Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Utakuta mwanamme amempenda mwanamke au amemwambia anampenda. Wakaanza urafiki na urafiki ukakolea na hatimaye "pilau" likaandikiwa siku. Watu wakaja kula na kunywa na kushangilia huku wakiimba "sundasunda" na "anameremeta". Kweli, siku ile ungewaona ungekubali kabisa kuwa wawili hao kweli wamepatana na kupendana. Mapenzi yao yakawa motomoto na mbele za watu joto lake linaweza kuonekana.
Kumbe baada ya kuanza kukaa pamoja na baadaya siku za fungate kuisha ndio ukweli unaonekana. Kwamba, wamejifunga kifungo cha maisha! Kumbe ndoa siyo harusi! Ndoa ni maisha - matamu, machungu, ya furaha na ya kuudhi yote yamo ndani; ndoa kumbe ni kuamka asubuhi na kujikuta umeamka upande ule ambapo "adui yako" mliyegombana jana usiku yupo!
Sasa, mwanamme kwa upande wake anaanza maneno makali na majibizano ya chini chini na vijembe wanaanza kutupiana. Mara siku moja hasira zinapanda sana baada ya kujibiwa vibaya na mke wake mwanamme anaanza kumpiga vibao.
"Nitakupiga kama mbwa leo!" mwanamme anafoka na kweli kupiga ni neno dogo; anambonda kweli kweli.
Mwanamke naye baada ya kichapo anajiambia "kwa kweli nilistahili kwani nilimvunjia heshima mume wangu".
Wanaishia kuombana msamaha na yanakwisha. Kumbe yanasubiri siku nyingine!
Sasa unajiuliza yale mapenzi motomoto waliyokuwa wanapeana na kuambiana yameishia wapi? Yule mwanamme aliyekuwa anakuja na maneno matamu na maua alipotelea wapi? Yule binti aliyekuwa anamaneno matamu na ya furaha ameenda wapi?
Sasa kama hali ni hivyo na kila siku kupigana na kutukanana na wakati mwingine kuumizana - hasa kwa maneno - ni uungwana kweli kuendelea kuwa pamoja? Je kweli ni uungwana kuwaleta watoto katika mazingira kama haya? Je ni wakati gani mwanamke au mwanamme inampasa kuondoka katika mazingira kama hayo?