Je huu ni uungwana?

Mwaikibaki

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,993
3,684
Wadau,
Unamkuta mtu mwenye akili timamu kabisa kwa uhuru wake na utashi anakata tiketi ya safari ya bus na kutaka apewe ya dirishani kwa haya mabasi yetu ambayo hawataki kuwasha kiyoyozi.

Jambo la ajabu ni mtu huyu kutokutaka kufungua kioo hata kidogo kuruhusu hewa safi iingie.

Ndugu kama una tatizo la kiafya..au hupendi tu upepo si ungekaa siti ya kawaida? Najua ni haki yako kutumia huduma uliyoilipia ila unachofanya ni simply UZUZU.
Badilika wewe ...magonjwa ..joto etc vimezidi!!!

Wewe mwenye tabia hii nakuambia huu sio uungwana!
 
Mkuu, mtu kuomba kukaa dirishani sio kwa anaumwa au anahitaji hewa ya nje, wenginne nikiwemo mimi huwa tunaka kufanya utalii wa ndani, safari nzima mimi naangalia nje tu, hasa kama nimekaa na watu wakorofi kama wewe.
well and good...ni sawa la utalii wa ndani..vipi.la hewa safi kidogo unaonaje?
 
Kweli mkuu,kuna watu wakikaa dirishana wanakuwa wasumbufu utadhani ni Usafiri wa binafsi lkn wakati mwingine wanaokuwa pembeni wanaweza kuwa wasumbufu pia.
 
Yote tisa umesafir ma mtu mkae nae siti moja mnapofika maeneo yenye stand aagizie mayai ya kuchemsha aanze kuyala aisee mi binafsi huwa yananchefua sana na hayakawii kuchafua hali ya hewa na kama mnaenda mbali ndo kabisa akianza kuachia mashuzi unaweza fika safar hoi
 
Wadau,
Unamkuta mtu mwenye akili timamu kabisa kwa uhuru wake na utashi anakata tiketi ya safari ya bus na kutaka apewe ya dirishani kwa haya mabasi yetu ambayo hawataki kuwasha kiyoyozi.

Jambo la ajabu ni mtu huyu kutokutaka kufungua kioo hata kidogo kuruhusu hewa safi iingie.

Ndugu kama una tatizo la kiafya..au hupendi tu upepo si ungekaa siti ya kawaida? Najua ni haki yako kutumia huduma uliyoilipia ila unachofanya ni simply UZUZU.
Badilika wewe ...magonjwa ..joto etc vimezidi!!!

Wewe mwenye tabia hii nakuambia huu sio uungwana!

Mbaya zaidi mtu mwenye awe hakupiga mswaki asubuhi au hajaoga
 
Nunua gari lako mkuu, uache kutumia usafiri wa umma
ha ha Hii ni case study! wacha kukariri mkuu kuwa kila anayesema tatizo basi anashida.

Siko levo hiyo kabisa gari zipo.Hoja ni ustaarabu na kujitambua ili kuwa na civilized society with less cases of "ego's".
 
Wewe na aliyetoa comment hapo juu, lazima mtakuwa wenye asili ya Ziwa Magharibi
 
huwa wanakera wanaowasha visimu vyao,nyimbo aloweka mbaya basi yan kelele tu sauti kuuubwa,cjui gar au daladala zima tukifanya ivo itakuaje
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom