Je Huu ni Ukweli Kuhusu Rais Ahmedinejad wa Iran?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Huu ni Ukweli Kuhusu Rais Ahmedinejad wa Iran??

Discussion in 'International Forum' started by Nsololi, Feb 14, 2009.

 1. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2009
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kama ni kweli basi atakuwa ni kiongozi wa Taifa aliye wa kipee. Je, kuna jambo viongozi wetu wanaweza wakajifunza kwake???
   

  Attached Files:

 2. m

  msabato masalia Senior Member

  #2
  Feb 14, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Niaje?
   
 3. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2009
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  du, I feel this dude!!....anatembelea na economy class kwenye ndege ilihali sisi tuliambiwa kuwa tutakula majani ikibidi, mpaka ndege ikanunuliwa!! Kweli kalagabaho sisi.
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hamna kitu hapo..Wananchi wa Iran wana hali mbaya kama kawa..
   
 5. K

  Kjnne46 Member

  #5
  Feb 14, 2009
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtindio:
  1) Jibu swali - "Huu ni Ukweli Kuhusu Rais Ahmedinejad wa Iran?"
  2) Baada ya hapo, tuongezee hayo unayoyadai kama unazo data au picha zake. Usisahau kutuwekea 'Source' - Nsololi katupa ni FoxNewsTV (USA)
  3) Hali mbaya ya wananchi hata Marekani ni hivyo hivyo. Uliziona picha na mambo ya kusikitisha wakati wa Katrina? Hadi leo baadhi ya "wapiga-miyao" bado hawajapata maskani ya kuishi ambapo Bush ndio anapeta na mabilioni ya dola za kustaafu na kuiacha dunia inalalama na eti 'greatest depression'!!
  4) Kwa wale tuliopita Iran na kumwona MAN (Mahmoud Ahmad Nejad) ana kwa ana, hizo picha zimechapishwa chache tu katika maajabu anayoonyesha kwa kuishi maisha ya mtu (MAN) wa kawaida! Lakini Mtindio hawezi kuyasoma au kuyasikia hayo kwani yeye wakweli ni bbc, cnn, voa au dw..
  5) Tunamwombea Mungu ailinde nchi yake asishambuliwe kwa kuendeleza nuclear technology ambayo Wayahudi tayari wanayo lakini hawashutumiwi ..

  Kweli kazi ipo - double standards everywhere!
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160


  Ndg sikulazimishi uone ninayoyaona mimi.

  Labda pata kidogo mtazamo wa watu wengine huenda labda ukaungaunga na kupata habari nzima.

  BBC NEWS | Middle East | Iran economy facing 'perfect storm' .

  Kuhusu raisi huyo wa Irani na maisha yake na hayo mapicha sidhani kama yana maana yeyote kwangu au kwa mtu yeyote mwenye kupenda kuelewa mambo kwa undani. Haya makeke ya kuondoa mazulia mekundu na kujifaragua kuwa hana makuu hata mzee wetu wa 'Uwazi' & 'Ukweli' a.k.a 'Che Nkapa' alianza hivyo pamoja na kutangaza mali zake siku alipoingia mlango wa neema, ila siku zilivyoenda hakutupa tena 'update' ya UKWASI WAKE na kuishia kutoka ikulu 'kimyakimya' akiwa 'amenona'.

  N-way sipingi mtu kuishi anavyotaka(iwe kulala kitanda cha 'shuka tuvute' au 'kwenye full AC Kempinski etc ) ilimradi havunji kanuni na sheria, kitu cha msingi mtu anapopewa dhamana ya kuiongoza nchi kutimiza matarajio ya wananchi wake hususan watu wa kawaida wa hali ya chini.

  Huyu Bw. baada ya kupewa urais kaamua kupeleka mapesa ya nchi kwenye miradi ya kununua ugomvi, na sasa wananchi wake wameshamchoka.
   
 7. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2009
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Ndugu Kjnne46,

  Ahsante ufafanuzi uliompa ndugu Mtindiowaubongo.

  Muhimu ni haya yalioandikwa ni kweli au siyo????

  Kuhusu kupeleka mapesa kwenye miradi ya kununua ugonvi si kweli kwani miradi hiyo ilianzishwa na serikali iliyopita yeye ameikuta tu. Ila la msingi ameunga mkono na kuendeleza miradi hiyo. Tena zuri zaidi rais aliyemtangulia hakuwa wa mlengo wa siasa sawa na huyu wa sasa.

  Pia kuhusu technnology ya Nuclear, watu wasisahau kuwa kuna nchi kama India na Pakstani wanaendeleza miradi hiyo na haohao Wamarekani wanafanya urafiki nao.

  Sasa kwa nini iwe tu kwa Irani??? naomba ieleweka hapa watu tutoe maoni pasipo kuweka motives za dini mbili hizi Ukristo na Uislam.
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ndg Nsololi,

  Kuhusu hayo mapicha kuhusu maisha yake binafsi sidhani kama yana umuhimu wowote, kama nilivyoeleza kwenye post yangu iliyopita.

  Kuhusu mradi wa nuclear, ni wazi huu mradi unaleta madhara kwa raia wake, iwe ameanzisha yeye au ameukuta ukiendelea. Miradi kama hii ni ya gharama kubwa na mbaya zaidi ni kuwa kama makusudio ya miradi hayajakubaliwa na 'wakubwa' ni wazi kinachofuata hapo ni vikwazo vya kibiashara na vingine, na hivyo kuzidi kuyafanya maisha ya mwananchi wa kawaida kuwa magumu zaidi. Sidhani kama unahitaji darubini kuziona hoja hizi.
   
 9. Ngonalugali

  Ngonalugali JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2009
  Joined: Jan 12, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wakuu,

  Hivi wewe uliyeleta mada hii unatala kuniambia kuwa huyu jamaa ni majalala kiasi hicho?
  Sidhani kama ukweli wowote kuhusu hizo picha na hadithi yenyewe.

  Hivi unataka kuiambia jamii kuwa jamaa haishi na familia yake? Mbona mke haonekani?
  Inawezekana vipi jamaa ampige picha huku amelala eti ni ndg yake, hiyo ruhusa kaipata wapi?
  Kwa ujumla naonamauza mauza kwenye habari hiyo.
   
 10. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Jamani this was a fake E-mail in circulation. Hata hiyo aina ya reporting siyo ya Fox News ambao huwa wako so negative kwa Ahmedinejad na Iran.
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Feb 15, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Miradi hayajakubaliwa na 'wakubwa'.... Kwii...! Kwii...! Kwii...! Kwii...! Kwii...!
   
Loading...