Mkuu Kivule, hiyo uliyopewa ni "offer" ambayo unaweza kuikubali ama kuikataa. Ingawaje si jambo la kawaida kwa muajiriwa kuaminiwa ili apewe madaraka ya juu akakataa, kwa kuwa muajiri atapata mashaka juu uadilifu na uaminifu wako.
Katika hali ya kawaida ukipata madaraka ya juu, huambatana na ongezeko la mshahara na marupurupu mengine. Sasa kwa kukataa kwako ni lazima muajiri wako ataona kuna mgogoro kati ya "personal objectives" dhidi ya "organisational objectives" hali inayopelekea wewe kusimama ktk maslahi yako binafsi, badala ya muajiri kuwa yanapaswa kupewa kipaumbele.
Lakini ktk dhana za menejimenti ya rasilimali watu, ipo ile inayotambulika kama kanuni ya Petro, ambayo ili kutopoteza maana yake kwa lugha ya Kiingereza tunaweza kuinukuu kama ifuatavyo:
The Peter Principle is a concept in management developed by Laurence J. Peter, which observes that people in a hierarchy tend to rise to their "level of incompetence": The underlying fact being employees are promoted based on their success in previous jobs until they reach a level at which they are no longer competent, as skills in one job do not necessarily translate to another.
Pengine hili ndilo linakupa wasiwasi na kutokujiamini. Ondoa mashaka ukijukumishwa zaidi na muajiri wako kuwa tayari kujukumika, kwani kuna faida nyingi za kupandishwa cheo zaidi ya kubaki na cheo kimoja tu kwa muda mrefu.