Je, inawezekana huyu anatumia bangi?

Nrangoo

JF-Expert Member
May 22, 2017
3,352
5,249
Wadau kwema?

Nipo mbele yenu kuomba kufahamishwa kuhusiana na huyu kijana ambaye nina wasiwasi ameanza kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya ambayo ni bangi.

Cha kwanza.

Kijana kampani yake asilimia 70 nimehakikisha wanatumia bangi.

Cha pili.

Huyu kijana anakula kama mchwa, yani ni kama vile haridhiki na mlo wa sahani moja , na hatumii dakika tatu ashafuta sahani.

Cha tatu.

Kila mara analalamika kuumwa sana kichwa.

Cha nne.

Ana hasira sana, yaani hataki kuelezwa chochote na wazazi hata mtu yeyote aliyemzidi umri, yani kwa kifupi kila analolifanya yeye anaona yupo sawa. Wakati mwingine yupo tiyari kumsukuma mzazi ama kumpiga kabisa

Wadau hizo ni tabia chache ambazo kijana huyu anazo.

Nina fahamu kuna ambao wameshatumia au kuishi karibu na kijana aliye katika matumizi ya bangi. Naomba tusaidiane uhakikisho ili niweze kuchukua hatua thabiti za kumdhibiti.

Pia naomba mnisaidie njia sahihi za kumshughulikia na ikiwezekana aachane kabisa na haya matumizi ya bangi kwani wengi wetu tunafahamu matumizi ya bangi kiafya na kiakili siyo mazuri.

Naomba kuwasilisha.
 
Naomba kuwasilisha...
Ndio.

Anavuta Bange aka anakula Jani aka weed inahusika hapo.
 
Back
Top Bottom