Je kuna masharti ya kuvaa SUTI?

Je kuna masharti ya kuvaa SUTI?

lukelo sakafu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2015
Posts
2,938
Reaction score
517
Wakuu, hivi kuna masharti yoyote ya kuvaa vazi la SUTI? Kwa sababu kuna watu wanasema eti ukivaa SUTI hautakiwi kufanya yafuatayo? Kupanda daladala? Kushika bomba kwenye basi, kugongea sigara, kula chakula bila kijiko, kunywa maji ya viroba, kula ugali, kuongea kiswahili, kutumia simu ya mchina,kuangalia tv ya chogo, kuvaa raba au buti, kulilia chenji, ubishana hadharani, kuulizia bili ya chakula. Je! Hii ni kweli? Maana hata mimi nimesikia tu mpaka naogopa kuvaa SUTI yangu mpya ya harusi maana wanaweza kunicheka,

Jamani nielewesheni
 
Wavaa suti ndio wezi siku hizi.
Mkuu uko moto sana utakuwa ni Shy land wewe
 
Last edited by a moderator:
wala kucheza miziki ya kukatikakatika marufuku
 
najua sheria moja tu usivae suti kama wasira
 
Kumbuka kutoa ile label kwenye mkono wengi huwa hawajui inatakiwa kutoka wanaivaa ikiwa inaonekana
 
ukiwa umevaa suti haitakiwi kucheka kwa sauti eti haahaahaaaaa huku umepanua limdomo inatakiwa kucheka huku umefumba mdomo tena unapiga mara mbili yaani mh mh, halafu unakaa kimya.
 
huruhusiwi kuvaa sutu halafu unaanza kula kula vitu barabarani kama vitumbua.
Huruhusiwi kuvaa suti halafu utembee kwa tz 11 huku ukivuja jasho.
Ukiwa umevaa suti hata ukiibiwa hairuhusiwi kumkimbiza mwizi huku ukipga kelele

unamkimbiza mwizi kimya kimya
 
Huruhusiwi kula magengeni au kunywa soda ndani ya chupa unatakiwa kumimina katika gilasi.
 
Ki ukweli bila ya mzaha si ruhusa kuvaa suti na tai siku ya jumamosi kuanzia asubuhi mpaka mid day.
Pili:uvaapo suti shati lazima liendane na suti.siyo suti nyeusi shati la njano.
Tatu;viatu vya suti huwa ni black
Nne:Ukikaa unafungua vifungo vya koti..ukisimama unavifunga kama afanyavyo Nambar One na JanuaryMakamba na pia Kamanda Mbowe.Wakati wa kupiga picha ukiwa umesimama unafunga vifungo..lakini siyo vyote.kuna suti one touch..two buttons and three buttons.hii ya mwisho ni kwa watu warefu wafupi haiwapendezi
 
Back
Top Bottom