Je, jamii inatumia jukwaa gani kumshauri Rais?

MASSANDA OMTIMA

Senior Member
Mar 22, 2017
159
47
Siku chache zilizopita, pale Chuo Kikuu cha Kivukoni, kulikuwa na mdahalo. Katika mdahalo ule, Rais Mtaafu Benjamini W. Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph S. Warioba walisikika, kwa nyakati tofauti, wakisema, "KIONGOZI MZURI NI YULE ANAYESIKILIZA USHAURI"

Ninachojiuliza, ni kwamba, jamii inatumia jukwaa gani katika kuwasilisha ushauri wao kwa Rais? Wabunge wanaweza kutumia Bunge; Mawaziri hutumia vikao (ingawa sijui ratiba ya vikao vyao ikoje na kama kweli vipo inakuwaje wakati mwingine wanatoa majibu tofauti kwa maswali ya aina moja - ingawa sina reference lakini hilo linajulikana); timu ya washauri wa nyanja mbalimbali hukutana Ikulu, n.k.

Endapo hakuna jukwaa la namna hiyo, nashauri Rais ateue mtu/watu pale Ikulu wa kufuatilia mitandao ya kijamii ili kukusanya maoni ya jamii (constructive ideas) kutoka kwenye mitandao hii na kuiwasilisha kwake na kuwa na wafuatiliaji wa utekelezaji wa maoni hayo. Na kama itakuwa hivyo, nadhani hata utoaji maoni kwenye mitandao hii utakuwa na aina Fulani ya nidhamu yenye kuonyesha dhamira ya dhati (seriousness) ndani yake ili kuleta tija.
 
Kumshauri ili iweje?? HASHAURIWI WALA HAPANGIWI,
 
Nakushauri mtoa mada uwe unafuatilia hotuba za rais wetu. Utaweza kugundua tu kirahisi kwamba mitandao ya kijamii huwa anaifuatilia sana tu.
 
Back
Top Bottom