Je, kusubiri tupate herd immunity ni njia sahihi ya kukabiliana na #COVID19TZA?

gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,274
20,673
Wanabodi salaam!

Leo nimekuja kwenu ninataka tujadili kuhusu njia za kupambana na #COVID19TZ.
Katika hali.isiyo rasmi inaonekana tayari wizara ya afya kwa baraka za mheshimiwa rais imeamua kutatuta tatizO hili kwa njia ya herd immunity.

Herd immunity ni njia ya kitaalam ya kuacha ugonjwa wa kuambukiza usambae kwenye jamii bila YA kuchukua tahadhari zozote zile kwa nia ya kujengea watu kinga ya mwili yenye uwezo wa kukabiliana na ugonjwa husika. njia hii ni nzuri kwa sababu hujenga natural immunity kwa watu ama jamii lakini ni njia mbayo inapingwa sana na wanaharakati wa masualaq ya haki za binadamu pamoja na wana sociolojia kwasababu huua watu wengi na husababisha wagonjwa wengi kwa makusudi.

kwa kuzingatia hali yetu ya maambukizi ya sasa unaweza kuona kwamba serikali imeacha ugonjwa uenee miongoni mwa jamii hii wakiwa na nia ya kwamba labda wale watu dhaifu sana kiafya watakufa na watabaki watu wenye nguvu na afya (strongest)

kauli ya rais kwamba hawez kufunga DSM kwasababu ndio kitovu cha uchumi cha taifa hili, na kwamba watu wajifukize na kuomba Mungu kinatafsiriwa na wengi kuwa ni sawa na kusema "let the weaker die and the strongest survive" or "survive for the fittest"

kitaalamu kutokana na model kadhaa ambazo zimekuwa zikipredict kuhusu outcome ya herd immunity kwa nchi mbalimbali zilizoendelea ilionesha kwamba nchi kama uingereza wangekufa watu takriban 500,000 wakaamua kuacha njia hiyo na kuamua sasa lockdown, close of borders, isolate the sick and followups kwa contact person wa victims iwe ndio solution. na wakifanya hivi watapunguza vifo sio chini ya 400,000.

kwa Tanzania inaonekana kuwa lockdown iwe partial ama complete n ngumu kwa kuhofia kaukosa mapato ya taifa lakin pia isolation of the sick individuals imekuwa ngumu sana kwasabb ya miundombinu hafifu. upatikanaji wa vifaa tiba (PPE) nao ni changamoto sana kwa wauguzi na hata mashine za kupumulia (ventilators).

sasa hoja yangu ya msingi ni hii hapa kulingana na estimation za model za kukadiria matokeo ya herd immunity inaonesha kuwa tanzania tutapoteza si chini ya watu millio n2 ikiwa tutaacha ugonjwa uenee na watu si chini ya milioni 3 wataugua huu uginjwa. na watu zaidi ya million 10 watabaki wakiwa salama na kinga hii ni kama tuu wakati ugionjwa unaenea basi kuna kauwa na social distancing kati yetu.

ikiwa hatutaweza social distancing basi watu si chini ya 6 million watakufa kwa ugonjwa (yaan mkoa wote wa dsm) watu zaidi ya millioni 9 wataugua.

kutokana na hali hii je serikali kwa uwezo wa hospital zetu TUTAWEZA KUKABILIANA NA HALI HII?
Tunao wauguzi na madaktari wa kutosha? vipi kuhusu madaktari wataokufa kwenye hili zoezi? serikali imejipangaje?

je wanaharakati wetu wa haki za binadamu wamekubaliana na hali hii?

mimi binafsi bado ninaona tunao uwezo wa kupata njia nzuri zaidi ya kudeal na huu ugonjwa.
bado ninabaki na msimamo kuwa partial lockdown, isolation of the sick ones na followup kwa contact person wa victims ni suluhisho. huku tukiendelea kupractice safe practices kama kunawa mikono na kuvaa barakoa kila mara.
 
sasa jambo la ajabu ninaona hata waziri kingwangala licha ya kwamba ni medical Dr pia anaongea kirahisi tu kwamba mwongozo utolewe watu turudi kwenye shugfhuli zetu kwasabbu gonjwa hili si la kuisha leo ama kesho.

na mwigulu alipendekeza zisitolewe data za wagonjwa tena na rais akasema wazi kuwa haWEZ KUFUNGA DAR watu wajifukize na kuomba MUNGU: Suprisingly jana usiku makaburi ya kisutu wamezika watu wanaokadiriwa 20 kwa sababu ya covid19 yaan imekuwa ni utaratibu wetu kwasasa.

hali hii inaaminisha kuwa tunategemea herd immunity iwe ni suluhisho na mwenye nchi yake yuko jamhuri ya chattle land.

tuamke watanzania kudai haki yetu ya kuishi

angala
 
Herd immunity kwa Tanzania haifai. Kwanza hakuna huduma bora za kuwahudumia hao watakaozidiwa mpaka kushindwa kuhema. Nchi nzima ventilators hazizidi tano.

Hakuna PPE. Wahudumu wengi watakufa au kuugua. Nani atahudumia? Na hii itapelekea hata wagonjwa wengine nje ya Covid 19 kukosa huduma.

Hii ni njia ya kwenda kaburi kwa mamilion ya Watanzania. Mungu anipe uhai nione Tanzania itabaki na wananchi wangapi?
 
Mkuu naomba ufafanue maswali yafuatayo.

1. Je, serikali imeweka wazi kwamba imeamua kuacha COVID19 isambae ili kujenga kinga kwa jamii yote? Au intelijensia yako ndo inaonesha serikali imekusudia iwe hivyo?

2. Mbali na chanjo (vaccination program), kuna ugonjwa wowote umewahi kuzuilika/kutokomezwa kwa herd immunity inayotokana na "field infection"?
 
Hakuna mahali popote hapa duniani mpaka sasa ambapo Herd immunity imeweza kufaa katika Corona. Nina uhakika mzee Meko hajui hata maana ya herd immunity sembuse mantiki.

Ni uwendawazimu kuwaza kichawi halafu ukategemea matokeo ya kisayansi. Sisi tumeambiwa tujifukize na virusi vitapasuka pasuka kwa mvuke wa joto!
 
Back
Top Bottom