Je, kauli ya Mwenezi Makonda kwamba Watu wasitenganishe mafanikio ya Rais Samia na Magufuli inalenga Kulinda Legacy?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,128
49,849
Bwana Mwenezi Ametoa Kauli ya kushangaza sana ambayo kiufupi Haina maana.

Anatakiwa kuelewa kwamba ulinganisho ndio huleta Kipimo Cha ufanisi.

Kwa muda mrefu Magufuli amekuwa akichukuliwa kama benchline ya Kulinganisha Uongozi lakini Sasa hivi baada ya kuona Dalili za benchmark hii kuhama,Mwenezi ambae amejitanabaisha kwamba hawezi mkana Magufuli Kwa sababu ni role model wake anaonekana kukasirika hasa na takwimu zinazoonesha Ligacy inafunikwa.

Ukweli mchungu ambao bwana Makonda anatakiwa kuukubali ni kwamba Samia amewashangaza wengi ambao walitarajia ashindwe wapate visingizio vya 2025 Sasa imekuwa kinyume chake.

Je, ni Uongozi kwamba alikuta bwawa la Nyerere liko 30% na Sasa limekamilika?

Je, ni uongo kwamba 70% ya Sgr imejengwa awamu ya 6 na soon treni kutoka Dar-Dom inaenda kufanya kazi?

Je, ni uongo kwamba Samia ameleta mapinduzi sekta ya Afya?

Je, ni Uongozi kwamba Samia ameleta Mageuzi makubwa sekta ya Kilimo

Je, ni Uongo kwamba Kwa miaka 3 ya Samia TRA imepata mafanikio makubwa bila maguvu?

Je ni uongo kwamba Wapinzani wako huru kuongea vikiwemo vyombo vya habari vilivyofungiwa?

Je ni Uongo kwamba Samia amerejesha maelfu ya Ajira ?

My Take
Legacy hailindwi Bali inajilinda.Kwa hiyo bwana Mwenezi aache Kila anachokiita unafiki Kwa sababu haitakaa itokeee na haiwezekani Samia afanane na Magufuli.
 
Hapa ndio wanajichanganya zaidi. Kwani hao viongozi wanatekeleza mawazo yao au ilani ya chama!!??

Labda uniambie kwenye usimamizi wa utekeleza wa ilani ya chama na fedha Magufuli anaongoza
 
Nani angeshidwa peleka maji mwanza yani maji yapo nnje ushidwe kuingiza ndani kweliii??
Waliotangulia a
Walishindwa.Maji hayaendi Mwanza tuu Bali yanaenda Kila Kijiji na Kila Mji.

Samia ame double hiyo budget twice with no visingizio vya Sgr na bwawa or Mabeberu.
 
Waliotangulia a
Walishindwa.Maji hayaendi Mwanza tuu Bali yanaenda Kila Kijiji na Kila Mji.

Samia ame double hiyo budget twice with no visingizio vya Sgr na bwawa or Mabeberu.
Kwamba Dar inayo maji ya kutosha una uhakika kwamba mwaza vijiji vyote vimepata maji au mnadanganya watu wasio na hatia.
 
Bora ungeandika tu kiswahili kuliko kufuata mkumbo, chawa mna nini nyie? Haya LIGACY ni neno kutoka lugha gani?
 
Kwamba Dar inayo maji ya kutosha una uhakika kwamba mwaza vijiji vyote vimepata maji au mnadanganya watu wasio na hatia.
Kwa hiyo unatarajia ndani ya miaka 3 Kila Kijiji Kila mtaa uwe na maji wakati mlishindwa Kwa miaka 60 ya Mwanzo?

Lengo la Samia ni 95% vs 85% by 2025 kuwe na maji ya Bomba Kila maeneo.

Kule ambako Bomba litakuwa bado watachimba visima ndio maana amenunua mtambo wa kuchimba Kila Mkoa.

Nani mwingine amewahi kufanya hayo?
 
Samia kawashangaza wengi Kwa lipi,????.

Embu nisaidie
Soma hapa 👇
20240326_154430.jpg
20240326_154435.jpg
20240325_140420.jpg
20240324_091838.jpg
20240324_091840.jpg
20240321_201348.jpg
20240319_183136.jpg
20240321_201240.jpg
20240319_140904.jpg
20240319_102022.jpg
20240319_101511.jpg
 
Kwa hiyo unatarajia ndani ya miaka 3 Kila Kijiji Kila mtaa uwe na maji wakati mlishindwa Kwa miaka 60 ya Mwanzo?

Lengo la Samia ni 95% vs 85% by 2025 kuwe na maji ya Bomba Kila maeneo.

Kule ambako Bomba litakuwa bado watachimba visima ndio maana amenunua mtambo wa kuchimba Kila Mkoa.

Nani mwingine amewahi kufanya hayo?
Nani ameshidwa?
 
Back
Top Bottom