Wabongo wenye kusikilizia nini watu wengine wamesema ili mkariri na kukirudiarudia mna kazi! Tatizo la Barça kwa sasa ni mabeki wazuri wenye kasi, basi.. Hiyo habari ya Barça kutokuwa na plani b tulianza kuisikia mwaka ule man u walipopaki basi huko Camp Nou halafu wakawatoa kwa goli la Scholes huko OT. Wanaokariri wakaibuka tena mwaka juzi Inter chini ya Mourinho ilipowatoa. Cha ajabu ni kuwa kila Barça inapotolewa ikirudi inarudi na style ileile na inazikandamiza tena vibaya timu pinzani! Wazee wa kukariri tuambieni, ni kweli kuwa timu zitakazopangwa na Barça CL ijayo zitakuwa na mteremko kwa sababu 'tactic zao hazina maana' na 'zama zao zimeisha?' Timu yoyote itakayocheza mfumo wa 10-0-0 na baadaye 9-0-0 lazima itaisumbua timu pinzani hata ikiwa bora kuliko Barça.