Je, kuna faida gani kupeleka ubalozi wetu Sudan?

rubibiman

Senior Member
Jul 5, 2015
111
44
Sudani na Tanzania ni Nchi ambazo zina historia ya ushirikiano ambapo 1962 ,mwaka mmoja tu baada ya kupata Uhuru kila Nchi ilifungua ubalozi wake,Tanzania ilifungua Khartoum-Sudan na Sudani ilifungua Dar-ssalaam

Tanzania.


mwaka 1985 Tanzania haikuwa na balozi Nchini Sudani mpaka sasa ampapo inajulikana balozi SILIMA HAJI KOMBO ameshateuliwa kuwa balozi Nchini Sudani.


Sudani na Tanzania ni miongoni mwa members walioanza na OAU 1963 huku wakiwa ni marafiki tangu kufunguliwa kwa balozi zao, miaka ya 70/80 kulikuwa na ushirikiano katika wizara za kilimo yaani Sudani na Tanzania.


Ndugu wanajamvi naomba tuelimishane zaidi katika haya.

1.Ni kitu gani kilisababisha Tanzania kuondoa balozi wake mwaka 1985 mjini Khartoum??

2.Tulinufaika vipi katika uhusiano huu??

3.Tutanufaika vipi kwa kufungua mara nyingine Ubalozi huu,Zingatia:-
  • Kiuchumi
  • Kisiasa
  • Kielimu na
  • kiteknolojia.
 
nikija kuwa mkubwa nataka nikaishi Khartoum so ni vzuri wafungue ubalozi.
sasa kama Tanzania ina ubalozi Afrika ya Kati, Gabon na Chad si bora na Sudan waweke maana yote ni sawa tu.
 
Labda tumuulize mkuu General omar bashir Rais Wa Sudan anaweza fafanua sababu husika ,ila ninachojua kwa maendeleo yaliyopo Khartoum Sudan kwa sasa , mzizima (dar) itasubiri sana.
 
Hii thread ni ya kipuuzi na kijinga.Kuna tatizo gani kuwa na ubalozi Khartoum ?Au ndiyo yaleyale
 
Tatizo Hapo sielewi, Kwa nini Ushangae, Nadhani ungeleta hasara wewe kwanza.
Mfano Sudan Kusin, Kuna Bus Lilikuwa Linatoka DSM hadi Juba kupitia kampala.
Hapo kuna business nzuri tu kule sema walilianzisha tena amani Imewekwa mfukoni.

Sidhani kama kuna Ubalozi au Mahusiani ambayo Hayana faida. Hao jamaa Linaweza kuwa soko zuri tu la bidhaa za ndani kwetu mipango ikiwekwa sawa. na mambo mengine mengi kutegemea na Usharp wa Balozi na watu wa Economic Deplomacy
 
Back
Top Bottom