SI KWELI Je, Kenya wana Nuclear power station?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
 
Tunachokijua
Madai

Mtumiaji mmoja wa X amechapisha picha inayoonekana kuwa ni ya kituo cha Nishati ya nyukilia huko Mombasa na kuuliza kwanini Tanzania hatuna kituo kama hicho. Tazama hapa na hapa

Uhalisia wa madai hayo

Jamiicheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa picha hiyo si halisi na hakuna kituo cha nishati ya nyukilia nchini Kenya.

Ufuatiliaji umebaini kuwa Barani Afrika kuna kituo kimoja tu cha Nishati ya Nyukilia ambacho kiitwacho Koeberg Nuclear power station kilichopo Cape Town, Afrika Kusini.

Mataifa mengine yaliyopanga kuwa na vituo hivyo ni Misri, Afrika kusini (kituo cha pili), Ghana, Uganda, Morocco, Kenya, Algeria, Tunisia.

Hivyo hadi kufikia sasa hakuna kituo chochote cha Nyuklia kilichojengwa nchini Kenya ingawa wana mpango wa kuanza ujenzi wa kituo hicho.

Ufuatiliaji kwa kutumia nyenzo ya kidigitali ya kubaini maudhui yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya Akili Unde imedhihirisha kuwa picha hiyo imetengenezwa kwa AI kwa zaidi ya 99%.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…