Je, kinga ya Rais inamzuia kuhojiwa kwa mambo aliyoyafanya akiwa waziri?

cacacuona

JF-Expert Member
Feb 24, 2017
655
776
Wajuzi wa mambo na waliosoma katiba vizur naomba ufafanuzi kwa jambo hili.Maana naona tunachanganywa.huyu anasema hivi yule anasema vile.Nimemanisha kwamba ikitokea raisi ambaye alishawahi kuwa waziri.na alifanya madudu wakati akiwa waziri.je sheria na katiba inasemaje kuhusu kinga yake?.anaweza kushitakiwa na kuhojiwa au hawezi kuhojiwa.?
 
MKUU MAMBO MENGINE SIO YA KUULIZA WATU VIJIWENI,FUNGUA KATIBA ISOME VEMA NINA IMANI UTAPATA JIBU MUBASHARA
 
Wajuzi wa mambo na waliosoma katiba vizur naomba ufafanuzi kwa jambo hili.Maana naona tunachanganywa.huyu anasema hivi yule anasema vile.Nimemanisha kwamba ikitokea raisi ambaye alishawahi kuwa waziri.na alifanya madudu wakati akiwa waziri.je sheria na katiba inasemaje kuhusu kinga yake?.anaweza kushitakiwa na kuhojiwa au hawezi kuhojiwa.?
Kama alitenda Uovu akiwa waziri yaani Dhambi zake kabla ya kuwa Rais zipo pale pale katiba haina kinga juu ya hilo lazima ashitakiwe tu, magufuli atalemewa na mizigo ya kubeba kambeba Daud Bashite, Mrisho gambo na rambirambi sasa ameamua kuwabeba kikwete na mkapa
 
Je hivi kinga ya raisi haiwezi kuondolewa na yeye akashitakiwa?
 
Wajuzi wa mambo na waliosoma katiba vizur naomba ufafanuzi kwa jambo hili.Maana naona tunachanganywa.huyu anasema hivi yule anasema vile.Nimemanisha kwamba ikitokea raisi ambaye alishawahi kuwa waziri.na alifanya madudu wakati akiwa waziri.je sheria na katiba inasemaje kuhusu kinga yake?.anaweza kushitakiwa na kuhojiwa au hawezi kuhojiwa.?

Kimsingi, kinga ni kwa ajili ya kushitakiwa, sio kuhojiwa. Lakini pia, Bunge linaweza kutoa azimio ahojiwe. Hilo haliwezi kuwa uamuzi na Mwendesha Mashataka Mkuu wa serikali.

Na pia niseme wazi kwamba ni makosa makubwa kwa Raisi Magufuli kutoa tamko kwamba maraisi wastaafu wasibughudhiwe. Hii si sawa. Tunaelewa kwamba kutokana na sheria iliyopo hatuwezi kuwashitaki, lakini haina maana kukiwa na ushahidi ulio wazi kwamba walifanya ufisadi hatupaswi kuongelea jambo hilo.

Waziri wa Sheria yeye ameliweka vema, kwamba pamoja na kuwa na ukweli kuwa walihusika na ufisadi, kwa heshima yao hatuwezi kuwataja katika taarifa za tume. Lakini hatupaswi kusema kwamba vyombo huru vya habari vizuiwe kuwataja au kuongelea ufisadi wao.

In fact, ni vema kama hatuwezi kuwashitaki, basi tuwataje hadharani (name and shame). Kama wao wataona wameonewa basi waende mahakamani kushitaki kukashifiwa ili wawe wamefungulia wenyewe njia ya kuweka mambo yote wazi.
 
Wajuzi wa mambo na waliosoma katiba vizur naomba ufafanuzi kwa jambo hili.Maana naona tunachanganywa.huyu anasema hivi yule anasema vile.Nimemanisha kwamba ikitokea raisi ambaye alishawahi kuwa waziri.na alifanya madudu wakati akiwa waziri.je sheria na katiba inasemaje kuhusu kinga yake?.anaweza kushitakiwa na kuhojiwa au hawezi kuhojiwa.?

Hivi kwanini. Mnapenda sana kuangalia half empty badala ya half full .watu kama nyinyi will never be Happy in life.
 
Kama alitenda Uovu akiwa waziri yaani Dhambi zake kabla ya kuwa Rais zipo pale pale katiba haina kinga juu ya hilo lazima ashitakiwe tu, magufuli atalemewa na mizigo ya kubeba kambeba Daud Bashite, Mrisho gambo na rambirambi sasa ameamua kuwabeba kikwete na mkapa
Lakn mkuu sijauliza kwa lengo la kumkosoa mkulu..
 
Hivi kwanini. Mnapenda sana kuangalia half empty badala ya half full .watu kama nyinyi will never be Happy in life.
Sijakuelewa.sitakuwa na furaha katika maisha yangu kivipi? Kushitakiwa au kutoshitakiwa kwa raisi kunapunguza au kuongeza vp furaha yangu.Lumumba wamekutuma waambie wamekutuma kwa mtu asie sahihi..sishabikii uchama.ninachohitaji kuelewa huu ukakasi basi..
 
Wajuzi wa mambo na waliosoma katiba vizur naomba ufafanuzi kwa jambo hili.Maana naona tunachanganywa.huyu anasema hivi yule anasema vile.Nimemanisha kwamba ikitokea raisi ambaye alishawahi kuwa waziri.na alifanya madudu wakati akiwa waziri.je sheria na katiba inasemaje kuhusu kinga yake?.anaweza kushitakiwa na kuhojiwa au hawezi kuhojiwa.?
Mkuu Kaka Kuona, tenganisha vitu viwili, kitu kinachoitwa cheo, na kitu kinachoitwa mtu!.

Cheo ni nafasi ya kazi aliyoshika, yaa position ya uwaziri, urais. Hizi positions ni institutions, uwaziri ni institution na urais ni institution, mtu anayeshika nafasi hizo ni mtu kwa uwaziri anaitwa waziri, na kwa urais anaitwa rais. Sasa uwaziri unashitakika na urais pia unashitakika!. Kinga haitolewi kwa institution, bali inatolewa kwa Mtu aliyeshika urais!.

Sasa ikitokea mtu aliyekuwa waziri na akafanya madudu kibao kwenye uwaziri wake, kisha mtu huyo akaja kuwa rais, ile kinga inamhusu direct kwa sababu kinga ni ya mtu!.

Mfano kwenye issue ya IPTL namfahamu aliyekuwa Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini, Patrick Rutabanzibwa alipewa zawadi fulani ya x-mass na mtu fulani, akaikataa, akairudisha, kisha namjua waziri wake alikuwa nani, na rais alikuwa nani, nao wote walizawadiwa, wakapokea!, taarifa ilipofika kuwa Rutabanzibwa karudisha zawadi, huku wakuu wamepokea, ikaamuliwa Rutabanzibwa aondolewa IPTL ikapitishwa!. Sasa katika kuifukua issue ya IPTL kuna watu hawahojiki!.

Hata ikitokea mbunge yoyote kulalamikia uuzwaji wa nyumba za serikali, samaki wa Magufuli, kivuko cha MV Kigamboni, then hiki kitakuwa ni kilio cha samaki, machozi yatakwenda na maji!.

Rais sio tuu hawezi kushitakiwa, hawezi kuhojiwa!. Ila kwa ridhaa yake mwenyewe, anaweza kufika mahakamani kutoa ushsahidi wowote!.

Paskali
 
Mungu akipenda tutabadili katiba ya Tanzania , maana kuna watu wanalindwa hata kuliko Mungu anavyolindwa na Misahafu , inawezekana tu .
 
Back
Top Bottom