, na Je, sera za uchumi za serikali ya Awamu ya Tano, ambazo zimejikita kwenye maendeleo ya vitu, badala ya maendeleo ya watu, zitalisaidia taifa kupata maendeleo ya kweli, au zitalisaidia taifa kupata maendeleo ya vitu, huku ukiliangamiza taifa katika maendeleo ya watu, na mwisho wa siku, Tanzania iwe ni nchi ya maendeleo makubwa ya vitu na miundombinu lakini watu wake wakaendelea kubaki kuwa masikini wa kutupwa kama Ethiopia?.

Baba wa Taifa hili, Mwalimu Nyerere alikuwa ni muumini wa falsafa ya "Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu na Sio Maendeleo ya Vitu" , falsafa ya Uchumi wa serikali ya awamu ya Tano chini ya Jemedari wake, Rais, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, (Chuma, Jiwe, Mwamba), imejikita kwenye maendeleo ya vitu kwanza, kama kununua midege na kujenga miundombinu kwanza, halafu ndipo uje kwenye maendeleo ya watu, hivyo wachumi wetu, tusaidieni kutuelimisha, jee mfumo huu, wa kuanza na maendeleo ya vitu kwanza ndipo tuje kwenye maendeleo ya watu, utalisaidia taifa letu kuja kupata maendeleo ya kweli ambayo ni maendeleo ya watu, au na sisi Tanzania, baada ya kupata maendeleo ya vitu, ndege, reli, mabarabara mazuri, flyovers, etc, tutaishia kuwa kama Ethiopia ambayo ina miundombinu bora kabisa Barani Africa, huku ikiwa ndio nchi inayoongoza kukua kwa uchumi wa GDP ya zaidi ya 10% kwa mwaka, lakini uchumi wa mtu mmoja mmoja ukizidi kudididimia na watu wake ni maskini wa kutupa?

Kama kawaida yetu, maswali haya nayauliza genuinely kwa kutumia the right to expression provided na katiba yetu kwa kuuliza, jee awamu hii ya 5, inatumia falsafa gani ya kiuchumi?, jee uchumi huu wa kutanguliza kwanza vitu, unalisaidia taifa kwa kulipatia maendeleo ya kweli ya watu au unatupatia maendeleo ya vitu huku uchumi wa mtu mmoja mmoja ukizidi kudidimia, na kuangamia na mwisho wa siku tukajikuta uchumi, unalipaisha taifa kiuchumi, lakini kwa upande wa uchumi wa mtu mmoja mmoja, ukizidi kudidimia na kutufanya Watanzania tukaishia kuwa kama wa Ethiopians?

Kwa vile mimi sio mchumi, na tuna wachumi wetu lukuki humu mtandaoni, naombeni tusaidieni, tuelimisheni, kwa uchumi huu wa awamu ya 5, chini ya rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, Tanzania hapa tulipo, are we on the right track?,
tumetoka wapi, tuko wapi na tunakwenda wapi?, are we realy heading to the right direction?
Ili Tuendelee, Tunahitaji Nini Haswa kati ya Kuwaendeleza Watu au Vitu?
Hili ni swali la msingi sana, ili taifa letu liendelee, je tunahitaji maendeleo gani kwanza, tuanze kuendeleza watu kwa kuweka mazingira wezeshi ili watu wapate maendeleo, wajenge uchumi imara, wachangie kodi na wachangie uchumi wa taifa ndipo tutumie fedha za ndani kuleta maendeleo ya vitu, au tuanze kwa kukopa ili kujenga maendeleo ya vitu kwanza, hata kama ni kwa kukopa, tukiishapata vitu, ndipo tuje maendeleo ya watu?. What are our priorities?

Naomba kutumia falsafa mbili kutolea mifano Falsafa ya Mwalimu Nyerere, na Falsafa ya Adam Smith.

Falsafa ya Mwalimu Nyerere: Ili Tuendelee Tunahitaji Vitu Vinne,
  1. Watu-tunao
  2. Ardhi- tunayo
  3. Siasa Safi- tunayo?
  4. Uongozi bora-?
Kama vitu hivi vyote vinne tunavyo, sasa sisi Tanzania tumekosa nini?, kwa nini bado ni masikini?. Kati ya watu milioni 55 wa Tanzania, watu milioni 15 wanaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku!.

Nyerere alipotangaza Azimio la Arusha la siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, alisema kazi ya kujenga ujamaa ingechukua miaka 30. Lakini siku anatangaza kung'atuka alikiri kuwa tumekosea!, akakiri kwa kusema "kufanya kosa sii kosa, kosa ni kurudia kosa"

Je, mnajua tulikosea wapi?. Tumsikilize mwanauchumi Adam Smith kwenye theory yake ambayo itaonyesha kosa la Nyerere.

Economic Theory Ya Adam Smith-Land, Labor, Capital & Entrepreneurship
Katika theory hii ya Adam Smith, inashabihiana na theory ya Nyerere kwenye watu na ardhi, na itatofautiana na Nyerere kwenye Siasa Safi na Uongozi Bora, Adam Smith anasema tunahitaji Capital na Entrepreneurship. Hivyo theory ya Nyerere kuweka siasa safi na uongozi bora ni kitu kile kile, kwenye theory ya Nyerere kulikosekana Capital, Nyerere alifanya kosa kubwa kwa kuamini fedha sii msingi bali ni matokeo, but in reality, pesa ni msingi sana wa kupata mitaji tena intact kwenye kuleta maendeleo, pesa ni kila kitu!. Kama una watu, ardhi, siasa safi, na uongozi bora, bila mitaji fedha ya kuwawezesha hao watu kuitumia ardhi kuzalisha mali, bila fedha ni tulitwanga tuu maji kwenye kinu!.

Kitendo cha kutegemea kilimo cha jembe la mkono badala ya mechanised agriculture na modern farming, (kilimo biashara), hakutufikishi popote zaidi ya kupinda tuu migongo!.

Kitendo cha kutokuwa na mitaji ya rasilimali fedha za kuchimba madini, mitaji ya kujenga viwanda, hatuwezi kupiga hatua zozote za maendeleo ya watu.

Mwinyi alipoingia, alifungulia rukhsa zote, lakini wapi!, Mkapa akaja na sera ya ubinafsishaji kwa uongo kuwa fedha za ubinafsishaji zitawekwa kwenye mfuko maalum wa mitaji kuwawezesha Watanzania ili waje kuwa wamiliki wa uchumi wao!, ikaundwa shirika la CHC, fedha za ubinafsishaji zikawekwa humo, kumbe it was all a lie!, kumbe walijigawia wenyewe na hapa ndipo matabaka ya wenye nacho na wasionacho yalipoanzia!.

Magufuli Anafuata Sera Gani ya Kiuchumi na Anatupeleka Wapi?
Hapa ndipo mimi na akina sisi tusiojua uchumi, tunahitaji kuelimishwa na kueleweshwa, Magufuli anafuata mfumo gani wa kiuchumi na utatupekeka wapi?. Hili la kukopa dola milioni 500 kutoka Credit Suisse kwa ajili ya kujengea miundombinu, kwa riba ya asilimia 80% interest, ndani ya miaka 5! Hivyo tutalipa dola milioni 900!, kiukweli kabisa, mimi hili limenishtua na kuniogopesha!. Kama hili ni kweli tunakopa hivi, kwa mwendo huu, Magufuli atalikomboa taifa letu, au atalizamisha kwenye mzigo mkubwa wa madeni?. Kama fedha za bombadia, SGR, flyover, uwanja wa Chato, tunaelezwa ni fedha za ndani, hii mikopo mikubwa ya kisirisiri kwenye mabenki ya kibiashara kama Credits Suisse ni fedha za nini?. Tunaelezwa tunajenga miradi mikubwa kwa fedha za ndani!, fedha gani hizo wakati hata bajeti yetu bado ni bajeti tegemezi ya mikopo na ufadhili?. Tuna mikopo mikubwa ya kujenga hii miundondominu, tungeitumia kama capital ya kuwajengea uwezo kuwawezesha Watanzania kuinua sekta ya kilimo, tuzalishe zaidi, na kuwakopesha mitaji ya kumiliki viwanda vya agro processing industries, tusiuze tena mazao ghafi, bali tuuze semi processed na processed products ambazo zimekuwa na added value, kisha fedha zinazotokana na uzalishaji ndizo tukazitumia kujengea huu ufahari wa barabara na reli za kupaa, na kununua ndege taratibu, kuna tofauti gani?.

Wachumi tuelimisheni nasi tuelewe, faida za bombadia, SGR, flyover, uwanja wa Chato na miundombinu mingine inayowafaidia only 10% ya Watanzania, ukilinganisha na kuwajengea uwezo wakulima asilimia 67% wanaotegemea kilimo?!. Wachumi wetu jamani tufafanulieni tuwaelewe, mnalipeleka wapi taifa letu hili changa lenye umri wa zaidi miaka 55!.

Nadhani ili tusiingizane kwenye mikopo chechefu ya deni la taifa, tufike mahali Tanzania tukitaka kukopa kuingiza kwenye deni la taifa, Bunge lielezwe tunakopa fedha za nini, kiasi gani kwa riba gani ili Bunge ndilo liidhinishe mikopo ya deni la taifa, tusije kujikuta taifa linabebeshwa mzigo mkubwa wa madeni, kumbe tumejengea white elephants na matumbo ya watu!

Kupanga ni kuchagua.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea.
Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas.
Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza ...
 
Paskali katika vitu hivyo vinne Tanzania inakosa kimoja, WATU. Ardhi tunayo, siasa safi tunayo, Uongozi bora tunao, Watu ndio hatuna!! Hili hata Rais Museveni aliwahi kutuambia.
 
Mimi si Mchumi ila nakubaliana kabisa na Baba wa Taifa kuwa Maendeleo yanapaswa kuwa ya Watu na sio vitu,Kuna faida gani ya kuwa na barabara nzuri, mandege mengi ili hali watu wako ni wajinga,maradhi yanawasumbua na mlo kwao shida?

Tuanze kuinua hali za watu katika Elimu, Afya na huduma zote stahiki, Mtu akiendelea ni lazima maendeleo ya vitu yatafata!

Naomba Wachumi mjitokeze kama mlivyoombwa na mtoa Uzi ili nasi tuweze pata elewa kama tunaelekea njia sahihi.
 
Nunua boeing and airbus na zifike hadi vijijini

Jenga madaraja yanayounganisha Dar es salaam na Tokyo

Weka reli zinazotumia bluetooth na infrared

Hakikisha kila mtaa kunakuwa na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa

Weka flyovers kiasi kwamba unaweza kusafiri Dar hadi Kigoma juu kwa juu

Weka daraja la chini ya habari litalowezesha watu kusafiri hadi Zanzibar bila kuona bahari

Weka hadi paa la vioo kufunika miji mikubwa ili isiathirike na mvua na kusimamisha shughuli za watu (enzi zetu tulikuwa tunadanganywa Paris imefunikwa na vioo)

Mengine ongeza mwenyewe lakini sisi watu wa welfare economy mwishoni tutaka kuona hayo yote yamemwezesha vipi mwanachi wa kawaida kupata huduma bora za elimu (access and availability), huduma bora za afya (access and availability), access and availability ya maji safi na salama, food security, stable income and many more or else, investments husika are just bullshit!
 
Hakuna siku taarifa ya habari itapita bila ya issue ya maji safi na salama. Maji ndio kila kitu, miundo mbinu haijengwi bila maji, gari, treni, ndege, n.k. haviendi bila maji.

Chakula hakipikiki bila maji, asilimia kubwa ya mwili wa binadamu ni maji na unahitaji maji. Maji ndio kila kitu hata sayari mpya zinazofikiriwa kuhamiwa na binadamu kwanza wanaangalia uwezekano wa kuwepo maji. Serikali itatue tatizo la maji vijijini as a first priority.
 
Bwana huyu ni mkemia na sio mchumi, hana akijuacho kwenye uchumi. Ni bahati mbaya kwa taifa kujifanya anajua kila kitu
Urais ni taasisi haya mambo ya professional yanaingiaje?acha kuandika pumba ili mradi tu uonekane na ww umechangia.

hao waliowahi kuwa wachumi walikusaidia nini mbona shida zilikuwa palepale.
 
Paskali katika vitu hivyo vinne Tanzania inakosa kimoja, WATU. Ardhi tunayo, siasa safi tunayo, Uongozi bora tunao, Watu ndio hatuna!! Hili hata Rais Museveni aliwahi kutuambia.
Kweli tuna upungufu wa watu ikiwa mpo mnaoweza kuiita chupi kofia kwa kuwa tu imevaliwa kichwani na baba mkwe.

Uongozi bora ni upi? Huu wa 'Mwalimu wa Nidhamu' kukataza rasta shuleni Jumatatu halafu Alhamisi 'Mwalimu Mkuu' anamuumbua hadharani as if alishindwa kujadiliana naye ofisini?

Museven huyu wa Uganda? Huyu anayerudisha nyuma umri na kubadili katiba kila uchao ili aendelee kubakia madarakani?

Ashakhum si matusi, mjinga wewe! Uongozi bora hauhitaji nguvu kuumimina mioyoni mwa wananchi. Kiongozi bora hang'ang'anii madaraka. Kiongozi bora huacha nyuma yake ushawishi na sio hoja ya nguvu. Nyuma ya kiongozi bora kuna mamia ya wafuasi walio tayari kuliendeleza aliloliacha kiongozi wao.
 
huyu mshamba wetu kuna tatizo mahali
mimi naamini kuwa ukiendeleza watu ni rahisi sana vitu kuendelea.
ukiendeleza vitu ni ngumu sana kwa watu kuendelea
watu wakiwa na hela watajenga ila majengo bila watu kuwa na hela ni sawa na kazi bure
 
Maendeleo yoyote yasiyowagusa watu wake kwa maana ya kuinua hali zao za maisha na uchumi si maendeleo kwa kweli kama vitu ni maendeleo basi na mimi nimeendelea nina mavitu mengi sana kwenye stoo yangu
Maendeleo lazima yawe ni people centered!
 
Mimi sifahamu sana mambo haya,ila niulize kitu,hivi mwalimu Nyerere alikuwa mchumi?na kama alikuwa mchumi vipi alifanikiwa sana kutufanya tuige falsafa zake za kuongoza uchumi?pili,wakati wa utawala wake uchumi wa mtu mmoja mmmoja ulikuwa juu kuliko ulivyo sasa?tatu,nyanja kama za madini zilikuwa na udhibiti wa kutosha kuliko udhibiti huu anaoufanya Magufuli?Nne,Ningeomba ufafanuzi kidogo hapo penye maendeleo ya vitu,ni hayo tu,mnisaidie hapo.
 
Mimi pia sio mchumi, ila kwahali inavokwenda, hauhitaji kuwa mchumi ili kuelewa uchumi wa nchi yetu. Zaidi sana naona mkulu ndo anawapa ushauri wachumi wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…