Je, inawezekana amepata ujauzito?

lovenessy

Senior Member
Aug 20, 2013
105
68
Habari, nina mdogo wangu kaniuliza swali nimeshindwa kumjibu ...

Yeye huwa anaingia katika siku zake tarehe 7 au kumi na mbili sasa tarehe tatu alikutana kimwili ananiuliza atakua hana mimba??

Tarehe saba imepita hajaingia period ..wenye utaalam tafadhali hapo mimba ipo au la?
 
Mwezi uliopita alianza kupata tarehe ngapi.? hesabu siku 11 mpaka 16 kutoka siku hiyo alipoanza mzunguko wa mwezi uliopita, kwa sababu yai hutolewa siku ya 14 ya mzunguko ,hivyo kuna uwezekano kurutubishwa na kutunga mimba endapo mwanamke atafanya mapenzi ndani ya siku 3 kabla au baada ya yai hilo kutolewa yaani siku ya 11,12,13,14,15,16,17.
Kwa kesi yake ninavyoiona uwezekano wa mimba ni mdogo sana.
 
kama hayupo kwenye ndoa mshauri aache zinaa. kama hawezi kuacha basi awe anatumia yale manailoni kujikinga na mimba na mengineyo ili aaikose amani.
 
Haya mambo nimagumu sana haya mambo nimeyasoma pr na sec ila bado yananipiga chenga ujanja kutumia kinga! Na kinga hujisikii ile kitu roho inapenda
 
Haya mambo nimagumu sana haya mambo nimeyasoma pr na sec ila bado yananipiga chenga ujanja kutumia kinga! Na kinga hujisikii ile kitu roho inapenda
Ni vizuri kuelewa mzunguko huo kwa wale walio kwenye ndoa kwani sio rahisi kwao kutumia condom, kuufaham mzunguko huu kutawasaidia kuepuka mimba zisizopangwa.Kwa hiyo ni muhimu kwako pia bro kuelewa ili uweze kupanga vizuri na shemeji.
 
mwezi ulopita alianza tareh 10 trigeminal
Basi uwezekano wa mimba hapo ingekua tarehe 21 hadi 27 kama mzunguko wake ni normal, ingawa kuna wakati irregularities zinatokea kwa sababu ya vitu kama stress,diet,matumizi ya madawa ya kuzuia mimba,disturbance ya level za hormone za uzazi, kwa hiyo ni vizuri akapima tu kujihakikishia
 
Kama anatumia smartphone mwambie aende kwenye store aka-search na kudownload application itakayomsaidia kujua mzunguko wake ulivyo
 
Dada wala usihangaike mpe hongera mama yako mdogo ingawa nahc ni wewe ila hutak kuwa muwaz, jiambie hivi kuwa nina mimba anza maandaliz ya kupokea kiumbe na clinic kwa sana, hongera maelezo ni meng ningekupa ila jua kuwa umenasa vizuri kabisa hongera sana.

Na kwa jinsi unavyouliza ni dhahiri una wasiwasi na haukuwa tayari kupata hiyo mimba! jibu ni kwamba unayo mimba, incase ni mwanafunz wajulishe wazaz wako mapema na aliyekupa mimba. Hongera loveness

ONYO:usifikirie kuitoa hiyo mimb ukithubutu kuitoa utakufa.
 
Hahaha!! Wabongo ni mabingwa wa kusingizia wenzao shida zao, umenifurahisha sana kumwambia ukweli!!
 
Back
Top Bottom