Israel na Wayahudi kwa ujumla, ndiyo Taifa lililopigana vita vingi kuliko taifa lolote Duniani, na baadhi ya wachambuzi wanaitaja IDF kama ndilo jeshi bora kabisa Duniani.
Lakini hata hivyo, kwenye vita hata ukiwa bora kiasi gani, unaweza kukutana na matokeo tofauti kabisa na ulivyotarajia:
Marekani iilikutana na matokeo tofauti sana ilipopigana na Vietnam.
Halikadhalika, China ilitandikwa na Vietnam, tofauti kabisa na matarajio yake.
Huko Ukraine, Urusi imekutana na hali tofauti mno na ilivyotegemea. Kutoka siku 3 ambazo ilidhani itakuwa imelitiisha adabu jeshi la Ukraine, sasa ni mwaka wa 3.
Lakini pia Iran, kwa kiburi chake, nakuendelra kutengeneza na kuyategemeza makundi ya kigaidi inaweza kupata matokeo tofauti sana, ikiwa ni pamoja na kipigo toka kwa Israel na majirani zake wanaoichukia Iran kutokana na kupandikiza makundi ya kigaidi katika mataifa yao.