Je, huyu jamaa ni nani?

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,037
Reaction score
168,688


Mnamo mwanzoni mwa miaka ya 1900 huko Urusi kulikuwapo na jamaa mmoja aliyeaminika kuwa na nguvu za miujiza katika kuponya wagonjwa. Lakini vilevile alionekana kuwa ni mtu mwenye uwezo wa kutabiri.

Uwepo wa jamaa huyo katika falme ya urusi, ulisababisha migogoro kwenye uongozi wa dola hiyo, kitu kilichochochea kupinduliwa kwa aliyekuwa mfalme wa urusi, Tsar Nicholas II

Unajua ilikuwaje?
Jamaa huyo alikuja kupata Umaarufu mkubwa mnamo mwaka 1903, pale alipoingia mjini st Petersburg Na kukutana na familia ya mfalme Tsar Nicholaus II na mkewe Aliyeitwa Alexandra.

Mtoto wa mfalme aliyeitwa Alexei alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa uliyejulikana kama Haemopholia ambao alikuwa akitokwa na damu na damu mfululizo hali iliyomfanya akaribie kufa.

Sasa kwakuwa huyo jamaa alisifika kuwa ni mtu mwenye uwezo wa kuponesha watu kimiujiza ndipo akskutanishwa na familia ya mfalme ili kujaribu kumponesha Alexei..Na kwa bahati mtoto yule alipona mara baada ya kukutana na huyu jamaa.

Mara baada ya tukio hilo, Ikatokea kwamba mke wa mfalme Nicholas II, Aliyeitwa Alexandra alitokea kumshukuru sana na kumthamini jamaa huyo kwa kitendo chake cha kuokoa uhai wa mwanae. Na Hivyo walimwambia aanze kuishi hapo (kwenye makazi ya mfalme) kama shukrani.

Ndipo hapo ukawa mwanzo wa jamaa huyu kuishi 'palace' na familia ya mfalme.
***
Kipindi cha vita ya kwanza ya dunia, Mfalme nicholaus aliondoka urusi na kwenda kwenye viwanja vya mapambano kuvisimamia vikosi vyake vilivyokuwa vinapigana vita.

Sasa huku nyuma, alimuacha mkewe pamoja na jamaa huyo...(kilichotokea sitakielezea hapa, utatafuta mwenyewe kwa muda wako)

Ila kilichochea viongozi wengine wa serikali kuja juu na kupanga njama za kumuua, njia waliyoitumia kujaribu kumuua ni kumuwekea sumu kwenye kinywaji, lakini cha ajabu jamaa huyo sumu ilikuwa haina madhara mwilini kwake...hahah.

Lakini mwisho wa siku walimuua tu kwa njia nyingine, na baadae tukaona Tsar nicholaus na mkewe wanauwawa na kufanya mwisho wa utawala wa kifalme urusi. Na kujulikana kama Mapinduzi ya Urusi ya mwaka 1917.

Je, huyu jamaa ni Nani?

Uzi huu ni kwa HISANI ya Kichwa kikuu
0621002295.
 

Attachments

  • IMG-20180727-WA0011.jpg
    47.9 KB · Views: 93
Last edited by a moderator:
Ndio Huyo kazungumziwa kwenye nyimbo za Abba au bonny em kitu kama hicho. Alipewa sumu ina yoweza kuua farasi?
 
Unasema "kilichotokea huwezi kueleza" unaogopa jamaa atasikia kuwa umetoa siri?
 
Kisa ni kwamba mfalme alikua anamsikiliza jamaa kama vile ni mshauri mkuu wakati alikua ni mdananda tu. Kama Jiwe na Bashite vile. Officials wengine wakapanga kumuu.

Alipewa sumu.
Akasurvive.

Wakamshambulia na mashoka, the guy was so strong, ingawa alikua na sumu mwilini, bado alibingirishana nao.

Wakamfunga wakamtupa kwenye ziwa.

Mwili ulivyokuja kuopolewa uchunguzi ulionyesha kilichomuua ni hyporthemia. Siyo sumu, mashoka wala kipigo ni hyporthemia.

Kama nimechanganya watu mtanisamehe ila ni stori niliisoma zamani sana hata jina nimemsahau.
 
Eti kama stone na empty. Mifano mingine inachekesha sana ingawa inafundisha.
 
NAHUJA Nimepita kumsoma huyo huyo jamaa
Pia inaonyesha hata ntandaoni hawajaonesha kipi kilimtokea yeye na Mke wa mfalme...
Born to a peasant family in the Siberian village of Pokrovskoye, Rasputin had a religious conversion experience after taking a pilgrimage to a monastery in 1897. He has been described as a monk or as a "strannik" (wanderer, or pilgrim), though he held no official position in the Russian Orthodox Church. After traveling to St. Petersburg, either in 1903 or the winter of 1904–5, Rasputin captivated some church and social leaders. He became a society figure, and met the Tsar in November 1905.

In late 1906, Rasputin began acting as a healer for the Tsar and his wife Alexandra's son Alexei, who suffered from hemophilia and was Nicholas' only heir (Tsarevitch). At court, he was a divisive figure, seen by some Russians as a mystic, visionary, and prophet, and by others as a religious charlatan. The high point of Rasputin's power was in 1915, when Nicholas II left St Petersburg to oversee Russian armies fighting World War I, increasing both Alexandra and Rasputin's influence. As Russian defeats in the war mounted, however, both Rasputin and Alexandra became increasingly unpopular. In the early morning of 30 December [O.S. 17 December] 1916, Rasputin was assassinated by a group of conservative noblemen who opposed his influence over Alexandra and the Tsar.

Some writers have suggested that Rasputin helped discredit the tsarist government, and thus helped precipitate the Russian Revolution and the fall of the Romanov dynasty. Very little about Rasputin's life and influence is certain, however, as accounts have often been based on hearsay, rumor, and legend
 
Hauna ya kiswahili, ili na sisi wa la 7 B tusikose ya kusimulia huku kitaa...,[emoji20][emoji20][emoji20]
 
Hauna ya kiswahili, ili na sisi wa la 7 B tusikose ya kusimulia huku kitaa...,[emoji20][emoji20][emoji20]
Hapana mkuu ya kiswahili sijaipata,Labda hayo maneno uyaingize Google translate/S translate japo inaweza kuwa ngumu zaidi usielew kabisa.
 
Kumbe haya mambo ya usaliti ndani ya ndoa yameanza kitambo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…