Je, Kuna Apps zenye "virus" kwenye Play Store !?

JAYJAY

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2008
Posts
9,071
Reaction score
9,674
Mimi si fundi simu ila najitahidi tahidi kuwasaidia jamaa zangu wa karibu kwenye changamoto kadhaa za simu.

Hivi karibuni nimepata kama kesi nne za simu inakuwa kama "imetekwa" baada ya application moja ya ku_download games kuwa installed. Kinachotokea baada ya ku_install hiyo application inakuwa kila application unayotaka kuitumia inakupeleka kwenye link fulani. Yaani huwezi kupiga simu, meseji na application nyingine zote zinakupeleka kwenye link. Kila mwenye simu anadai ugonjwa ulianza baada ya ku_install hiyo game downloader app.

Ila nikitumia shortcut ya kuingia kwenye "apps manager" na kui_unstall hiyo app, simu inarudi kuwa sawa. Brand za simu husika ni Samsung na tecno. Na kwenye app manger zote zinaoneaha kuwa hoyo app imepatikana kutoka app store ya google.

Sasa hapa shida ni nini!? Au hiyo app iko na faults!? Au ni tatizo la simu zenyewe!? Inawezekana play store wakawa na app zenye faults!?
 
Sio rahisi, watu wanainstall apk za ku download ambazo ziko modified na malware. Zishawahi kutokea play store ila Google wakizitambua wanazifuta hadi kwenye simu.
 
Sio rahisi, watu wanainstall apk za ku download ambazo ziko modified na malware. Zishawahi kutokea play store ila Google wakizitambua wanazifuta hadi kwenye simu.
Lakini hiyo app inaonesha source yake ni play store. Ku_install kwa apk ni ngumu kwa asiye na uzoefu wa kuichezea simu. Bahati mbaya sikumbuki jina la hiyo app. Ila kila aliyepata shida aliniambia vivyo hivyo.
 
Hiyo ni game downloader au video downloader, na hapo simu inasumbuliwa na hayo matangazo, hata ukitaka kwenda sehemu nyingine ya simu kama settings, apps zingine nk ukitouch tu inakupeleka huko.

Nenda sehemu ya apps mpya ambazo zimeongezeka katika simu, uninstall hizo app na simu itakuwa salama. Majuzi nimetoka kesi hiyo ya Muha mmoja hivi kutoka Kasulu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…