Je, huyu house boy atakuwa anavuta bangi?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,871
155,837
Ninaishi nje kidogo ya mji ambako nimejenga kanyumba kadogo tu ka kunisitiri.

Ninaishi na mvulana wa kazi ambaye huwa ananisaidia shughuli za nyumbani kama usafi, kuangalia mifugo, kuangalia nyumba nk

Juzi asubuhi nilikuwa natoka, akanifungulia geti, wakati narudisha gari nyuma nikaona analifunga geti, nikamuuliza mbona unafunga geti? Akanijibu nilidhani umeshatoka.

Jana nimechelewa kurudi, nikakaa getini kama dakika kumi, nimepiga sana honi, hakufungua, nikapiga Simu yake akawa hapatikani.

Nikachukia jiwe na kuanza kugonga geti, hatimaye akaja kunifungulia.

Nikaingiza gari ndani, niliposhuka akaanza kunigombeza kwanini namharibia usingizi, akaenda mbali kwa kusema kuwa kuzurura usiku ni tabia mbaya nitakutana na Malaya wanipe ukimwi.

Leo nimerudi jioni hii, ananiambia gesi imeisha hivyo mtungi ameutupa jalalani.

Uzuri ni kwamba jalala liko humu humu ndani ya uzio.

Hivi huyu angekuwa house boy wako ungemwelewaje?
 
Back
Top Bottom