Je, Kuna umuhimu wa kuanzisha mahakama ya mafisadi?

bizzle for shizzle

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
1,012
741
Wadau wa JF,

Napenda kuuliza pia kuelimishwa juu ya hili hivi kuna umuhimu gani wa kuanzishwa kwa mahakama ya kifisadi kama hali yenyewe ndio hii.

Hivi kweli mahakama imeeakuta na hatia Mh Daniel Yona na Basil Mramba wa kuliinguzia taifa mabilion ya fedha halafu leo tuna ambiwa wamepewa kifungo cha nje cha kufanya usafi hivi hii ina makesense kweli?

Sasa kuna haja gani ya kuanzisha mahakama ya mafisadi kama tutakuwa tunawaonea huruma mafisadi hii sio hakhi hata kidogo na haingii akilini kwa mtu yeyote leo tuna ona masikini anaiba kuku kwa ajiri ya kitoweo nyumbani anakamwata ana hukumiwa miaka 10 jela na lakini fisadi aliye iba mabilion ya watanzania eti ana hukumiwa miaka mitatu tena kwa kifungo cha nje wana kiita cha kufanya shughul za jamii.

Jamanai mahakimu mtende haki watanzani hawajaridhishwa na hukumu hiyo ya miaka mitatu tena ya kufungo cha nje maana ndani sijui walikaa miezi mitatu tu kwa kweli inasikitisha.
 
Hakuna haja kwa kuwa watahukumiwa na majaji wale wale ambao walikuwa wanapiga makofi walipoambia na Magufuli haraka sana wahukunu kesi za watu ili awapatie b.250 za kufanya kazi.
 
Hakuna haja kwa kuwa watahukumiwa na majaji wale wale ambao walikuwa wanapiga makofi walipoambia na Magufuli haraka sana wahukunu kesi za watu ili awapatie b.250 za kufanya kazi.
Ni kweli mkuu naona itakuwa ni mwendo wa kupoteza fedha tu maana hakuna jipya litakalo fanyika na ungana na wewe moja kwa moja
 
Labda wanatafuta watu wa kufanya usafi kwenye maeneo ya uma ndio maana wamekazana na hii mahakama ya mafisadi, ila hakuna magereza ya mafisadi.
 
Hakuna haja kwa kuwa watahukumiwa na majaji wale wale ambao walikuwa wanapiga makofi walipoambia na Magufuli haraka sana wahukunu kesi za watu ili awapatie b.250 za kufanya kazi.

Hivi ahadi aliyoitoa rais kwa majaji ya kuwapa robo ya trilioni moja itakayotokana na hukumu zao kwa washitakiwa haita influence maamuzi ya majaji mahakamani na hivyo kupelekea kutokutenda haki kwa wanaoshitakiwa? Nasema hivi kwa sababu wanaweza kutoa hukumu inayolenga kuwezesha serikali kupata hiyo trillion ambayo nayo itapelekea wao (yaani mahakama) kupata niseme "commission" ambayo ni robo ya makusanyo. Nadhani haikuwa sahihi rais kutamka mapema hiyo ahadi kabla ya hukumu na badala yake angesubiri hukumu itolewe ndipo atangaze kwamba robo ya malipo yatakayofanyika itaenda kusaidia shughuli za mahakama. Sana sana angehimiza kesi ziendeshwe haraka na kwa weledi.
 
Kwa kuwa walipiga makofi wakati anatamka hayo ndiyo maana tunasema hakuna haja ya hizo mahakama kwa kuwa majaji watakuwa ni hao hao waliokuwa wanapiga makofi. Labda kama watatoka kuke Ghana walikofukuzwa majaji kadhaa kwa sababu ya kujihusisha na rushwa.
 
For in future au kwa kipindi hiki?amfunge aliyekwapua mchuchuma??
Au mzee wa visenti maana ccm wote hakuna aliye hai hata yeye inaweza kumgeukia katika miradi ya vivuko na barabara.
 
Mafiasdi ndio hao hao wenye madaraka. Kuna haja gani ya kumhukumu mtu akafagie wakati kapoteza billions of money. Hii presidence ambayo mahakama zote zitafuata baadae. Kwani kkuza nyumba za serikali bei chee haikuwa ufisadi?
 
kwani zilizopo zinashindwa nn kuwakaba hao mafisadi hii nji bhana walianzisha takukuru lakini waliopo huko takukuru nao ni........ so hata hii mahakama haina maana tutatumia mafwedha kibao halafu humohumo pataibuka mafisadi
 
Inawezekana mkuu, inamaana baada ya utawala wake inakufa au inaendelea
Mmh! Hapo sasa. Kwa kuwa hata jaji mkuu na wengine hawakuweza kusimama na kutetea mhimili wao hii kitu inatia ukakasi. Tunajuaje hao majaji wa hiyo mahakama hawataamua kesi kwa matakawa ya rais kwa kuwa atawateua yeye? Narudia swali lako. Je, baada yake zitaendelea? Labda kama zitakuwa na ufanisi ambao mimi siuoni.
 
Hii inaitwa original komedi
 
Mleta mada subira ya vuta heri, itakapoanza hiyo mahakama ya mafisadi yapo mengi tutakayokuwa kwenye nafasi ya kuyafahamu kwa undani. Yona na Mramba walifungwa enzi za JK. Wakati huo hata wazo la kuwepo kwa mahakama ya ufisadi halikuwepo. Wazo hilo tumeanza kulisikia wakati wa kampeni za rais Magufuli. Mfumo mzima wa uendeshaji wa mahakama hiyo kwa sasa upo kwenye mchakato ili baada ya miezi kadhaa mahakama hiyo ianze kazi.
 
Majaji watakuwa hawa hawa au wengine? That is THE burning issue here. Unaweza kuwa na mahakama za michezo, ardhi, nyumba, mifugo, biashara na sasa mafisadi. Majaji na mahakimu ni wale wanaopokea orders kutoka mhimili mwingine au wataagizwa kutoka wapi? Ebu funguka.
 
Unao ushahidi wa hicho unachokisema?. Mbunge mmoja alifungiwa asihudhurie vikao viwili vya bunge kwa sababu ya hizo hizo habari ambazo mtu anaziongea mbele ya kadamnasi halafu anashindwa kutoa ushahidi. Ukitakiwa kuongea kwa kirefu uelezee jinsi majaji wanavyopokea orders unao uwezo wa kuuthibitishia umma?. Ni tusi kubwa sana kusema eti majaji wataagizwa, ni hawa hawa ambao wewe unapopata shida na kwenda mahakamani, wanatumia elimu zao katika kutatua shida zako.
 
Back
Top Bottom