Serikali ya Tanzania yaondoa raia wake nchini Sudan, watumia mabasi raia wa nchi nyingine walisaidiwa na mabasi hayo pia

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,033
Kwa muda sasa mji Mkuu wa Sudan, Kahrtoum umegeuka uwanja wa vita ukishuhudi mapigano makali ya kati ya jeshi la nchi hiyo na wanamgambo nchini humo ambapo miundombinu imeharibiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Mshike mshike wa nchi mbalimbali kuwaondoa raia wake nchini Sudan unaendelea huku nchi za Ulaya zikiwa zinatuma ndege za kijeshi na helikopta kuondoa raia wake na kuwapeleka maeneo salama na taarifa zinazoripotiwa zinaeleza kuwa Maelfu ya watu wameshaondoshwa hadi sasa.

Ikiwa nchi za Magharibi zinaondoa raia wake kwa uharaka, hali ya raia wa mataifa mengi ya Afrika, bado inasuasua, kuna idadi ndogo hasa wale wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao wameondolewa. Wengi bado wamekwama wakisubiria hatima ya ahadi wanazo pewa na serikali zao.

Hali ikiwa hivyo, Wananchi wa Tanzania hasa wanafunzi walioko nchini Sudan kwao hali ni tofauti kwani kwa jitihada za Serikali Tanzania imekusanya si tu Watanzania bali wanafunzi wa mataifa mbalimbali kwenye msafara wenye jumla ya mabasi matano na kuwaondoa katika uwanja wa vita Khartoum.

Raia mmoja wa Sierra Leone ambaye yupo Khartoum ameiambia BBC kuwa "anashukuru sana" kwa juhudi ambazo ubalozi wa Tanzania umefanya kuwahamisha wanafunzi wa mataifa yote kutoka Sudan wakati ambao nchi hiyo ikiwa kwenye ghasia zaidi.

Balozi wa Tanzania, Silima Kombo Haji, alisema nchi yake inajaribu kuwasaidia raia wengine wa Afrika, na si Watanzania pekee;

Katika nyakati ngumu, katika nyakati ambazo Afrika inaihitaji Tanzania, Tanzania imesimama tena na kuwashika mkono kama ilivyokuwa enzi za kumng'oa mkoloni.

KONGOLE SERIKALI YA TANZANIA
KONGOLE RAIS SAMIA SULUHU
KONGOLE WIZARA YA MAMBO YA NJE
 
Balozi apewe wizara ya mambo ya nje ili aendeleze spirit ya kusaidia wananchi nje kupitia Balozi zote
 
Back
Top Bottom