JE KUWA NA MWANAMKE/MWANAUME MWENYE GUNDU?

Eagle J

Member
Jan 30, 2020
27
51
katika harakati zetu za maisha kuna mengi kama wanadamu tunakutana nayo/pitia kufikia malengo yetu ya maisha, pia katika malengo yetu unajikuta unapata mwenza/mchumba/mpenzi ila muweze jenga maisha. Katika mahusiano yenu unakuja kuona mabalaa yanakuandama tu na hausogei kimaendeleo kama ulivyokuwa na mpenzi X baadae jamii inakuambia mpenzi ulienae ana gundu kwako ndio maana husogei na ukicheki umezama mwili mzima

jeumeshakutana na mtu wa namna hii? ulijuaje ? na ulifanyaje kujinasua bila kujua yeye ndio gundu kwako?

Je ina uhusiano na nyota (tarehe za kuzaliwa)
 
Sijawahi kuwa kwenye mahusiano nikahisi mwanamke niliyenae ana gundu/nuksi, isipokuwa mwanamke wangu niliyenae namuona kama ana bahati sana tangu nilipokuwa nae naseleleka tu kuelekea mbele! Ile kumuweka tu ndani nikapata kazi na mambo mengine mazuri!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nachoona kuna wanawake ukiwa nao maisha yanakunyookea kila unachogusa kitu kinatiki...alafu kuna wale mambo hayaendi kila unachogusa mambo yanakuwa jiwe
 
Kuna wanaume wana gundu. Ukiwa nae husogei. Ukiachana nae ndo kama kakuachia magundu buku, unakua mtu usieleweka.
Kama mshana anavyosema bora uoge maji ya chumvi kuondoa gundu la huyo mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata marafiki wakawaida awe Ke au Me ...wapo...ukishawaelewa unajichomoa taratibu.
 
Honestly, Siaminigi haya mambo lakini nakumbuka miaka flani hivi nipo chuo nilikuwa na date na Manzi mmoja hivi....

Aisee sijui ndio ilikuwa ana nyota yule manzi au vipi maana ilikuwa kila nikikutana nae lazima nipate deal la hela... sio masihara hii ni live kabisa.

Nakumbuka siku moja nimekaa sina maisha nikamcheki aje ghetto tupashe kidogo... ile tupo kwenye mechi napokea simu ya jamaa wangu mmoja ananipa mishe ya hela ndefu.

Too bad tulikuja kuachana lakini maisha yangu yanaendelea fresh tuu.

#Bagwell
 
Back
Top Bottom