Je Israel itaishambulia Iran?

Je Israel itaishambulia Iran?

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
18,379
Reaction score
26,923
Netanyahu amesema kama mazungumzo ya US na Iran yatashindikana juu ya Iran kuachana na urutubishaji wa mabomu ya nyuklia basi Israeli itashambulia vinu vya nyuklia vya Iran upesi iwezekanavyo.

Ayatollah Khomenei kasema hawezi kukubaliana na hoja za Marekani za kuachana na utengenezaji wa zana za nyuklia kwa ahadi ambazo anaona zina uongo ndani yake. Hivyo kwa yeye binafsi anasema mazungumzo hayo hayana tija. Mazungumzo bado yanaendelea kati ya wajumbe wa serikali ya Iran na wa Marekani.

Hivyo kwa akili ya Netanyahu na alivyo na misimamo na ahadi za kweli bilashaka atashambulia vinu vya nyuklia vya Iran na kuidumbuliza mashariki ya kati katika vita kubwa. Maana Iran pia imetishia kulipiza kwa uzito kama Israeli itafanya hivyo. Na imesema itashambulia ngome zote za Marekani za kijeshi kwa mashariki ya kati.

Trump hapendi vita bali mazungumzo hasa yanayohusisha shekeli, ni mfanya biashara ila Nyahu ni lord of war. Sasa tutaona itakavyokuwa ila tusiombee hayo kwa sasa maana hata sisi tutaathirika.

Mchambuzi wa Siasa,dini na historia

Mwanazuoni wa kujitegemea
 
Hivyo ni vitisho tu. Kuendesha vita tatu kwa wakati mmoja sio rahisi hasa kwa nchi ndogo kama Israel. Japo wanategemea msaada wa marekani kumbuka mtegemea cha nduguye hufa masikini. Ukraine kiko wap?
 
Hivyo ni vitisho tu. Kuendesha vita tatu kwa wakati mmoja sio rahisi hasa kwa nchi ndogo kama Israel. Japo wanategemea msaada wa marekani kumbuka mtegemea cha nduguye hufa masikini. Ukraine kiko wap?
Israel ingekuwa nchi ndogo isingegawa kichapo kwa nchi nne za kiarabu kwenye ile vita maaana kipindi kile alisimama mwenyewe hapakuwepo huyo mmarekani hata sasa anawafinya tu tatizo kobazi mmewekeza kwenye madufu mnategemea nini
 
Netanyahu amesema kama mazungumzo ya US na Iran yatashindikana juu ya Iran kuachana na urutubishaji wa mabomu ya nyuklia basi Israeli itashambulia vinu vya nyuklia vya Iran upesi iwezekanavyo.

Ayatollah Khomenei kasema hawezi kukubaliana na hoja za Marekani za kuachana na utengenezaji wa zana za nyuklia kwa ahadi ambazo anaona zina uongo ndani yake. Hivyo kwa yeye binafsi anasema mazungumzo hayo hayana tija. Mazungumzo bado yanaendelea kati ya wajumbe wa serikali ya Iran na wa Marekani.

Hivyo kwa akili ya Netanyahu na alivyo na misimamo na ahadi za kweli bilashaka atashambulia vinu vya nyuklia vya Iran na kuidumbuliza mashariki ya kati katika vita kubwa. Maana Iran pia imetishia kulipiza kwa uzito kama Israeli itafanya hivyo. Na imesema itashambulia ngome zote za Marekani za kijeshi kwa mashariki ya kati.

Trump hapendi vita bali mazungumzo hasa yanayohusisha shekeli, ni mfanya biashara ila Nyahu ni lord of war. Sasa tutaona itakavyokuwa ila tusiombee hayo kwa sasa maana hata sisi tutaathirika.

Mchambuzi wa Siasa,dini na historia

Mwanazuoni wa kujitegemea
Ila mheshimiwa mchambuzi mbona umebadiri kabisa maudhui ya hii mada, urutubishaji wa nini ya Nyuklia si vema kupotosha kwa kujua au kutojua.

Ni urutubishaji wa nishati au madini ya uranium na sio Mabomu ya Nyuklia.
Eti my friend unawezaje kurutubisha mabomu ya Nyuklia ili kitokee nini?

Iran inarutubisha madini ya uranium na sio mabomu, Iran bado hajaweza kutengeneza bomu la Nyuklia ila uranium inayorutubishwa nchini humo inakaribia kufikia kiwango ambacho kinaweza kutumika kutengeneza bomu la nyuklia.

Iran daima imekuwa ikisema Dini yao Shia hawaamini katika kutengeneza bomu la nyuklia, kama wangekuwa wanataka wanasema wangekuwa nalo siku nyingi.

Jambo la pili ambalo ungepaswa uelewe ni kuwa endapo Iran ingekuwa na hata bomu 1 tuu la nyuklia ina maana Hadithi ya vitisho kutoka Israel ingeishia hapo. Maana nchi yeyote ikishakuwa na bomu hata moja tuu la nyuklia basi haigusiki tena. Teknolojia ya makombola yenye uwezo wa kubeba mabomu hayo Iran tayari wanayo na yanaweza kufika Israel kama tulivyoona mwaka jana.

Mambo yalikuwa matatu la kwanza ilikuwa kuizuia isiweze kurutubisha uraniam kuzidi asilimia 3 maana ili uranium iwezeze kutumika kutengeneza bomu ninlazima ifikie asilimia 12(sikumbuki vizuri).

Uranium inayorutubishwa nchini Iran ni kwaajili ya umeme na vinu hivyo alijengewa na Urusi.
Hivyo wao baada ya migogoro mikubwa na Israel na Marekani na kuwekewa maelfu ya vikwazo waakamua kupambana kiteknolojia na kufaulu kujenga vinu vyao vingine vya utafiti chini ya ardhi, na miaka ya karibuni wanasema wao wenyewe wamefanikiwa kurutubisha uranium hadi kufikia 9 percent na Ayatollah akasema kuwa kama wangekuwa na interest na bomu la nyuklia basi wangeweza kurutubisha kufikia asilimia 12 maana wanadai huo uwezo wa kurutubisha kufikia hizo percent kwa sasa wanao(no any proof).

Marekani ilipambana sana kwa kuisaidia Israel kuhakikisha kuwa Iran haipati technolojia ya Balistic missile yaani makombola ya masafa marefu lakini kwa maajabu Iran imepamba leo inayo tena sio ballistic tuu na cruise missile na sio super sonic tuu wanadai hata hypersonic kumbuka mwaka jana lile shambulio lao la mwisho kwa Israel ambalo walishindwa ku intercept kwa kutumia technolojia zote za magharibi.

Sasa Israel amechanganyikiwa kabisa kwa sababu asipoangamiza vinu vya Nyuklia vya Iran haraka iwezekanavyo what if one morning tunaamka tunasikia Iran anatangaza kuwa amefanya jaribio la bomu la nyuklia chini ya Ardhi, hiyo siku ndiyo nightmare inayoisumbua Israel halali hata siku moja.

Maana wanaona kwa miaka karibu 40 ya kuidhibiti iran kila kona bado imefanikiwa kufikia malengo yote ambayo wao hawakutaka kabisa ayafikie.
Ndio maana ilibidi waisambaratishe kwanza Gaza yote, Lebanon, Syria na Sasa Yemen ili kuondoa au kutengeneza njia rahisi ya kumpiga Iran bila kupata resistance kubwa ya ndani au karibu yao.

Tumaini kubwa pekee wanalolitegemea ni Trump tu maana yupo upande wao, anawaunga mkono zaidi kwa maneno but no action. Hili linawachukiza sana Israel. Wanajua Trump akimaliza muda wake tuu kwisha habari yao wakiingia Democrat's hawata sapoti suala kuishambulia Iran.

Trump anaogopa sana hajui nini kitatokea endapo wakiishambulia Iran hasa kwa sababu ya Mrusi je hataingilia na juzi juzi tunaona walivyokuwa karibu na kusainishana mikataba mingi ya kiusalama kati ya Iran na Urusi..
Tatu kumbuka Russia anapakana na Irani kwa upande wa kusini kupitia bahari ya Caspian na for future kwa kuwa Russian ni kama land locked kwa sababu ili afike kwokwote kwa maji ni lazima apite pale kwa mturuki ambaye ni member wa nato na ni mnafiki hatabiri.

Hivyo kuna mipango ya kujenga reli kutoka urusi mpaka bahari ya ghuba ya uajemi Iran(India ocean) pia wanataka wachimbe mfereji mrefu kuliko yote Duniani yaani kutokea Caspian sea hadi ghuba ya uajemi yaani iran katika bahari ya hindi.

Kikwazo kikubwa kwa mradi huo ni giografia yake ni ngumu ngumu sana kuna milima ya kufa mtu mabonde miamba kimsingi ni ngumu sana. Pili ni bajeti hawana maana inahitaji billions of billions changanya hali ya uchumi wa Urusi ilivyo tete kwa vikwazo.
Hivyo future ya Urusi kwa Iran ni kubwa mno kuliko kwa Israel kwa sababu za kiuchumi ni kiusalama, maana ikitokea lolote halafu nato wakablock ili njia ya Uturuki urusi itakuwa kama Rwanda tuu. Ndio maana wanapambana kutafuta alternative ya kudumu kwa miaka mingi ijayo.
 
Hivyo ni vitisho tu. Kuendesha vita tatu kwa wakati mmoja sio rahisi hasa kwa nchi ndogo kama Israel. Japo wanategemea msaada wa marekani kumbuka mtegemea cha nduguye hufa masikini. Ukraine kiko wap?
Hiv wewe kwa akili yako kati ya marekan na Israel nani anamtawala mwenzie.
 
Hivyo ni vitisho tu. Kuendesha vita tatu kwa wakati mmoja sio rahisi hasa kwa nchi ndogo kama Israel. Japo wanategemea msaada wa marekani kumbuka mtegemea cha nduguye hufa masikini. Ukraine kiko wap?
Israel sio nchi ndogo Kwa kichapo inachotoa Kwa magaidi mpaka waarabu wote wa mashariki ya kati mnahimizwa kumchangia Israel kwenye vita
 
Mimi sio kobazi. Israeli ni ndogo kijografia ila ina jeshi dogo imara lenyel ujuzi na uzoefu wa kivita. Wasi wasi wangu ni kwamba kama mashambulizi yatatoka Yemen na iran huku Hezbollah itakuwaje? Ataweza kuhimili vishindo?
Hezbollah imekula kichapo imezohofika Haina hata kiongozi
 
Ngoja nimzoom Ayatollah
1000438248.jpg
 
Netanyahu amesema kama mazungumzo ya US na Iran yatashindikana juu ya Iran kuachana na urutubishaji wa mabomu ya nyuklia basi Israeli itashambulia vinu vya nyuklia vya Iran upesi iwezekanavyo.

Ayatollah Khomenei kasema hawezi kukubaliana na hoja za Marekani za kuachana na utengenezaji wa zana za nyuklia kwa ahadi ambazo anaona zina uongo ndani yake. Hivyo kwa yeye binafsi anasema mazungumzo hayo hayana tija. Mazungumzo bado yanaendelea kati ya wajumbe wa serikali ya Iran na wa Marekani.

Hivyo kwa akili ya Netanyahu na alivyo na misimamo na ahadi za kweli bilashaka atashambulia vinu vya nyuklia vya Iran na kuidumbuliza mashariki ya kati katika vita kubwa. Maana Iran pia imetishia kulipiza kwa uzito kama Israeli itafanya hivyo. Na imesema itashambulia ngome zote za Marekani za kijeshi kwa mashariki ya kati.

Trump hapendi vita bali mazungumzo hasa yanayohusisha shekeli, ni mfanya biashara ila Nyahu ni lord of war. Sasa tutaona itakavyokuwa ila tusiombee hayo kwa sasa maana hata sisi tutaathirika.

Mchambuzi wa Siasa,dini na historia

Mwanazuoni wa kujitegemea
IRAN uwa anapiga kambi za kaka ake Israel 🇮🇱 USA alifanya ivyo kipindi kamanda mkuu aliyefyekwa na Marekani alafu anatokea mtu anaichukulia poa IRAN
 
Mwambieni Israel awache comedy kadundwa mala2 na akunakitu kafanya zaid ya mapicha picha ya kihindi na propaganda!!!!

awache kelele mambo ya Nuclear ndio ajipeleke geto kwa Iran!!!!!

General wa Iran alisema Israel aijawai kuwa na uwezo wala nia ya kuishambulia Iran!!! 1)

akaongeza 2) nawala awakuwai kuwa na uwo uwezo uko nyuma kabla yake!!

3) wala miaka ijayo bado Israel atokuwa na uwezo wa kuishambulia Iran !!

Sasa Netanyahu akishiba magimbi ndio anawafuraisha walokole wa kijiji cha mwenda mbioo!!!
 
Mimi sio kobazi. Israeli ni ndogo kijografia ila ina jeshi dogo imara lenyel ujuzi na uzoefu wa kivita. Wasi wasi wangu ni kwamba kama mashambulizi yatatoka Yemen na iran huku Hezbollah itakuwaje? Ataweza kuhimili vishindo?
Israel na Wayahudi kwa ujumla, ndiyo Taifa lililopigana vita vingi kuliko taifa lolote Duniani, na baadhi ya wachambuzi wanaitaja IDF kama ndilo jeshi bora kabisa Duniani.

Lakini hata hivyo, kwenye vita hata ukiwa bora kiasi gani, unaweza kukutana na matokeo tofauti kabisa na ulivyotarajia:

Marekani iilikutana na matokeo tofauti sana ilipopigana na Vietnam.

Halikadhalika, China ilitandikwa na Vietnam, tofauti kabisa na matarajio yake.

Huko Ukraine, Urusi imekutana na hali tofauti mno na ilivyotegemea. Kutoka siku 3 ambazo ilidhani itakuwa imelitiisha adabu jeshi la Ukraine, sasa ni mwaka wa 3.

Lakini pia Iran, kwa kiburi chake, nakuendelra kutengeneza na kuyategemeza makundi ya kigaidi inaweza kupata matokeo tofauti sana, ikiwa ni pamoja na kipigo toka kwa Israel na majirani zake wanaoichukia Iran kutokana na kupandikiza makundi ya kigaidi katika mataifa yao.
 
Israel haijawahi kuanzisha vita na haijawahi kushindwa vita.!!

Toka Oct 07,2023 Magaidi wa Hamas,Hezbollah,Houth,waasi wa Syria na Iraq,Magaidi wa kutoka West-Bank na Baba yao Iran wote hao walikuwa wakiishambulia Israel lakini ilianza kuwabutua mmoja baada ya mwingine wakianza na Magaidi wa Hamas,Waasi wa Syria,Iraq na Hezboullah hadi sasa hivi Magaidi hao hawana hamu na Majeshi ya Israel na wamepoteza viongozi wao karibu wote akiwemo Hassan Nasrallah.

Mbele ya majeshi shupavu ya Israel magaidi wote watanyooshwa tu wala hawawezi kuwa tishio lolote!!
 
Attachments

  • IMG_1124.jpeg
    IMG_1124.jpeg
    110.1 KB · Views: 17
Back
Top Bottom