Je, kuna umuhimu wowote wa watu kuombeana kheri na baraka katika Maisha yao

Je, kuna umuhimu wowote wa watu kuombeana kheri na baraka katika Maisha yao

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
31,636
Reaction score
81,533
Je kuna umuhimu wowote wa watu kuombeana kheri na baraka katika maisha yao?

jibu ni ndiyo .

Katika MAISHA chochote kinachokufikia wewe kuna sehemu kilikuepo na kuna sehemu kimetoka hadi kukufikia wewe.

Ikiwemo Pesa n.k. Hivyo ni muhimu kuelewa everything is connected , kila kitu kimeunganishwa sehemu.

Ikiwa utaelewa hii concept.

Utapapata picha kuhusu mzunguko wa maisha

Mfano ukimuona MTU ana hustle ili apate kitu fulani usimkatishe tamaa au ku-block njia yake kwa kufanya hivyo unakuwa sio Una-block njia ya MTU mmoja bali unakuwa ume-block njia za watu wengi Sana .

Unaweza kuona MTU Kama Diamond (Msanii) kupitia taasisi yake ya Wasafi ameajiri watu wengi ambao wanaendesha maisha yao kupitia wasafi .

Je angebaniwa na kupigwa block which means ni njia nyingi Sana za watu zingekuwa zipo block hadi Leo hii.

Hivyo ikiwa utajifunza kuwaombea watu kheri na baraka ili wafanikiwe Mara dufu sio tu watafanikiwa wao Ila yawezekana kabisa kufanikiwa kwao kukakufikia hadi wewe. In difference ways.


Ila jamii zetu hazitambui huu mzunguko wa maisha.

Mfano, Kijana Jobless aliyepo mtaani . Akipata Kazi , maana yake atapanga Sehemu atalipa kodi , hiyo kodi mwenye Nyumba ataitumia kulipia watoto wake Ada ya Shule , hiyo Ada ya Shule itatumika kumlipa Mwalimu mshahara na huo mshahara Mwalimu atautumia kulipa bill zake na kidogo atawatumia wazazi wake waliopo kijijini na wao watanunua sukari n.k unaweza kuutazama huo mzunguko ulivyo.

Au unauza Magari, na anayekuja kukunua kwako Magari anamsubiria mteja wake wa kununua korosho amuingizie hela na huyo Mteja wake hiyo hela anategemea kuipata baada ya kulipwa na Mteja wake aliyepo nchi Fulani Ila ndani ya nchi Fulani kuna shida ya utumaji wa hela kwenda nje.

So changamoto ya sehemu Fulani inaweza kukuathiri hadi wewe na mafanikio ya sehemu Fulani pia yanaweza kukuathiri .

so everything is connected , kuombeana kheri na kutakiana Amani ni muhimu Sana.

Hivyo kuwaombea watu mabaya ni sawa sawa na kujiombea wewe mwenyewe hayo mabaya the same

Kuwaombea watu mazuri ni sawa sawa na kujiombea wewe mwenywe .

Be positive and pray to each other, we are on the same way but different destination

Thank you.

FB_IMG_17444409549909634.jpg
 
Back
Top Bottom