No 0ne
Member
- May 22, 2014
- 96
- 104
Kama ilivyo sasa tupo kwenye awamu ambapo serikali inasisitza sana juu ya viwanda na uwekezaji mkubwa sana umefanyika na tunaona viwanda Vingi vikijengwa katika mkoa wa Pwani.
Lakini wawekezaji wakubwa wamekuwa ni wachina wahindi na wazungu. Wabongo wenye viwanda ni wachache sana.
Sababu kubwa ya kuandika Uzi huu ni kuwa ingawa kweli wachina na wahindi wamewekeza kwetu ila bado tunachangamoto kubwa sana. Baadhi ya changamoto hizo ni: Utumiaji mkubwa wa vibarua wa bei rahisi(cheap labour).
Malighafi nyingi wanaleta kutoka kwao(import) tena kama mchina ndo kabisaa yeye kila kitu analeta kutoka kwao hivyo hivyo bado Tanzania inanufaika kwa kiwango kidogo sana.
Kazi nyingi zenye ujira mkubwa hupeana wao kwa wao nakupa mifano, Angalia jinsi wachina wengi wanawaleta wenzao kutoka China kuja kufanya kazi katika viwanda vilivyoanzishwa na wenzao na wanalipana vizuri sana na wengine hata elimu hawana na wakati nchii hii ina tatizo kubwa tu la ajira, sio tu wachina, nenda kwenye viwanda vya kina MO, Bakhresa uone wahindi wanakula mashavu na wabongo wanaishia kuwa watumwa tu kwa kufanya kazi za vibarua...... Ushawahi kukutana na watu wanatatafuta mawazo ya kibiashara?
Na tena unasikia wakisema kuna hela nyingi sana lakini tumekosa mawazo ya kibiashara ningewashauri watu kama hawa waanzishe viwanda tu.
Hivyo basi, KAMA MTANZANIA MWEUSI HATOWEZA KUWEKEZA KATIKA NCHI YAKE MWENYEWE BADO SANA KUPAMBANA KATIKA VITA YA UCHUMI. Kama na wewe mwanajamii umeshawahi kuziona changamoto za hawa wawekezaji kutoka njee karibu kwa maoni.