Je, inawezekana matumizi ya aina fulani ya pedi yakabadili 'flow' ya damu ya hedhi?

mimi ni mimi

Senior Member
Nov 2, 2012
129
51
Nimekuwa mtumiaji wa pedi hizi aina ya Human Cherish maarufu kama HQ nilitokea kuzipenda kutokana na hali yake ya ubaridi kama Air Conditioner na harufu yake nzuri ya aerobic tea.

Lakini ninahisi pad hizi si salama na zinaweza kuwa chanzo cha matatizo mengi kwa wanawake hapo baadae.

Kwa uzoefu wangu na baadhi ya watu niliowauliza, unapotumia pedi hizi damu hutoka kidogo sana kuliko kawaida na mzunguko humalizika kabla ya siku za kawaida.

Kwa kulithibitisha hili nilibadili aina ya pedi katikati ya mzunguko na damu zikaongezeka kama kawaida na wakati wa kuchange nikatumia HC na flow ikarudi katika hali ya vitone.

Je wahusika wanatuambia nini kuhusiana na tatizo hili la pedi zao? Je usalama wa afya zetu za uzazi utaachwa salama?

f1b279e1e3be8b81c64dbf78f52a13af.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimetumia HC sijaona tatizo lolote , nyuma nilikuwa natumia pad za free style na alwayz yani nilikuwa siponi fungus mara miwasho mara harufu mbaya nikaachana navyo baada ya kutumia hc niko murua na sihami

Sent using Jamii Forums mobile app
kuna always moja ile ambayo pink yake imekolea sana inawasha balaa sijui ni ya nchi gani kuna siku nilivua chupi barabarani
 
Nakubaliana na wewe kabisa. Hata mimi nilishatumia HQ kama mara mbili na zikanibadilishia mzunguko, nikajaribu kufanya research kwa wengine pia ikawa na wao mzunguko hauko sawa. Baada ya kuachana nazo sijakutana tena na hilo tatizo. Labda watengenezaji watuambie sababu ni nini pad zao kubadilisha mzunguko. Maana kwa style hii sio pad nzuri kabisa inapokuja matumizi ya calendar.
 
It's very true.. Mimi nikitumia days zinakua chache na hata utokaji wa damu flow inakua ndogo ukilinganisha ninapotumia pedi aina nyingine. kuna muda unataka kubadili pedi unakuta kitu holla...

halafu zina ubaridi fulani ile ukiivaa unasikia ubaridi wa haja huko chini
 
Back
Top Bottom