Je, Lipumba na timu yake wanafikiri kuitumia karata ya Jaji Mkuu itasaidia kubadili uamuzi wa Mahakama?

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Siku ya jana mbele ya Mheshimiwa Jaji Wilfred Dyansobera wajumbe wa bodi ya Wadhamini ya CUF ya Lipumba waliitwa kusikilizwa maombi yao ya kumtaka Jaji Dyansobera ajitoe kusikiliza mashauri yote yaliyombele yake na kumuomba Mheshimiwa Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma atumie mamlaka yake ya kiutawala (Administrative Steps/Order) kumwondoa na kuwapangia Jaji mwingine kwa madai kuwa hawana imani nae baada ya kubatilisha kufukuzwa uanachama kwa waliokuwa wabunge wa viti maalum.

Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi, CUF wakiongozwa na Profesa Ibrahim Haruna Lipumba pamoja na Thomas Malima, Peter Malebo , Hajira Omar Silia, Aziz Issa Dagheshi, Abdul Rajab Magomba, Amina Thomas Mshamu, Asha Said Suleiman, Musa Haji Kombo, Salha Hilal Mohamed na Suleiman Makame Issa.

Wajumbe hao wote walifika jana mbele ya Jaji isipokuwa Hajira Omar Silia na Aziza Issa Dagheshi ambao inasemekana wamejiuzulu nafasi zao kutokana na msuguano mkubwa wa kukosa nafasi za kuteuliwa kuwa Wabunge wa Viti Maalumu hivi karibuni.

> Mahakama baada ya kusoma na kuzipitia kwa makini barua zao mbili zenye Kumb. Na. CUF/AK/DSM/RPP/28/2017 ya Tarehe 30/8/2017 na Kumb.Na.CUF/AK/DSM/RPP/27/2017 ya Tarehe 27/17/2017 Mahakama ilionekana zina matatizo Kisheria na baada ya mjadala mkali wa kisheria na Wasomi Mawakili (The Learned Advocates) akiwemo Msomi Wakili Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gabriel Malata, ilionekana haziwezi kujadiliwa na kuwa kumbukumbu ya Mahakama. Ifahamike kuwa Mahakama ni nyumba ya kumbukumbu (House of Records).

> Mahakama imewaagiza wajumbe hao kwenda kufanya marekebisho na hivyo kuandika upya malalamiko yao kwa kuzingatia kumbukumbu za kila Shauri. Aidha wawapatie wadau wote kwa kila shauri ili kama wakiona inafaa waweze kuwasilisha majibu yao kimaandishi kabla ya siku iliyopangwa kusikilizwa mashauri hayo wanayolalamikia.
 
Profesa Ibrahimu Juma
Profesa Ibrahim Haruna Lipumba

mzee wa buguruni anataka kutembelea nyota ya majina
 
Siku ya jana mbele ya Mheshimiwa Jaji Wilfred Dyansobera wajumbe wa bodi ya Wadhamini ya CUF ya Lipumba waliitwa kusikilizwa maombi yao ya kumtaka Jaji Dyansobera ajitoe kusikiliza mashauri yote yaliyombele yake na kumuomba Mheshimiwa Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma atumie mamlaka yake ya kiutawala (Administrative Steps/Order) kumwondoa na kuwapangia Jaji mwingine kwa madai kuwa hawana imani nae baada ya kubatilisha kufukuzwa uanachama kwa waliokuwa wabunge wa viti maalum.

Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi, CUF wakiongozwa na Profesa Ibrahim Haruna Lipumba pamoja na Thomas Malima, Peter Malebo , Hajira Omar Silia, Aziz Issa Dagheshi, Abdul Rajab Magomba, Amina Thomas Mshamu, Asha Said Suleiman, Musa Haji Kombo, Salha Hilal Mohamed na Suleiman Makame Issa.

Wajumbe hao wote walifika jana mbele ya Jaji isipokuwa Hajira Omar Silia na Aziza Issa Dagheshi ambao inasemekana wamejiuzulu nafasi zao kutokana na msuguano mkubwa wa kukosa nafasi za kuteuliwa kuwa Wabunge wa Viti Maalumu hivi karibuni.

> Mahakama baada ya kusoma na kuzipitia kwa makini barua zao mbili zenye Kumb. Na. CUF/AK/DSM/RPP/28/2017 ya Tarehe 30/8/2017 na Kumb.Na.CUF/AK/DSM/RPP/27/2017 ya Tarehe 27/17/2017 Mahakama ilionekana zina matatizo Kisheria na baada ya mjadala mkali wa kisheria na Wasomi Mawakili (The Learned Advocates) akiwemo Msomi Wakili Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gabriel Malata, ilionekana haziwezi kujadiliwa na kuwa kumbukumbu ya Mahakama. Ifahamike kuwa Mahakama ni nyumba ya kumbukumbu (House of Records).
Walitakiwa hoja yao waipeleke juu kwa waliowaweka Keisha maagizo ya kumuondoa yatokee huko kwenda mahakamani, ingependeza zaidi.
 
Back
Top Bottom