Nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu sasa wenzetu wanakua na lengo moja linalotumia mda mrefu(mfano mpango wa china kutawala anga ifikapo mwaka 2050) ila hapa nyumbani tuna endeshwa na ilani ya CCM yenye mambo lukuki yasio tekelezeka.
Na chakushangaza zaidi imekua ikibadilika kila baada ya miaka mitano naomba niulize swali ivi ile sera ya kilimo kwanza ingepewa mda wa miaka ishirini na kufanya uwekezaji mkubwa katika zao la mpunga kwa kutumia pesa ilio tumika kujenga daraja la kigamboni kutengeneza irrigation system katika maeneo mbali mbali nchini tungekuwa wapi katika kuzalisha mpunga?
Na je tungepata pesa kisi gani kwa kuuza zao hili kwa majirani zetu? Tungeokoa pesa kiasi gani tunazotumia kuagiza mchele nje ya nchi?
Kwa kiasi hicho cha pesa nadhani tungejenga madaraja hata kumi na kipato cha wananchi kingeongezeka.
Nadhani sasa ni wakati wa wantanzania kubadirika kifikra je tunahitaji kuendelea kutumia ilani ya uchaguzi ya chama fulani