Je, inawezekana mtu akalala na mwenye UKIMWI tena peku na asipate UKIMWI?

Your case is very very interesting..

I wait for it to be continued
 
Incredible
Austonishing
Flabbergasting
Outstanding.
....juice ya limao kwanzia ni rafiki yangu badala ya pombe.
 
mi ninavyofaham ni kwamba virus wanaishi kwenye blood plasma/umajimaji wa damu, so kushiriki ngono na muathirika kuna probability kubwa ya kuweza kuambukizwa, kwenye hii michezo michubuko inaweza kuwepo au hata katikamate kamaunayekiss naye ana mchubuko basi wajomba watapitia huko huko
 
Nakuomba ndugu yangu inafaa zaidi ungeanza kuusoma huu uzi tokea mwanzo.
 
Hii kitu inaitwa HIV mimi hua naona kama ni laana na si ugonjwa,unachanganya sana huu,kuna watu mke na mume m1 anao mwingine hana,kuna watu wengine wamepima wakakutwa nao lakini mpaka hapa wana miaka zaidi ya 20 wanaishi na wanakufa wenye malalia,huu ni ugonjwa kweli huu!!!!???
 
Kinachoniacha hoi, yaani dawa zake zinaenda kumteketeza mdudu ndani ya seli, hapo unaponaje..mdudu mwenyewe hajulikani kiini macho...na upimaji wake uko tofauti na ugonjwa wowote....cha msingi ni kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha, mazoezi na kupumzisha mwili wako....utosikia ilo lidubwana lakufoji....
 
ARV haziui virusi (cidal) bali huzuia kuongezeka kwao (static)

Kinga yako ya mwili ndio huviua
 
Mkuu,vipi kuhusu mbadilishano wa manii,maana si wote mtafika kileleni kwa maana ya wote kutoa semen
Mkuu nadhani sina uelewa wa kukujibu hapo, nadhani wachangiaji wengine wataweza kujibu.
Manii haziusiani na ukimwi kwa sababu mwanaume huwa anatoa hvyo virusi vya ukimwi haviwezi kupita kwenye bomba la mkojo(urethira)
Pia virusi vya ukimwi haviishi kwenye manii
 
kuna uhusiano kati ya blood transfusion na kuambukizana HIV, yaani anayeweza kukuambukiza ni yule ambaye anaweza kukuongezea damu.
mfano: universal recipient ndio anaweza kuambukizwa hiv na kila mtu
 
MADHARA YATOKANAYO NA ARVS NCHINI YATAFUTIWE UFUMBUZI WA HARAKA


MADHARA yatokanayo na dawa za ARVs kwa baadhi ya watumiaji hapa nchini yanahitaji ufumbuzi wa haraka ili kuweza kuondokana na tatizo hilo.


Hivi karibuni, vyombo vya habari vimeripoti tukio la kusikitisha lilitokea mkoa wa Mtwara kwamba kuna mwanaume anayeishi na virusi vya UKIMWI amebadilika maumbile yake na kuota matiti kama mwanamke katika kifua chake baada ya kuanza kutumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARV).


Alipotoa taarifa kwa daktari aliambiwa hali hiyo ni ya kawaida kwa watu ambao wanatumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo kwa muda mrefu.


Sikika imeguswa na matukio yanayotokana na utumiaji wa dawa hizo na kufuatilia suala hilo kwa ukaribu zaidi. Pamoja na baadhi ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (WAVIU), kutoa taarifa ya kuwa dawa wanazotumia zinawaletea madhara makubwa, bado baadhi wa watoa huduma husika wamekuwa hawachukui hatua yoyote juu ya ubadilishaji wa dawa hizo kwa WAVIU.


Kutokana na taarifa kutoka kwa baadhi ya watumiaji wa dawa hizo wamepatwa na madhara mengi ambayo ni uzito kupungua, mwili kuchoka, miguu na mikono kufa ganzi, mapele, kucha kubadilika rangi kuwa nyeusi na pia baadhi yao kubadilika kimaumbile pindi tu wanapoanza kutumia dawa hizo.


Utaratibu uliopo ni kwamba mtumia dawa hizo anapoona athari zinaanza kutokea anapaswa kutoa taarifa kwa muuguzi wake ili aweze kubadilishiwa dawa nyingine lakini imegundulika kuwa mgonjwa anapotoa taarifa juu ya madhara hayo humchukua zaidi ya miezi sita kabla ya kubadilishiwa dawa na wakati mwingine huambiwa kuwa hali hiyo ni ya kawaida na itaisha.


Sikika pia imegundua kuwa baadhi ya vituo vya kutolea huduma hizo havina mashine za CD4. Kifaa hiki ni muhimu kwa ajili ya kujua maendeleo ya mgonjwa na kutoa ushauri katika kinga za mwili na pia kuendelea na aina ya dawa wanazotumia. Tatizo hili limeendelea kuwa sugu hasa katika maeneno ya vijijini ambapo WAVIU wanalazimika kwenda mwendo mrefu sana kwa ajili ya vipimo vya hivyo. Suala hili limeonekana wazi katika wilaya za Kondoa na Mpwapwa ambapo baadhi ya vituo vya afya havina mashine za CD4.


Vituo hivyo ni Kisese, Hamai, Songolo, Busi na Kwa Mtoro vinavyopatikana wilayani Kondoa na vituo vya afya vya Kibakwe, Rudi, Mima na Pwaga vilivyopo wilaya ya Mpwapwa.Ukosekanaji wa kifaa hiki kwa kiasi kikubwa unachangia mgonjwa kuendelea kutumia aina ya dawa moja ambayo huenda haimfai tena kulingana na CD4 zake kutojua kama zimepanda au zimeshuka.


Sikika inapendekeza kuwa hatua kali zichukuliwe kwa watoa huduma ambao hawafuati utaratibu wa maadili ya kazi zao. Wizara husika pia iwajibike katika kuwasaidia wale ambao wameathirika kutokana na madhara ya utumiaji wa dawa hizo. Mfumo wa sasa wa kusikiliza matatizo ya watumia huduma uimarishwe ili kupunguza athari kubwa zinazotokana na madhara ya kutumia madawa hayo kutokana na wahudumu wengi kutumia lugha chafu.


Pia serikali inapaswa kuweka mashine za CD4 kwenye vituo ambavyo havina na kuzifanyia matengenezo haraka pale zinapoharibika ili zitumike kuwapima wagonjwa maendeleo ya kinga zao za mwili kabla hawajaanza matumizi ya dawa hizo ili kuondokana na tatizo hilo kubwa. chanzo.MICHUZI BLOG: Madhara yatokanayo na ARVs nchini yatafutiwe ufumbuzi wa haraka


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…