Pole sana!! Kwa wale wote ambao walishawahi kuumia kwa ajili ya mapenzi wanafahamu maumivu ya mapenzi yanavyoumiza,maumivu ya mapenzi huumiza moyo, ubongo na hutapakaa kila kiungo ndani ya mwili wako hivyo maumivu ya mapenzi usiombe yakukuta maana utapungua kilo kwa kila siku zinavyokwenda na hata mambo yako ya msingi hayatakwenda vizuri......maumivu ya mapenzi siyo maumivu kama maumivu mengine kama ya kichwa,tumbo n.k kuwa utaweza kumeza dawa yeyote ile ya kupunguza maumivu na baada ya muda flani yatapowa hiyo ni NO ktk maumivu haya........ili uweze kupona pindi unapopatwa na jambo kama hili unatakiwa ufanye vitu hivi fuatavyo...
1.. Uzoeshe ubongo kumsahau yule aliyekuumiza kwa kujishughulisha na vitu mbalimbli kama michezo,kucheza games,
2.. Kaa mbali na vitu vyote vitakavyokupa kumbukumbu ya mpenzi wako kama vile cards,maua na hata sms zake kwenye simu futa nk..
3.. Hakikisha uingii ktk mapenzi mapema tena baada ya kuachwa na mpenzi wako kwani ni rahisi mno kumpata mpenzi fake atakayetaka kukuchezea tu na kukuacha hii yote ni baada ya kukugundua tu umeachwa na uko mpweke na atakuja kwa maneno mazuri ya kukupa matumain kwa mara nyingine kumbe umeingizwa ktk mkenge..
4.. Mwisho hakikisha pindi tu utakapoamua kuingia tena kwenye mapenzi mchunguze kwa makin mno utakayetaka kuunga nae uhusiano kwani dawa pekee ya maumivu yamapenzi ni kumpata mpenzi ambae atakae jua thamani yako,atakaekuheshimu na kukuthamini kama mtu pekee na muhimu ktk maisha yake,mtu huyo ndo maalum wa kukusahaulisha yale ya nyuma.
NB: kuumizwa ktk mapenzi kusikufanye ukashindwa kupenda tena,kila binadamu ameumbiwa pacha wake ambae wamefanana mioyo yao,muda ukifika utampata pacha wako huyo huenda mpenzi uliyekuwa nae si pacha wako uliyepangiwa kuishi nae ktk dunia hii ndo maana ameondoka, muhimu ni kujipa moyo wakati ukifika utampata mtu sahihi ktk maisha yako..
Ni maoni yangu tu waweza kuyachukua au kuyaacha!!