Je, kusubiri tupate herd immunity ni njia sahihi ya kukabiliana na #COVID19TZA?

magu2016,

Shida ni kwamba haijulikani kama waliopona wanakuwa protected kupata reinfection. Na kama wanakuwa protected haijulikani ni kwa muda gani. Na ni kiasi gani cha antibodies kinatakiwa Kiwe cut-off points kuonyesha huyu mtu yupo protected. Kuna Virusi wengine wa Corona( sio Covid-19) mtu akipata maambukizi anadevelop Kinga ya miezi sita na wengine hadi miezi 18, kutegemeana na aina ya kirusi.

Tatizo la virusi huwa ni kubadilika badilika kwao. US huwa wanatoa chanjo ya flu ( influenza virus), lakini wanachotarget zaidi ni kuzuia severity tu ya ugonjwa na sio kukinga. Ukiangalia uwezo wa vaccine hiyo kukukinga na flu ni chini ya 50%

Kwa hiyo Safari bado ni ndefu sana


Sent using Jamii Forums mobile app
Ulichoeleza mkuu ni sawa kabisa lakini COVID-19 imeonyesha kuwa ni virus ambaye hawezi kumsumbua mtu mwenye kinga (immune) nzuri ndiyo maana asilimia kubwa waonakufa na virus huyu ama wanakinga dhaifu au wana mangonjwa mengine yanayoshambua mfumo wa kupumua. Hivyo bado COVID-19 utathibitiwa kirasi sana karibuni ndiyo maana hata majaribio ya chanjo yameanza mapema sana.
 
Halafu nyie mmenielewa vibayaaaa.Mnafikiri nipo pro Herd immunity in Tanzania.
Hiyo comment nilikuwa namjibu mtu aliesema duniani hakuna nchi iliyoamua kufanya process ya kujipatia kinga hiyo. Ndo nikamjibu Sweden wameamua kila kitu kiende kama ilivyokuwa ili kupata Herd immunity.
I was actually correcting you that Sweden has closed schools,puds etc
 
Hiyo bold hapo ni Wrong kwa njia zote, iwe ni Kisarufi, Kimanti na hata kielimu.
Hakuna ugonjwa unaitwa "herd community"
Kuna uwezekano hujanielewa tu labda kiswangilishi ndiyo imeleta taabu. Sina maana ya kuwa herd immunity ni ugonjwa bali nilikuwa na maana ili utambue huyu anakinga lazima augue kwanza na kupona au apimwe antibodies zake kama ambavyo wanafanya sasa Marekani. Ila sijaelewa una maana gani na "Herd Community"?
 
kuna model nimetumia kucalculate. principles of herd immunity and social distancing

Swali muruwa sanaa..?!!
Kifupi hakuna hoja hapaa, hiyo mifano aliyotoa haina reference na mada imejikita kwenye personal Opinion kulingana na uwelewa binafsi na sio Medical Hypothesis
 
I was actually correcting you that Sweden has closed schools,puds etc
Shule hazijafungwa.Watoto wanakwenda shule kama kawaida. Only vyuo na highschool ndo wamefunga kwa kusoma online.
Primary school,watoto wanakwenda shule kama kawaida.Bar restaurants vyote vipo wazi.
 
Katika immunology ya kila siku, sterile immunity is hard to achieve, sijui kama kuna ugonjwa ambao victim wake wamewahi ku acquire sterile immunity by natural infection todate! (stand to be corrected here). Hivyo huwezi kuleta majaribio ambayo hayako supported na science! Utaua watu wengi sana
Ndiyo sababu tunapinga kufanyika kwa jaribio LA kuzembea maambukizi ya COVID-19 tukitegemea herd immunity kujijenga kwa watakaosurvive.Huo utakuwa ni unyama kama wa Atomic Bomb.
 
Katika immunology ya kila siku, sterile immunity is hard to achieve, sijui kama kuna ugonjwa ambao victim wake wamewahi ku acquire sterile immunity by natural infection todate! (stand to be corrected here). Hivyo huwezi kuleta majaribio ambayo hayako supported na science! Utaua watu wengi sana
supporting herd immunity bila vaccine ni gemocide.
Kwaanza ugonjwa umeonesha kuna chances za reinfection so haiwez kuwa rahisi
 
Hiyo bold hapo ni Wrong kwa njia zote, iwe ni Kisarufi, Kimanti na hata kielimu.
Hakuna ugonjwa unaitwa "herd community"
Mbona kama ww ndio unakosea? Yeye kasema njia pekee ya kujua kuwa.mtu.huyu ka-acquire herd immunity ni augue na kupona. Kuugua meansaugiuee ugonjwa husika
 
Ulichoeleza mkuu ni sawa kabisa lakini COVID-19 imeonyesha kuwa ni virus ambaye hawezi kumsumbua mtu mwenye kinga (immune) nzuri ndiyo maana asilimia kubwa waonakufa na virus huyu ama wanakinga dhaifu au wana mangonjwa mengine yanayoshambua mfumo wa kupumua. Hivyo bado COVID-19 utathibitiwa kirasi sana karibuni ndiyo maana hata majaribio ya chanjo yameanza mapema sana.
You are wrong. Mtu yeyote anaweza kusumbuliwa ingawa hao.uliowataja wataathirika kwa haraka zaidi.

Iko.hivi sisi hatujipimi afya kujua tuna.hali.gani. unaweza kujiona huna kansa wala.hiv wala.presha wala asthma kumbe una tatizo jingine linakuwa bila ww kujua. Na ukipata covid19 ikakupelekesha.

Ushauri wangu tupate mlo kamili kila siku na tufanye mazoezi
Mbali.na hapo kuna blood groupa.ambazo ni vulnerable kwa diseases. Hilo tusiliunder estimate
 
Hata huko Uingereza hakuna lockdown, kuna isolation na self isolation na ukipatikana mgonjwa kuna Quarantine. Tena quarantine yao ina stages. Hata ukikutwa positive Kwanza unabaki nyumbani mpaka ufikie stage ya kuwa taabani ndiyo unapelekwa hospital kusaidiwa kupumua tu. Hakuna dawa ni msaada tu wa jupumua na kutibiwa mambo mengine yanayojitokeza lakini Corona kama Corona bado hana dawa.

Tusidanganyane, hata Tanzania mpaka sasa ndiyo tunafata mfumo huo tena sisi tunafata vizuri zaidi kwani tunasisitizwa tujifanyie self isolation (kama alivyofanya Mbowe) na tujikinge wenyewe kwanza na tujaribu dawa na tiba za asili, tusibweteke. Mpaka uwe taabani wa kusaidiwa ndiyo unaachwa hospital. Hili haya Ummy Mwalim kaliongelea. Na hata Rais alisisitiza sio mtu yupo "positive" tu na ni mzima basi awekwe tu quarantine.

Kuwa "positive" kwenye vipimo hakumaanishi ndiyo "death certificate". Kuna maanisha immunity yako imeshaanza kufanya kazi ya kushindana na virusi au ilifanya kazi ya kushindana na virusi na si lazima viwe vya covid-19. Inaweza kuwa virusi vya sars covid-2 au vingine vyovyote vile.

Soma zaidi...

Can you become immune to the coronavirus? A doctor weighs in
Asante kwa elimu
 
Njia yoyote inayiyofatwa au itayogundulika hata ya chanjo, ni eventually kuiharakisha "herd immunity" iwe faster.

Immunity itakuwepo tukitaka tusitake Kwa njia yeyote ile. Hakuna virus anaepiganwa nje ya mfumo wa kuwa na immune nae.

Tusijidanganye.
@ faizafoxy sipingi swala la immunity kuwepo hata kidogo. Na najua herd immunity is what the whole world is looking at im a sense kwamba watu wapate self immunity.

Lakin ninachopinga ni jins tunavyoacha ugonjwa uenee freely while system yetu ya afya tunaijua.na pia tunajua kuwa watanzania wengi wana underlying medical condition na uoatikanaj wa mlo kamili.ni.shida.

Kwasasa hivi focus yetu ingekuwa ni ku flattem the curve. Elimi zaid na safe practices
Plus isolation of the sick ones
 
Wao wanafanya zile basics. Mfano kunawa mikono,social distance. Ila Shule,kazi,usafiri,bar vinafanya kazi. Wana vifo vingi kuliko nchi yeyote hapo Scandinavia. Ila wameamua kujitoa mhaga. Watu wengi waugue ili baadae maambukizi yapungue.

Ndo nikasema kwetu Tanzania haitawezekna kutokana mpaka sasa hakuna vaccine na pia nchi yetu mfumo wa huduma ya afya ni uozo mtupu. Hivyo mpaka ujenge hiyo kinga utakuwa umeua raia wengi mno. Mimi naona catastrophe kabisa.
Umeshindwa kutoa 'source' inapoonyesha hii ndio sera waliyoamua itumike. weka hata habari iliyochapishwa gazetini ikiripoti juu ya sera hiyo ya kuitegemea 'herd immunity'.
Wewe umekurupuka tu na kuhitimisha kuwa ndio uamzi waliouchukua; "kuruhusu watu waambukizwe"?
Kawadanganye mazuzu wa Tanzania tunaoamini kila kitu kisemwacho bila kuhoji wala kuelewa kinachozungumziwa!
 
Wanabodi salaam!

Leo nimekuja kwenu ninataka tujadili kuhusu njia za kupambana na #COVID19TZ.
Katika hali.isiyo rasmi inaonekana tayari wizara ya afya kwa baraka za mheshimiwa rais imeamua kutatuta tatizO hili kwa njia ya herd immunity.

Herd immunity ni njia ya kitaalam ya kuacha ugonjwa wa kuambukiza usambae kwenye jamii bila YA kuchukua tahadhari zozote zile kwa nia ya kujengea watu kinga ya mwili yenye uwezo wa kukabiliana na ugonjwa husika. njia hii ni nzuri kwa sababu hujenga natural immunity kwa watu ama jamii lakini ni njia mbayo inapingwa sana na wanaharakati wa masualaq ya haki za binadamu pamoja na wana sociolojia kwasababu huua watu wengi na husababisha wagonjwa wengi kwa makusudi.

kwa kuzingatia hali yetu ya maambukizi ya sasa unaweza kuona kwamba serikali imeacha ugonjwa uenee miongoni mwa jamii hii wakiwa na nia ya kwamba labda wale watu dhaifu sana kiafya watakufa na watabaki watu wenye nguvu na afya (strongest)

kauli ya rais kwamba hawez kufunga DSM kwasababu ndio kitovu cha uchumi cha taifa hili, na kwamba watu wajifukize na kuomba Mungu kinatafsiriwa na wengi kuwa ni sawa na kusema "let the weaker die and the strongest survive" or "survive for the fittest"

kitaalamu kutokana na model kadhaa ambazo zimekuwa zikipredict kuhusu outcome ya herd immunity kwa nchi mbalimbali zilizoendelea ilionesha kwamba nchi kama uingereza wangekufa watu takriban 500,000 wakaamua kuacha njia hiyo na kuamua sasa lockdown, close of borders, isolate the sick and followups kwa contact person wa victims iwe ndio solution. na wakifanya hivi watapunguza vifo sio chini ya 400,000.

kwa Tanzania inaonekana kuwa lockdown iwe partial ama complete n ngumu kwa kuhofia kaukosa mapato ya taifa lakin pia isolation of the sick individuals imekuwa ngumu sana kwasabb ya miundombinu hafifu. upatikanaji wa vifaa tiba (PPE) nao ni changamoto sana kwa wauguzi na hata mashine za kupumulia (ventilators).

sasa hoja yangu ya msingi ni hii hapa kulingana na estimation za model za kukadiria matokeo ya herd immunity inaonesha kuwa tanzania tutapoteza si chini ya watu millio n2 ikiwa tutaacha ugonjwa uenee na watu si chini ya milioni 3 wataugua huu uginjwa. na watu zaidi ya million 10 watabaki wakiwa salama na kinga hii ni kama tuu wakati ugionjwa unaenea basi kuna kauwa na social distancing kati yetu.

ikiwa hatutaweza social distancing basi watu si chini ya 6 million watakufa kwa ugonjwa (yaan mkoa wote wa dsm) watu zaidi ya millioni 9 wataugua.

kutokana na hali hii je serikali kwa uwezo wa hospital zetu TUTAWEZA KUKABILIANA NA HALI HII?
Tunao wauguzi na madaktari wa kutosha? vipi kuhusu madaktari wataokufa kwenye hili zoezi? serikali imejipangaje?

je wanaharakati wetu wa haki za binadamu wamekubaliana na hali hii?

mimi binafsi bado ninaona tunao uwezo wa kupata njia nzuri zaidi ya kudeal na huu ugonjwa.
bado ninabaki na msimamo kuwa partial lockdown, isolation of the sick ones na followup kwa contact person wa victims ni suluhisho. huku tukiendelea kupractice safe practices kama kunawa mikono na kuvaa barakoa kila mara.
You are right, although the government is reluctant to completely close the borders. Partial lock-down does not help much if the country borders are open. Tumechelewa. Tungefunga mipaka yetu mara tu ungonjwa uliporipotiwa. Ninaishauri selikali iendelee kutoa taarifa kuhusu tatizo hili ili wananchi waendelee kuchukua hatua za kujikinga. Kunyamaza kunawafanya raia wengine wafikirie kuwa corona imeondoka.
 
Very soon viwanja vya michezo vitageuzwa kuwa makeshift hospitals,. Approach ya serikali ya Mzee Magu itafanya tupoteze wapendwa wetu wengi sana tukiwemo hata jf members.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikutegemea kuwa bado mnawatetea hawa viongozi waliolazimisha Cororna ienee Tanzania nzima wakidhani watu watapata Herd Immunity kwa kuugua.Lugha ya kutelekezwa ni ngumu kuielewa hadi unifananishe na msichana/mwali/mwari wa Kizaramo?Nitake radhi maana sijazoea kutukunana,changia mada na hizo lugha za matusi wapelekee mashoga zako.
Tujadili uzembe wa walioapa kututumikia sisi wananchi,badala ya kutimiza wajibu wao wanajifanya wapo likizo/mapumziko yasiyo na kikomo wakati Taifa likiteketea kwa COVID-19.Unaridhishwa na hali hiyo?
 
Mbona kama ww ndio unakosea? Yeye kasema njia pekee ya kujua kuwa.mtu.huyu ka-acquire herd immunity ni augue na kupona. Kuugua meansaugiuee ugonjwa husika

Hakuna mtu anaweza kupata (aquire) herd community)! labda hujapata ni nini hasa concept ya herd community
 
Back
Top Bottom