Je, Israel Imezuia Vita vya Nyuklia au Kuianzisha?"

Je, Israel Imezuia Vita vya Nyuklia au Kuianzisha?"

its MalekoGJ

Senior Member
Joined
Aug 27, 2020
Posts
135
Reaction score
285
ISRAEL NA IRAN 2025

KUCHOKOZA FUKUTO LA VITA KUBWA ZAIDI MASHARIKI YA KATI


Je, Israel Imezuia Vita vya Nyuklia au Kuianzisha?"


Na

MALEKOGJ
Katika saa za giza alfajiri ya Ijumaa, jeshi la anga la Israel lilianzisha kile kinachoitwa Operation Rising Lion shambulizi la anga kubwa zaidi kuwahi kufanywa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tangu kumalizika kwa Vita vya Iran na Iraq mwaka 1988. Lakini tofauti na mapambano ya kijeshi yaliyopita, safari hii Israel haikulenga tu mitambo ya nyuklia ya Iran, bali ilipenya hadi ndani kabisa ya mtandao wa uongozi wa kijeshi na kisayansi wa taifa hilo, na kusababisha tetemeko la kijiografia, kisiasa, na kiusalama.
Taarifa za awali zinasema kuwa zaidi ya watu 78 wameuawa, wakiwemo watoto na raia wa kawaida, huku zaidi ya 300 wakijeruhiwa. Miongoni mwa waliouawa ni viongozi wakuu wa kijeshi: Maj. Jenerali Mohammad Hossein Bagheri, Kamanda Mkuu wa Majeshi; Jenerali Hossein Salami wa IRGC; Jenerali Gholam Rashid, Mkuu wa Vikosi vya Dharura; pamoja na wanasayansi sita waandamizi wa nyuklia. Kwa mara nyingine tena, Mossad – shirika la ujasusi la Israel – limeonesha uwezo wake wa kuingia ndani kabisa ya mfumo wa usalama wa Iran bila kutambulika.

Mitambo ya nyuklia kama Natanz, ambayo imekuwa kiini cha utata wa mpango wa Iran wa kurutubisha uranium, ilishambuliwa kwa makombora na drone. Katika miji ya Tabriz, Shiraz, Arak, Isfahan na Tehran, milipuko mikubwa ilisikika, huku moshi mzito ukitanda angani. Iran ilijibu kwa kutuma zaidi ya drone 100 kuelekea Israel, lakini IDF (Jeshi la Ulinzi la Israel) ilisema ziliangamizwa kabla hazijafika. Hii ilikuwa awamu ya kwanza tu ya kile ambacho wanasiasa wa Israel wanasema ni “kampeni ya muda mrefu” dhidi ya Iran.
Msemaji wa serikali ya Iran alisema wazi kuwa mashambulizi haya ni “tamko la vita,” na Ayatollah Ali Khamenei ameapa kisasi kikali. Iran pia ilijiondoa kwenye duru ya sita ya mazungumzo ya nyuklia yaliyokuwa yafanyike Oman siku ya Jumapili, na ikasema haitashiriki tena kwa “muda usiojulikana.”

Lakini kwanini sasa?
Kwa zaidi ya muongo mmoja, Israel imekuwa ikihofia kile kinachoitwa breakout capability hatua ya mwisho kabla ya taifa kutengeneza silaha ya nyuklia. Iran imeendelea kurutubisha uranium hadi kiwango cha 60%, kiwango kinachozidi kile kinachohitajika kwa matumizi ya kiraia. Kwa mujibu wa taarifa kutoka IAEA wiki hii, Iran imekiuka masharti ya mkataba wa kuzuia uenezaji wa silaha za nyuklia. Hii imewapa Israel uhalali wa kisiasa na kijeshi wa kuchukua hatua kwa upande wao.

Rais wa Marekani, Donald Trump, alidai kuwa Iran ilipewa siku 60 kufikia makubaliano mapya ya nyuklia lakini ilikataa. Trump alisema, “Walikuwa na nafasi. Sasa wanavuna walichopanda.” Lakini licha ya kauli hizo, Marekani imekana ushiriki wowote katika operesheni ya kijeshi ya Israel. Serikali ya Iran haikushawishika: ilisema huwezi kushambulia mtandao wa Iran kwa ukubwa huu bila msaada wa kijasusi na kijeshi kutoka kwa Marekani.

JIBU LA IRAN KISASI KINAANZA
Drones zaidi ya 100 zilirushwa kuelekea anga ya Israel – baadhi zikidunguliwa kabla ya kufika.
Iran imejiondoa rasmi katika mazungumzo ya Oman kuhusu mpango wa nyuklia.
Barua kwa Baraza la Usalama la UN imeelezea tukio hili kama “tamko la vita.”
Vitisho vya mashambulizi ya kimtandao na kupitia makundi ya washirika (Hezbollah, Houthis) vimeanza kutolewa.
Hata hivyo Ayatollah Ali Khamenei amesema "The Iranian armed forces will act with full force and will bring the despicable zionist entity to a state of collapse and impotence.The entity will not escape unscathed after this crime, and it will regret its actions.

Hali ya taharuki imetanda duniani. Bei ya mafuta imepaa kwa kasi, dhahabu imevunja rekodi, na mashirika ya ndege yamefuta safari za Mashariki ya Kati. Saudi Arabia, Jordan, na nchi za Ghuba licha ya kutofautiana kisiasa na Iran sasa zina hofu kuwa moto huu unaweza kuwafikia. Kwa miongo kadhaa, mataifa hayo yamejifunza kuishi na Jamhuri ya Kiislamu kama jirani. Lakini mgogoro huu unaweza kuwa mwanzo wa mbio mpya za silaha za nyuklia.

Mashambulizi haya yanaibua maswali mengi sanaa

Je, Iran itajibu kwa nguvu zaidi?

Je, Israel ina mipango ya awamu ya pili ya mashambulizi?

Je, Marekani itasukwa kuingia moja kwa moja?

Dunia iko katika kipindi cha masaa 72 hatari zaidi tangu vita vya Iraq 2003.

JE, ISRAEL IMEFANIKIWA? AU IMECHOCHEA JANGA LA MUDA MREFU?
Kwa sasa, Israel imepata mafanikio ya kijeshi kwanii
Imeua viongozi wakuu wa kijeshi na wanasayansi.
Imevuruga usambazaji wa nguvu wa Iran.
Imeonesha uwezo wake wa upenyo wa kiintelijensia.
Lakini faida ya kisiasa na kijeshi inaweza kuwa ya muda mfupi. Kumbuka Katika geopolitics, kila hatua ya kijeshi huzaa hatua ya kisiasa isiyotabirika. Sasa Iran ni taifa lililojeruhiwa na kama historia inavyotufundisha, majeruhi hujibu kwa hasira.
 
Back
Top Bottom