Je huu ni ushamba?

Je huu ni ushamba?

asanteelimu2016

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2016
Posts
248
Reaction score
146
Habari zenu

Mwenzenu huwa najisikia aibu sana lakini ni vile nimewahi kuona rafiki yangu akiwa ameibiwa na kibanda cha tigopesa fulani kama laki mbili hivi wakati alipoenda kutoa milioni mbili, hii ikanifanya niwe makini zaidi.

Ni sawa au ni kutokujua au ni ushamba wa mwendokasi NINAPOTOA FEDHA KWENYE ATM ni lazima nizihesabu?

Nimekuwa nikihesabu fedha kila ninapotoa kwenye mashine za atm kuhakikisha kama zimetimia.
 
Nakushauri endelea kuwa na moyo huo huo usimuamini mtu.
Hata ukienda hospitali mwambie daktari akuonyeshe vyeti vyake asije akakuibia.
Ukipeleka mtoto shule wadai walimu wakuoneshe vyeti vyao wasije wakawa hewa.
Na hata ukipanda daladala mwambie dereva akuonyeshe leseni kwanza asije akakuletea ajali.
 
Kwani unatokea Mwanza au Shinyanga? Just playing.

Si ushamba, bali ni umakini.
 
Nakushauri endelea kuwa na moyo huo huo usimuamini mtu.
Hata ukienda hospitali mwambie daktari akuonyeshe vyeti vyake asije akakuibia.
Ukipeleka mtoto shule wadai walimu wakuoneshe vyeti vyao wasije wakawa hewa.
Na hata ukipanda daladala mwambie dereva akuonyeshe leseni kwanza asije akakuletea ajali.
Walimu wenyewe ndo wale wa kule mbeya?
 
Nakushauri endelea kuwa na moyo huo huo usimuamini mtu.
Hata ukienda hospitali mwambie daktari akuonyeshe vyeti vyake asije akakuibia.
Ukipeleka mtoto shule wadai walimu wakuoneshe vyeti vyao wasije wakawa hewa.
Na hata ukipanda daladala mwambie dereva akuonyeshe leseni kwanza asije akakuletea ajali.
 
Hapana wale walikuwa ni wanafunzi wanaosomea shahada ya Ualimu.
Mimi nimezungumzia walimu waliohitimu shahada zao na kuajiriwa.
Lakini hata hao walioajiriwa pia si walikuwa wanafunzi?
mbwa kala mbwa
 
Mi naona ni sawa kuhesabu ni kujiridhisha na nafsi yako.
 
Habari zenu

Mwenzenu huwa najisikia aibu sana lakini ni vile nimewahi kuona rafiki yangu akiwa ameibiwa na kibanda cha tigopesa fulani kama laki mbili hivi wakati alipoenda kutoa milioni mbili, hii ikanifanya niwe makini zaidi.

Ni sawa au ni kutokujua au ni ushamba wa mwendokasi NINAPOTOA FEDHA KWENYE ATM ni lazima nizihesabu?

Nimekuwa nikihesabu fedha kila ninapotoa kwenye mashine za atm kuhakikisha kama zimetimia.
Utafiti unakuhusu
 
ivi kwa mfano siku ukikuta zimepungua utafanyaje sasa
 
Huu Uzi huku si mahali pake labda mimi sijaelewa????
 
Kibinaadam ndio iko hivyo.

Wala si ushamba
 
Back
Top Bottom