Amka mapema kabla haujalizwa,ukishaweka hiyo nyumba katika jina la hiyo kampuni kisheria ni ya kwao.
Hi karibuni nilifuatwa na madalali wa nyumba wakiambatana na dalali mwingine mwenye kampuni na 'offer' nono ajabu.
Anachotakiwa mwenye nyumba afanye makubaliana ya awali na huyu dalali kabla kuonana na huyo mbia. Baada ya kudadisi sana nikaambiwa kwamba:
1. Lazima kwanza nyumba hiyo niikabidhi kwa huyo mbia abadilishe hati iwe kwa jina la kampuni hiyo.
2. Iwapo mwenye nyumba anaishi katika nyumba husika, basi atapewa pesa isiyopungua sh. 500m/- kupisha ujenzi wa ghorofa 8 - 10 kwa muda usiozidi mwaka mmoja.
Hayo ni machache kati ya mengi niliyoelezwa na huyo dalali. Nimejiuliza maswali mengi nakosa majibu. Sasa wakuu, naomba mnijuze kuhusu hili jambo.
Nimepata maelezo ya ziada, nitawajuza baada ya muda mfupi.
mkuu, on my views mkataba huo usiingie kichwa kichwa. Tafuta wakili muupitie then akushauri.
Sharti namba tatu la huo mkataba unatia mashaka sana. Huoni kuwa baada ya 20 yrs itakuwa ni issue
kuthibitisha kama kweli hukuliuza eneo hilo? Kumbuka utakuwa umeshasaini malipo ya 300 mil. Huoni pia kuwa hiyo doc. Ya hayo malipo yaweza kuthibitisha kuwa ulishalipwa? Pia uombe mungu wewe mwenyewe uwepo baada ya hiyo miaka ili uthibitishe hayo makubaliano. Maana hutakuwa na hati yenye jina lako!. Mimi naona hizo 300 mil. Ni mtego tu na pengine unaweza kulipwa tu nusu nusu na hapo utakuwa umeshajicommit kwa kusaini mkataba. Mmh pagumu!