Huyu Msichana nampenda sana, naweza kuishi naye kwa jinsi hivi alivyo?

Boss Man

JF-Expert Member
Feb 10, 2022
458
991
Habari zenu wakubwa kwa wadogo, naombeni mnishauri kabla sijafanya maamuzi, kuna huyu mwanamke huwa ananipenda sana anataka niishi nae, japokuwa hatuna muda mrefu sana tangu tumejuana na Leo ndio ilikuwa mara ya kwanza kunibariki tunda.

Baada ya kufanya nae Mapenzi alionekana kuwa na wasiwasi ya kupata mimba sababu hatujatumia condom na nilivyomuuliza kuhusu mzunguko wake akasema yeye huwa hafuatili, Sasa wasiwasi wake ni kwamba Mimi nitakuwa tayari kuishi nae? ili mtoto apate matunzo ya uhakika (kama ikitokea amenasa lakn) na hataki tena kutoa mimba nyingine kwasababu alishawahi kufanya hivyo na Mimi pia sitaki atoe

Ila Sasa kwangu Binafsi naona huyu Msichana ana vipengele vingi ila ninachompendea huwa hanifichi kitu huwa ni muwazi sana (sijui ni kwangu tu au ndivyo jinsi alivyo)

Kipengele Cha kwanza, Huyu msichana anapenda Gambe, Yani anapenda sana pombe na kutoka out, kama ukimkazia asitoke basi hizo pombe azinywee nyumbani hapo kidogo ataridhika

Kipengele Cha pili, Huyu msichana ni Smoker mzuri tu, Yani bangi kwake ni kitu anachokipenda, Jana tu alikuwa anaongea na simu nikamsikia "Dada unanijua vizuri sidhani kama nitaacha kuvuta bangi" hapo alikuwa anaongea na rafiki yake huwa mara nyingi anapenda kumuita Dada.

Kipengele Cha tatu, Huyu Dada ana tattoos 5 mwilini, 1 ipo kiganjani, 2 ipo kifuani, 3 ipo kwenye Paja, 5 ipo kiunoni kwa nyuma, japo hii ya kiunoni Bado sijaiona ila ameniambia ni Jina lake tu ndio kaliandika

Huyu mwanamke kwao yeye ndio mkubwa ana miaka 21 ana wadogo zake 3 na anaishi na Mama yake na yeye ndio anahudumia familia kwa kiasi kikubwa, Wakati mwingine Hadi namuonea huruma hasa kuna msg amenitumia Leo imeniumiza sana, hiyo ambao nimeizungushia mstari wa red

Kiukweli nampenda huyu msichana na yeye ananipenda ila sasa ndio kama havyo, na kumbuka katika yote hayo anayofanya Mimi sipo katika hata moja

Sinywi pombe, nikinywa basi ni kwakulazimishwa sana na ma bloo au marafiki

Sivuti Bangi na sijawahi kuvuta ila huwa nakaa karibu nawanaovuta Bangi

Sita hata tattoo moja mwilini, na sidhani kama nitachora (but, never say never)

Ni hayo tu Wakuu, naomba experiences zenu kwa wale mliokuwa na Wanawake wa aina hiyo, pengine labda nina hofu nae tu na kumuwazia mambo ambayo hana, au kama ana hayo mambo kuna vile naweza mbadilisha?
Picsart_22-09-28_20-41-01-265.jpg
Picsart_22-09-28_20-42-02-173.jpg
 
Muda mwingine haya ndio madhara ya kuwa na Simu mbili na hauna matumizi nazo ya msingi. Kwa hiyo unaamua kujiongelesha. Kwa hali kama hii ndio maan hata Serikali inataka ianze kutoza tozo kwenye muda wa maongezi, maana suala la kuwa na huduma nafuu za mawasiliano kuna watu linawaathiri kisaikolojia.
 
Nimejiuliza sijapata jibu. Wamefanya kweli hawa au ni ndoto anahadithia?
Sasa naona mnataka nisimulie matukio kuanzia mwanzo wa mchezo Hadi mwisho pamoja na styles zilizotumika, kitu ambacho sio sawa
 
Back
Top Bottom