Je kuna tulichojifunza kutokana na makosa ya operation tokomeza ujangili?.

masonya

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
968
759
Wakati wa utawala wa mzee Ali Hassan Mwinyi kuliawai kuwa operation kupambana na ujangili huko tunduru.niliwahi kukutana na dhahama ya mwanaoperation,wakati huo nilikuwa nasoma sekondari,askari mmoja akiwa ndani kombati aliniomba nimpakie kwenye baskeli(swala) nilikataa nikambia rim yangu si mzuri alinipiga vibao, fimbo .nikafanikiwa kukimbia na baskeli yangu nikapita njia za porin .wakat narudi nikaambiwa angenipata angeniwekea bangi.pamoja na matukio kama hili na watu kulishwa samaki wabichi ukikamatwa nao operation hii ilikuwa ni bora na ilifanyika kwa weledi.walikuwa akikumbia una bunduki unaitumia kwa ujangili ukikataa utatajiwa serial number na lini na wapi imetumika na nani alitumia.ukiendelea kubisha hapo ukakutana naAfande Lazima na Afande Aheri ya Mungu,utateseka.operation hii iliwashughulikia watu sahihi, kulikuwa na wasomalia wengi wanaishi nyumba moja ambao biashara yao kuu meno ya ndovu walishughulikiwa .tembo wakongezeka.nilimsamehe askari aliyenipiga kutokana ubora wa ujumla wa operation.
YA OPERATION TOKOMEZA
Labda nikuonyeshe jinsi gani askari wa hii operation wamekosa weledi katika intelejisia,miezi michache kabla kuanza rasmi .Gari ilitoka morogoro kupitia dar hadi tunduru kumfuata mfanyabiashara wa meno ya tembo ambayo yamekamatwa morogoro .wakamweka lupango wakampekua baadae wakaona ni watu wawili tofauti majina tofauti isipokuwa jina la ukoo.fedha zote za kodi walizotumia zaidi watu wanne kwanini upelelezi usingetangulia?
OPERATION TOKOMEZA ;imeua ,imebaka,imeumiza imeetesa na kila aina ya ubaya unaoujua pamoja na kudhulumu mali za watu.imedhulum na kuwaonea hata baadhi ya wanasiasa, Mh NCHIMBI ,Mh David mattayo hao kwa uchache imewanyang'anya haki yao ya kuwatumikia watanzania,kusafishwa pekee hakutoshi.LAKINI JE TUMEJIFUNZA?
Kwa muda sasa operation kama tokomeza inaendelea masasi na sasa ipo tunduru.MAJANGILI si wakuonewa huruma wanaua askari pori wetu,wanyama wanapaswa washukilikiwe ipasavyo.LAKINI sasa operation inarudia makosa yaleyale wanapiga watu ,watesa watu kudai rushwa ukifikishwa dar kama huna mamilioni ni balaa.hapa tunduru wamewakamata baadhi.
mfano wa juzi wameenda Nyumban kwa mtuumiwa ambaye ana biashara tunduru na masasi wamewapiga mlinzi,mtoto wake wa kike,shemeji yake,house girl na mwenyewe.hawakuwa na mwenyekiti ,mjumbe mtaa wala jirani usiku mwingi.mtoto wa kike aliwataka wawaue kwa kuwa hakuna haki wataingia bila hata mjumbe wa mtaa na kufanyia ukatli kama majambazi.askari wanne wakaondoka wakabaki wanne wakajana polisi wa kituoni.wakapekua wamechukua hela 11,700,000/=na kama US $2000.alipooji kosa lake,wamedai wametumwa na wakubwa kumkamta kwakuwa anaenda china mara kwa mara na ana magari soloon 2 na nissan safari moja old model na amejenga guest masasi hata mwenge ulienda kufungua mwaka jana ,ukweli china mara moja tu pasport inasema.jana kuna mzee amepigwa vibaya ameletwa ameumia anatuumiwa ana bunduki.SIWATETEI majangili lakin intelejensia vipi watuhumiwa wanapelekwa dar wanapingwa hela kutokana na hofu,mateso,vitisho. wanatoa mamilioni.WATANZANIA TUACHE KUPIGA DEAL KWA KILA JAMBO ZINAUMIZA WENGINE.mr Nyarandu umewapa madaraka tafadhali angalia ana-abuse power unafanya kazi kubwa na mzuri.

pamoja tujenge taifa linda maliasili zetu kwa sasa na baadae
 
Back
Top Bottom