Je, kuna ''fukuto'' la kisiasa kati ya Mbunge na Meya katika Jiji la Arusha?

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
Baada ya kuangalia video nimegundua siasa za Arusha ni ngumu sana hasa kwa wanasiasa ambao ni vuguvugu!

Maelezo anayoyatoa Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro yanajenga picha inayoonyesha ndani ya nyumba yake ya kisiasa (CHADEMA) Arusha kuna mambo hayako sawa!

Meya Kalist anaposema waache siasa mpaka 2020 anakuwa na maana gani? Je, amekubaliana na kauli ya Rais Magufuli ambayo inapingana na mtazamo wa CHADEMA?

Meya Kalist anaposema ni ujinga kutoishukuru serikali ya Awamu ya Tano na Rais Magufuli kwa yale yanayofanyika Arusha anakuwa anatoa ujumbe kwa nani? Nani ambaye haishukuru Serikali ya Awamu ya Tano na Rais Magufuli?

Amemalizia kwa kusema, yeye hawezi kuacha kumshukuru Rais Magufuli na kama kuna watu wanachukia basi hilo ni tatizo lao!

Is the writing on the wall and the footprints are in the sand?

Video ya aliyoyasema Meya wa Jiji, Kalist Lazaro

 
Mkuu huyo kachuliwa saa 9 usiku chini ya mtutu na kulazimishwa kusema hayo Usiwe na hofu sisi wa Arusha Lema anatosha. Kalist ni mzuri sana ila ni jamii ya Dr Mihogo. Nafasi aliyonayo ni ya CHADEMA siyo yake
 
Hongera sana Meya Lazaro, ni jambo jema kupongeza mengi mema na mazuri ya awamu ya tano na kukosoa panapobidi.Huko ndiko kukomaa kiungozi tunajenga Tanzania iliyobora zaidi.
 
Hii NI habari mbaya kwa chadema! Mayor anayaona kakataa kuwa miongoni mwa wajinga
 
Hii NI habari mbaya kwa chadema! Mayor anayaona kakataa kuwa miongoni mwa wajinga
Amesema maneno hayo kama Meya sio kwenye kikao cha Chadema, unahitaji kujua tofauti ya Mwenyekiti wa ccm na rais wa Tanzania.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
mimi habari nilizonazo ni kwamba Lema hagombei tena ubunge mwakani, atakuwa mchungaji wa kituo cha SAFINA REDIO kule Mbauda
 
Back
Top Bottom