Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,221
- 2,425
Kwa mara ya kwanza ilitolewa mwaka 2019 imepita Miaka zaidi 6 Toka kuachiwa kwake, ni simu nzuri sana ambayo wakati inatambulishwa ilikuja ikiwa na feature Mbalimbali za kuvutia kama vile triple lens kwenye kamera, chip ya A14 Bionic nk.
Je simu hii ya iphone 11 Pro bado inafaa kununuliwa Kwa mwaka 2025 basi Leo nitakujuza mambo kadhaa kisha utachagua mwenyewe 👋.
💰 Kwenye soko la Sasa simu hizi zimeshuka sana utaweza kuzipata kwa Bei kitonga TU kuanzia 380k mpaka 490k utaweza kuipata iphone 11 Pro nzuri TU wakati inatoka ilikua inauzwa 2.5milioni ila sasa imeshuka.
🎲 Software & security
Kitu kikubwa ukimiliki simu za iphone unapata update ya Miaka mingi tofauti na simu za Android ambapo mpaka leo hii simu hii bado inapokea update ya mwaka 2025 na security kwa ujumla hivyo itapokea iOS version 18.7 pia itapokea iOS 26.
🚀 Performance & Hardware 2025
Bado simu hii ukiwa nayo iko poa kuanzia muonekano mpaka ufanisi kwenye Utendaji kamili ambapo ikiwa chipset ya A13 Bionic iko vizuri kwenye gaming , multitasking.
📸 Camera triple lens system ikiwa na 12MP wide , ultra wide yenye kutoa picha Kali kwa wale wapenzi wa photography.
🔋 Hakikisha unaipata betri health 85% iko vizuri sana, kama unahitaji simu ya iphone unaweza tumia hii Kwa mwaka 2025 / 2026.